Gyokeres kung'ara EPL?

Maelezo ya video, Nyota wa Sporting Gyokeres alipoifungia Swansea katika Kombe la FA
    • Author, Neil Johnston
    • Nafasi, BBC Sport journalist
  • Muda wa kusoma: Dakika 6

"Sidhani kama ni yeye," Rio Ferdinand anasema kuhusu Viktor Gyokeres.

"Nimemtazama labda mara tatu kweli, kwa karibu sana. Na mara tatu nimefanya hivyo: 'Yeye hawezi kupata fursa hiyo katika ligi ya Premia."

Gyokeres amefunga mabao 97 katika mechi 102 alizocheza akiwa na Sporting, pia ametoa pasi za mabao 26.

Mshambuliaji huyo wa Sweden alifunga wastani wa zaidi ya bao kwa kila mechi msimu uliopita, akiwa na mabao 54 katika mechi 52.

Lakini alipokuwa akihusishwa na Manchester United, Ferdinand alisema hakushawishika kuwa Gyokeres alikuwa anafaa kwa timu kuu katika ligi kuu ya Uingereza.

Mshindi huyo mara sita wa Ligi ya Premia, akiongea kwenye podikasti yake ya Rio Ferdinand Presents, aliuliza: "Je, anatosha - iwapo atakabiliwa akitafuta kupata bao?"

Ingawa mpango huo bado haujakamilika, inaonekana kana kwamba tunaweza kujua msimu huu, huku Arsenal wakiwa kwenye mazungumzo ya kumsajili Gyokeres.

Wamekuwa miongoni mwa vilabu vingi vikuu vinavyohusishwa na mchezaji huyo wa zamani wa Brighton baada ya misimu kadhaa bora akiwa na Sporting, ambapo alicheza chini ya bosi wa United, Ruben Amorim.

Mbali na mabao yake 39 kwenye Ligi Kuu ya Ureno msimu wa 2024-25, Gyokeres alijisaidia kufunga mabao mengine sita kwenye Ligi ya Mabingwa - ikiwa ni pamoja na hat-trick dhidi ya Manchester City.

Ameondoka Brighton bila kucheza hata dakika moja kwenye Ligi ya Premia hadi kuwa mmoja wa wachezaji waliocheza kwa mkopo barani Ulaya - kupitia kwa muda wa mkopo katika michuano ya Swansea na Coventry, na Ujerumani akiwa na St Pauli.

Kwa hivyo Gyokeres alijiimarisha vipi kama mmoja wa wachezaji wanaolengwa katika uhamisho?

Pia unaweza kusoma
A graph illustrating the impact Sporting Lisbon forward Viktor Gyokeres has had in 2024-25

Chanzo cha picha, @OptaAnalyst

Maelezo ya picha, Viktor Gyokeres alimaliza msimu wa 2024-25 Primeira Liga akiwa na mabao 39 - hakuna mchezaji mwingine aliyefikisha 20.

Yule aliyetoroka

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Brighton wamejijengea sifa ya soko la uhamisho - maarufu kwa kukuza vipaji vya vijana na kuwauza kwa ada kubwa.

Mnamo Januari 2019, walimsajili Alexis Mac Allister kutoka Argentinos Juniors kwa ada ambayo haijawekwa wazi, lakini inadaiwa kuwa ni ndogo. Kiungo huyo alifanikiwa kushinda Kombe la Dunia akiwa na Argentina mnamo 2022 kabla ya kujiunga na Liverpool kwa ada ya pauni milioni 55 mnamo 2023.

Kiungo Moises Caicedo alisajiliwa kutoka kwa klabu ya Ecuador ya Independiente del Valle kwa £4m mwaka wa 2021. Miaka miwili baadaye alijiunga na Chelsea kwa mkataba wa rekodi ya Uingereza £115m.

Gyokeres, hata hivyo, ni tofauti.

Akiwa ameshindwa kufuzu daraja hilo, Brighton ilimruhusu ajiunge na Coventry kwa ada ndogo mnamo Julai 2021 baada ya kufunga mabao matatu katika mechi 19 za Ubingwa akiwa kwa mkopo na Sky Blues.

Miaka miwili baadaye alienda Sporting kwa ada ya £20.5m baada ya kufunga mara 38 katika mechi 91 za ligi akiwa na Coventry katika misimu ya 2021-22 na 2022-23.

Akiwa anacheza huko Lisbon, Gyokeres amepanda thamani na sasa anatarajiwa kugharimu takriban £70m.

Pia amecheza kwenye jukwaa la kimataifa kama sehemu ya safu ya ushambuliaji ya Uswidi, pamoja na Alexander Isak wa Newcastle na Dejan Kulusevski wa Tottenham.

Gyokeres anajulikana kwa mchezo wake wa kutumia akili na kasi ya kutamba na mpira, mbali na mchanganyiko wake wa nguvu, ustadi wa kiufundi na ufahamu hali iliomfanya avutie macho ya klabu nyingi.

Yeye ni mtenegenezaji na vile vile mfungaji mabao, huku nafasi nyingi zikiwa zimetokana na kupenda kukimbia na mpira.

Je, Gyokeres ndiye aliyetoroka Brighton ?

"Wachezaji wanakua kwa viwango tofauti," Afisa mkuu mtendaji wa muda mrefu katika klabu hiyo Paul Barber aliiambia The Athletic Novemba mwaka jana.

"Mnamo 2021, wakati Viktor alihamishiwa Coventry, njia yake hapa haikuwa wazi na, pamoja na mkataba wake kumalizika, alitaka nyumba ya kudumu.

"Lazima tukubali uamuzi wa kuuza kwa jinsi ilivyokuwa wakati huo - sawa kwa mchezaji, na kwa klabu.

"Kile Viktor ameendelea kufanya ni kizuri."

'Viktor, toa pasi. Toa pasi '

Wachezaji wenzake na makocha wa zamani wa Gyokeres wanakumbuka mvulana mdogo ambaye alilia aliposhindwa. Wanazungumza kuhusu "mtoto mkaidi" ambaye alikuwa "mtukutu, mkali sana" na mara kwa mara angekutana na wachezaji wenzake.

"Nakumbuka wakubwa wakati mwingine walikuwa wakimwambia atulie kidogo, kwa sababu alikuwa kila wakati," Magni Fannberg, ambaye alimkabidhi Gyokeres mechi yake ya kwanza katika klabu ya Uswidi ya Brommapojkarna mnamo 2015, aliiambia Times.

Kuna hadithi kuhusu Gyokeres kuwa na nia moja, umakini na usimamizi.

Gustav Sandberg Magnusson, ambaye alicheza na Gyokeres pale Brommapojkarna, anaongeza: "Kuna kipindi kimoja cha mazoezi nilikuwa nikimfokea: 'Viktor, pitisha mpira. Toa pasi.' Na hakunitazama nilichanganyikiwa sana.

David Eklund, skauti wa akademi katika klabu hiyo, anaiambia BBC Sport: "Hakuwa nyota kama Dejan Kulusevski. Lakini alifunga mabao. Ni hivyo.

"Alikuwa na mawazo dhabiti lakini ni mtu mzuri sana. Kila mara kazi kwa bidii na alikuwa wazo la kuwa mchezaji bora, akifanya mazoezi kila siku. Alitaka kuwatoa watu makosa."

Dennis Lawrence, ambaye alikuwa sehemu ya kifundi wa kocha Mark Robins wakati Gyokeres alivyokuwa Coventry, anasema: "Ilinibidi nicheke nilipoona alifunga mpira wa adhabu kwa Sporting. Akiwa Coventry, angejaribu mipira ya adhabu [katika mazoezi] na ningesema: 'Hapana, hauko kwenye free-kick, Viktor.'

"Lakini mawazo yake ni, 'hapana, najua ninaweza kufanya hivi'.

Yote yalianza kwenye viwanja vya changarawe vya kilabu yake ya mashinani huko Stockholm, IFK Aspudden-Tellus. Gyokeres alikuwa na umri wa miaka mitano wakati huo na anamshukuru baba yake, Stefan, katika maendeleo yake.

"Kufanya safari hiyo pamoja kulinisaidia sana. Tungeshiriki nyakati nzuri na mbaya," anasema Gyokeres, ambaye tangu wakati huo amekuwa na hisia kubwa - ndani na nje ya uwanja.

Amekuwa nyota wa gazeti la Vogue Scandinavia, ambalo lilimuelezea mchezaji huyo kama "fahari na utukufu" wa soka la Uswidi.

Viktor Gyokeres celebrates scoring for Sporting Lisbon

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sherehe ya kipekee ya Gyokeres anapofunga goli imechochewa na Bane, muigizaji kutoka filamu ya Batman The Dark Knight Rises, na inamhusisha kuweka vidole vyake juu ya mdomo wake, akiiga barakoa.

Je, Gyokeres atastawi kwenye ligi ngumu zaidi?

Tazama orodha ya wafungaji bora katika ligi kuu za Uropa mnamo 2024-25 na wafungaji wa kawaida wapo.

Kylian Mbappe wa Real Madrid alifikisha mabao 31 katika msimu wake wa kwanza wa La Liga, Mohamed Salah alichangia mabao 29 huku Liverpool ikitwaa taji la Ligi Kuu ya England, huku Robert Lewandowski akimaliza akiwa na 27 wakati wa msimu wa kushinda taji la Barcelona - moja zaidi ya nahodha wa Uingereza Harry Kane aliyeifungia Bayern Munich.

Gyokeres, ambaye ana urefu wa futi 6 na inchi 2 (1.89m), alifunga magoli 39, ingawa Primeira Liga haizingatiwi kuwa moja ya ligi tano bora barani Ulaya.

Swali ni kama anaweza kuwa na uwezo mkubwa katika ligi yenye nguvu zaidi. Ametimiza umri wa miaka 27 na bado atacheza mchezo mmoja katika ligi kuu tano za Ulaya - hivyo ndivyo maoni ya Ferdinand.

Labda inafaa kukumbuka kwamba 35% ya mabao yake mnamo 2024-25 yalitokana na mikwaju ya penalti, kwani alifanikiwa kufunga penalti zake zote 19.

Hakuna ubishi kwamba Gyokeres ni mfungaji mabao, lakini je, atakuwa na mafanikio hayo dhidi ya safu zenye kiwango cha hali ya juu?

Toleo la nakala hii lilichapishwa kwa mara ya kwanza mnamo 12 Juni 2025

Pia unaweza kusoma