Tetesi za soka Ulaya Jumamosi: Galatasaray watoa ofa kwa Ederson

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Brazil Ederson
Muda wa kusoma: Dakika 3

Galatasaray wametoa ofa ya euro 3m (£2.6m) kwa mlinda mlango wa Manchester City na Brazil Ederson, 31. (L'Equipe - in French)

Manchester City wanafikiria kumnunua mlinda mlango Muingereza James Trafford, 22, arejee klabuni kutoka Burnley , lakini iwapo tu mmoja wa makipa wao wawili wakuu ataondoka. (Fabrizio Romano)

Kiungo wa kati wa Uholanzi na RB Leipzig Xavi Simons, 22, anapendelea kuhamia Ligi ya Primia, huku Chelsea na Arsenal wakifuatilia hali yake. (Bild -in Germany)

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Darwin Nunez

Barcelona, AC Milan, Al Hilal na Al Nassr wanavutiwa na mshambuliaji wa Liverpool na Uruguay Darwin Nunez, 26 . (Caughtoffside)

Winga wa Colombia na Liverpool Luis Diaz, 28, ameiambia klabu yake kwamba anataka kujiunga na Bayern Munich . Liverpool walikataa kuhusishwa mapema wiki hii. (Florian Plettenburg)

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Marcus Rashford

Jose Mourinho ana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na Muingereza Marcus Rashford, 27, kwa Fenerbahce. (T24 - in Turkish)

Sunderland wamekubali ada ya £17.5m na Sassuolo kwa winga wa Ufaransa Armand Lauriente, 25, 25. (Sky Sports)

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ethan Nwaneri

Kiungo mshambuliaji wa Uingereza Ethan Nwaneri, 18, amekubali mkataba mpya wa miaka mitano na Arsenal . (Telegraph - subscription required)

Tottenham imefanya uchunguzi kumnunua beki wa Bournemouth na Ukraine Ilya Zabarnyi, 22 . (TalkSport)

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rasmus Hojlund

Juventus wanafikiria kubadilishana mkataba wa mshambuliaji wa Manchester United na Denmark Rasmus Hojlund, 22, ili kubadilishana na kiungo wao wa kati wa Brazil Douglas Luiz, 27. (Tuttosport - in Italian)

Ipswich wanatarajia ofa iliyoboreshwa kutoka kwa Brentford kwa mshambuliaji Mwingereza Omari Hutchinson, 21. (Sky Sports)

Norwich wanakaribia kumuuza mshambuliaji wa Marekani Josh Sargent, 25, kwa Wolfsburg kwa £21m. (Sky Sports)