Boris Johnson: Sakata nne zinazomtia matatani Waziri Mkuu wa Uingereza

Boris

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Boris Johnson yuko mashakani

Serikali ya Waziri mkuu wa Uingereza amezama katika mzozo ambao athari zake hazijajulikana ambazo zimepelekea kujiuzulu kwa mawaziri na maafisa wengine wa ngazi ya juu waliodai kuwa wamekosa imani na uongozi wa nchi wa Johnson.

 Msukosuko huo ulianza Jumanne wake, baada ya kashfa ya unyanyasaji wa kingono inayomuhusisha Chris Pincher – mbunge wa Conservative ambaye yuko karibu na Johnson, akiwa Waziri wa uchumi , Rishi Sunak , na Waziri wa afya. Sajid Javid, viongozi wakuu katika serikali, walijiuzuru.

 Sunak alidai kuwa raia wanaitarajia serikali iendeshwe kwa njia "inayofaa, uwezo na kwa umakini "; huku Javid akidai kuwa utawala wa Johnson "haufanyi kazi kwa maslahi ya taifa".

Tangu wakati ule, katika kipindi cha saa 24, zaidi ya maibu mawaziri 40 na maafisa wengine wa ngazi ya juu wamewasilisha barua zao za kujiuzulu.

Jumatano Michael Gove, mjumbe wa muda mrefu wa baraza la mawaziri, alimuomba Waziri mkuu ajiuzulu. Ombi hili baadaye liliungwa mkono na maafisa kadhaa wa ngazi ya juu, akiwemo Waziri wa mambo ya ndani Priti Patel.

 Mawaziri kadhaa muhimu wa nchi hiyo pia walihudhuria makao makuu ya serikali ya Uingereza katika ofisi ya Waziri mkuu 10 Downing Street, ambao waliidhinisha uungaji mkono wao wa kumtaka Jonson aendelee kuwa mamlakani. Hawa ni pamoja na Waziri wa utamaduni,Nadine Dorries, na Waziri wa fursa za Brexit, Jacob Rees-Mogg.

 Kwa upande wake, Boris Johnson anaonekana kupinga uwezekano wa kung’atuka madarakani na badala yake alimuondoa mamlakani Gove, mtu ambaye amekuwa muhimu katika chama cha Conservative kwa muongo uliopita.

''Boris Johnson anataka kuendelea kupambamba .Anaamini ana watu wa kutosha wanaomzingira wanaoweza kumuwezesha kusonga mbele ,"Waziri Dorries alielezea kwa kifupi alipokuwa akiondoka katika makao makuu ya serikali Jumatano usiku.

 Boris amekuwa ni kiongozi Uingereza ambaye amepokea barua za kujiuzulu nyingi zaidi tangu mwaka 1932, alikabiliwa na maswali ya wabunge Jumatano kuhusu utawala wake, ambapo alieleza wazi utashi wake wa kuendelea kubaki mamlakani.

Wito unaomtaka ajiuzulu unakuja mwezi mmoja baada ya Waziri huyo mkuu kukabiliwa na hoja ya kutokuwa na imani naye ambapo 41% ya wabunge kutoka chama chake walipiga kura dhidi yake.

waziri

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Waziri wa uchumi Rishi Sunak alikuwa mmoja wa watu wenye mamlaka zaidi katika baraza la mawaziri

Jaribio hilo la kumg’oa madarakani lilifanyika baada ya picha na ushahidi wa mikutano na sherehe katika ofisi za serikali kubainika kufa vilifanyika wakati serikali yake mwenyewe Boris Johnson ilikuwa imeweka sheria kali za kuzuia mikusanyika wakati wa janga la Covid.

 BBC inajibu maswali muhimu kuhusu mzozo mpya unaotishia kuanguka kwa serikali ya Johnson ... 

1. Chanzo cha mzozo

Tarehe 30 Juni, gazeti la Uingereza The Sun lilichapisha taarifa kwamba aliyekuwa naibu kiongozi wa chama cha Conservative bungeni, Chris Pincher, alikuwa amewatomasa wanaume wawili katika kilabu binafsi mjini London.

Pincher, ambaye alikuwa ameteuliwa na Waziri mkuu Johnson katika mwezi Februari- mwaka huu wakati wa mabadiliko ya baraza la in Februari mwaka huu alijiuzulu mara moja.

Katika kipindi cha siku kadhaa, vyombo vya habari vya Uingereza vilichapisha taarifa kuhusu takribani matukio mengine sita ya madai ya unyanyasaji wa kingono yaliyofanywa na Pinche katika miaka ya hivi karibuni.

Pincher, ambaye alifutwa kazi na chama cha Conservative, ameomba msamaha na alisema atashirikiana kikamilifu na uchunguzi kuhusu mienendo yake na anatafuta, "usaidizi wa kimatibabu ".

2.Boris Johnson anahusika vipi?

Ingawa Waziri mkuu wa Uingereza sio mmoja wa wale waliohusika katika tabia za kingono, sakata ya Pincher inamuweka katika nafasi ngumu kwasababu uwezo wake wa kuamua mambo mema unahojiwa pamoja na uwazi katika namana serikali inavyoshughulikia sakata hiyo.

Chris

Chanzo cha picha, BP MEAN

Maelezo ya picha, Shutuma dhidi ya Chris Pincher zimefungua uwanja mwingine wa mapambano kwa Boris Johnson.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Tarehe 1 Julai, ofisi ya serikali iliwaambia waandishi wa habari kwamba Johnson hafahamu kuhusu madai yoyote dhidi ya Pincher kabla ya kuteuliwa kwake.

Msemaji wa serikloi alisema kuwa Waziri mkuu hakufahamu kuhusu ‘’madai maalumu" kumuhusu Pincher.

Hayo ndio matamshi ambayo wajumbe kadhaa wa baraza la mawaziri waliendelea kuyashikilia katika siku zilizofuata.

 Hatahivyo, tarehe 4 julai, msemaji wa Waziri mkuu alisema kuwa Johnson alikuwa anafahamu "madai kwamba ambayo yalitatuliwa au ambayo hayakuendezwa a kufikia awamu ya malalamiko" na kwamba sio jambo linaloangaliwa kuwa sawa kuzuia uteuzi wa Pincher kwasababu ya "madai ambayo hayana ushahidi."

 Mchana ule ule, BBC ilifichua kuwa Johnson alikuwa amefahamishwa kuhusu malalamiko rasmi kuhusu "tabia isiyofaa " ya Pincher wakati alipokuwa akifanya kazi katika Wizara ya mambo yan je baina yam waka 2019 na 2020.

Malalamiko yalipeleka kufanyika kwa mchakato wa kinidhamu ambao ulithibitisha kuwa tabia isiyofaa ilifanyika.

 Baadaye, katika mahojiano na BBC, Johnson : "Kulikuwa na malalamiko maalumu ambayo yaliletwa kwake .. ulikuwa ni muta mrefu uliopita na yaliletwa kwangu kwa mdomo. Lakini hiyo sio sababu, ningepaswa kuchukua hatua kuyahusu." ".

 Waziri mkuu alielezea kama "kosa" kumteua Bw Pincher, ambaye alisema kuwa alifanya tabia " mbaya, mbaya sana", ambapo aliomba msamaha kwa wale walioathiriwa.

 3. Kwanini wanamuhoji Waziri mkuu?

"Hii yote inahusu kitu kimoja: ukweli," anasema mhariri wa masuala ya kisiasa wa BBC Chris Mason, akichambua mzozo unaoendelea katika serikali ya uingereza.

 "Ukiachana na wimbi la maelezo na shutuma zinazoendelea suala kuu hapa ni kwamba watu wanajiuliza iwapo wanaweza kuamini taarifa zinazotoka katika ofisi ya Waziri mkuu au la ," anaongeza.

 Na ni kwamba jibu la serikali kuhusu Sakata ya Pincher limekuwa likiendelea kubadilika, huku mambo mengine yakijitokeza, kama ilivyojitokeza katika kile kilichoitwa ''partygate'', kisa kuhusu hafla zilizofanyika katika makao makuu ya serikali wakati watu walipokuwa wamewekewa marufuku ya kutoka nje kutokana na virusi vya corona, ambapo hatimaye ilithibitishwa kuwa hata Johnson mwenyewe alihudhuria baadhi ya mikusanyiko hii ya sherehe.

Boris

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kile kilichoitwa 'partygate' kiliharibu sifa ya uaminifu kwa Johnson

Alipoulizwa na mmoja wa manaibu iwapo ataendelea kufanya kazi kama Waziri mkuu "kesho", Johnson alijibu: " bila shaka" .

 Muda mfupi baadaye, Johnson aliwaambia wajumbe wa kamati ya bunge kwamba alikuwa na wiki nzuri sana" na akasema kuwa hawezi kuendesha uchaguzi wa mapema.

4. Nini kinachoweza kutokea sasa?

Kinadharia, kutokana na kwamba alinusurika na hoja za kum’goa mamlakani dhidi yake mwezi uliopita , Boris Johnson analindwa na hoja kama hiyo kwa mwaka mmoja ujao.

 Hii ni kwasababu ilianzishwa na sheria ya sasa ya kamati ya1922, kikundi ambacho kinawaleta pamoja wabunge wa chama cha Conservative cha Uingereza. Hii inaonyesha kuwa hiki ni kipindi ambacho lazima kiishe kabla ya kiongozi wa chama kuhojiwa tena.

Hatahivyo, wakosoaji wa Johnson wanataka kutumia miito ya kurekebisha muongozo huu wa chama wa kamati hiyo kujaribu kuchukua udhibiti wake na kubadili sheria hiyo ili kutoa hoja mpya ya uwezekano wa kumtaka ajiuzuru.

Johnson

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha, Johnson akiwa pamoja na mawaziri wawili wanaoondoka mamlakani , Rishi Sunak (kulia) na Sajid Javid.

Mbunge wa Conservative Andrew Bridgen,mmoja wa wakosoaji wakuu wa Johnson, aliiambia televisheni ya Sky News kwamba anatumai bodi mpya inapendelea kubadili sheria hiyo ili ukomo wa mwaka mmoja uweze kuondolewa kabla ya likizo za msimu wa majira ya joto.

 Alipoulizwa na BBC kuhusu uwezekano wa mabadiliko katika sheria, Sir Graham Brady, ambaye kwa sasa ni mkuu wa kamati ya 1922, alisema kuwa hilo "linawezekana".

 Katika kura iliyopigwa mwezi mmoja uliopita Johnson alipata kura 211 kati ya kura 148 dhidi yake.

 Hatahivyo, hali yake ya kisiasa imezorota katika siku za hivi karibuni kutokana na Sakata ya Pincher kwanza na sasa kujiuzuru kwa serikali yake.

Mbinu nyingine inayoweza kusababisha kuondoka kwa Johnson ni kwa kura ya kutokuwa na imani naye itakayoitishwa na bunge, ambapo wabunge kutoka vyama vyote vya kisiasa wanaweza kushiriki.

Kura hiyo tayari imependekezwa na Liberal Democrats, lakini kwa hilo kuwa sawa itahitaji kuwasilishwa na chama cha Labor na serikali itatakiwa kukubali ijumuishwe katika ajenda za sheria.

Dorries

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Waziri wa utamaduni Nadine Dorries alithibitisha kuwa yuko na Johnson kwa 100%

Pia inawezekana kwamba kujiuzurundani ya baraza la mawaziri kutaendelea ktokea, na kuongeza shinikizo zaidi kwa Johnson kujiuzulu.

 Hatimaye, kuna uwezekano kwamba Waziri mkuu wa Uingereza ataweza kumudu Dhoruba hili la upinzani kama alivyofanya katika mizozo iliyopita ambayo iliikabili serikali, ingawa wachambuzi wanasema muda huo umekwisha.