Boris Johnson: Mawaziri wa zamani waungana kushinikiza ajiuzulu

Chanzo cha picha, Getty Images
Mbunge mwingine wa chama cha Conservative amemtaka Boris Johnson kujiuzulu huku machafuko katika ofisi ya Waziri Mkuu yakiendelea.
Waziri wa zamani Nick Gibb ndiye wa hivi karibuni zaidi kuwasilisha barua ya kutokuwa na imani na waziri mkuu.
Alisema wapiga kura wake walikuwa na hasira kwamba kiongozi mkuu amekuwa "akipuuza waziwazi" sheria za Covid walizoweka wenyewe.
Wakati huo huo, gazeti la Daily Mirror linaripoti kuwa picha ya Bw Johnson akiwa ameshika bia kwenye mkutano wa siku ya kuzaliwa imekabidhiwa polisi wanaochunguza ukiukaji wa sheria za kupambana na ugonjwa wa corona.
Nyaraka hiyo ilisema picha hiyo ni moja ya 300 zilizowasilishwa kwa uchunguzi wa Polisi wa mji juu ya madai ya mikusanyiko 12, picha ambazo inadaiwa zilichukuliwa na mpiga picha rasmi wa Waziri Mkuu, ambaye anafadhiliwa na walipa kodi.
Inasema inaonyesha waziri mkuu akiwa ameshikilia bia katika hafla iliyofanyika Chumba cha Baraza la Mawaziri mnamo mwezi Juni 2020, pamoja na Kansela Rishi Sunak, ambaye alikuwa ameshikilia kinywaji laini.
Wakati huo, mikusanyiko ya zaidi ya watu wawili ndani ilipigwa marufuku na sheria.
Hilo linawadia mwishoni mwa wiki ambayo imekuwa ngumu kwa Waziri Mkuu ambapo hadi kufikia sasa wasaidizi watano wa Baraza la mawaziri wamejiuzulu na kuchapishwa kwa matokeo ya awali ya ripoti ya Sue Gray ya matukio yaliyotokea wakati vikwazo vya Covid vimewekwa.
Akiandika katika gazeti la Daily Telegraph, Bw Gibb, ambaye amehudumu chini ya mawaziri wakuu watatu na ambaye alipoteza nafasi yake kama waziri wa shule katika mabadiliko ya Boris Johnson Septemba iliyopita, alisema wapiga kura wake "walikuwa na hasira kwasababu ya kutokuwa na msimamo mmoja" na kwamba "kurejesha uaminifu, tunahitaji kubadilisha waziri mkuu."
Alisema masharti ya Covid yaliyowekwa na Boris Johnson "yalipuuzwa waziwazi" katika ofisi ya viongozi wakuu na Waziri Mkuu hakuwa sahihi mnamo mwezi Desemba, alipoambia Bunge kwamba hakuna tafrija yoyote.
"Baadhi wanabishana kwamba kula pipi chache na glasi kidogo za vinyaji sio sababu ya kujiuzulu. Lakini kusema ukweli ni muhimu, na hakuna mahali pengine kuliko katika Baraza la Bunge ambapo, kama mahakama ya sheria, ukweli lazima usemwe bila kujali matokeo ya kibinafsi," aliandika.
Bw Gibb alisema mwenzake Tory Aaron Bell "ameshangaza sana" alipomkosoa Bw Johnson kuhusu karamu zilizofanywa wakati kuna vikwazo vya corona mapema wiki hii.
Bw Bell alikuwa amemuuliza waziri mkuu kama alimchukulia kama mpumbavu kwa kufuata sheria mwenyewe - ikiwa ni pamoja na kutokumbatia familia yake kwenye mazishi ya nyanyake, au kwenda kunywa chai baada ya ibada.
Siku ya Ijumaa, Bw Bell alisema "ukiukwaji wa uaminifu" juu ya uvunjaji wa sheria na jinsi ulivyoshughulikiwa ulifanya msimamo wa Waziri Mkuu ushindwe, kwani alithibitisha pia alikuwa amewasilisha barua ya kutokuwa na imani na Sir Graham Brady - mwenyekiti wa mwaka 1922.
Takriban wabunge 54 wanatakiwa kumwandikia Sir Graham ili kuchochea kura kuhusu uongozi wa Waziri Mkuu chamani.
Wabunge wengine wa Conservative wanatarajiwa kutafakari iwapo wataandika barua zao mwishoni mwa juma.
Akizungumza kwenye Newsnight, Mbunge wa Conservative Andrew Bridgen alipendekeza kwamba sasa ni wakati wa baraza la mawaziri" kuonyesha uongozi" na "kukabiliana" na suala la uongozi wa waziri mkuu.
Lakini mbunge mwenzake chamani Richard Bacon alipendekeza kwamba haikuwa kwa wanasiasa kubadilisha serikali - kwa kuwa hiyo ni kazi ya wapiga kura.
Na Liam Fox, katibu wa zamani wa wizara ya biashara, alisema kuna hatari chama hicho kilikuwa kikijihusisha sana na masuala makubwa kama mfumuko wa bei, mzozo wa nishati na hali ya Ukraine.
Alikiambia kipindi cha BBC cha Today programme kwamba: "Kutakuwa na haja ya kumalizwa kwa suala hili, katika Chama cha Conservative na nchini, na nadhani kuna mengi ya kusema, tunapaswa kusema, na kuna maswali ambayo yatahitajika kujibiwa."
Bw Johnson amewaandikia wabunge wote wa chama chake kusema amejitolea kuboresha jinsi ofisi yake inavyofanya kazi.
Katibu wa Utamaduni Nadine Dorries pia alimtetea waziri mkuu, akiambia BBC kwamba alikuwa "chanya sana" alipowasiliana naye ndani ya saa 24 zilizopita.
Alisema kiasi kikubwa cha mabadiliko kilikuwa kinaendelea ndani ya Baraza la Mawaziri lakini alionyesha "tahadhari" na kumtaka abadilike sana, kwasababu ya mafanikio kama vile kuwa na watu wengi zaidi tangu Margaret Thatcher.
Dorries alisema wale wanaozungumza dhidi ya Bw Johnson ni "majina yale yale" ambayo "yanaendelea kujitokeza" na kwamba "hakuna waziri mkuu ambaye angemfurahisha yeyote kati ya hao".
Alisema kuna "sauti chache zinazokuzwa" na vyombo vya habari, akielezea maoni yaliyotolewa na Bw Gibb na Bw Bell kuwa "ya kukatisha tamaa."
Baadhi ya wafuasi wa Bw Johnson, akiwemo waziri mmoja wa zamani wa baraza la mawaziri, wamemkosoa Kansela Rishi Sunak, ambaye wiki hii alijitenga na maoni tata ya waziri mkuu kuhusu Sir Keir Starmer, kwa kukosa uaminifu katika wakati mgumu.












