Alexander Isak: Je, Liverpool itafanikiwa kumsajili mshambuliaji huyu wa Newcastle?

Alexander Isak

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Alexander Isak alijiunga na Newcastle kutoka Real Sociedad 2022 kwa £63m
    • Author, Joe Rindl
    • Nafasi, BBC Michezo
    • Author, Chris Collinson
    • Nafasi, Mtakwimu wa Michezo wa BBC
  • Muda wa kusoma: Dakika 4

Liverpool tayari imetumia zaidi ya pauni milioni 170 msimu huu wa kiangazi - na sasa wanamtaka mchezaji ambaye atawagharimu hela nyingi sana kumsajili.

Alexander Isak wa Newcastle United anakadiriwa kugharimu hadi pauni milioni 130, wakiamua kumsajili basi matumizi yao yatapanda kwa kiwango cha takriban £300m.

Hicho ni kiwango kikubwa sana.

Mabingwa hao wa Ligi ya Premia mwaka jana walitumia £10m kumsajili winga wa Italia Federico Chiesa na £25m kumsajili kipa wa Georgia Giorgi Mamardashvili wakati wa uhamisho wa wachezaji wa msimu wa kiangazi mwaka uliopita.

Liverpool tayari imemsajili kiungo Florian Wirtz kwa kima cha pauni milioni 116 katika kile kinachoonekana kuwa mkataba uliovunja rekodi msimu huu na kulipa pauni milioni 40 na pauni milioni 30 mtawalia kuwasajili mabeki Milos Kerkez na Jeremie Frimpong.

Darubini yao sasa wameilekeza kwa mshambuliaji wa Newcastle Alexander Isak.

Ingawa Liverpool wamejaribu kuwatafuta washambuliaji wengine wa safu ya kati BBC inafahamu kuwa klabu hiyo hivi karibuni imewasilisha ombi la kumsajili Isak.

The Reds pia wameonyesha nia ya kumsajili Hugo Ekitike ambaye juhudi za Newcastle za kumsajili kwa £70m kutoka Eintracht ziliambulia patupu Jumanne wiki hii.

Liverpool pia wamewaulizia wachezaji Yoane Wissa wa Brentford na Ollie Watkins wa Aston Villa wakitanua wigo wao wa kunasa washambuliaji.

Ukizingatia mipango hii yote swali linaloibuka ni je, timu hiyo inayoongozwa na kocha Arne Slot ina uwezo wa kutumia kiwango hicho kikubwa cha fedha kuwasajili wachezaji na kama kweli wana bajeti ya kutumia hela zaidi.

Je, Liverpool wana uwezo wa kumsajili Isak?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mapato ya Liverpool yameongezeka mwaka huu kutokana na mambo kadhaa muhimu.

Walipokea zawadi ya pauni milioni 175 baada ya kushinda Ligi Kuu; msimu uliopita ilikuwa ushindi wa kwanza wa klabu hiyo ikiwa na uwanja wa Anfield uliyopanuliwa na uwezo wa juu zaidi; na kuanzia tarehe 1 Agosti watakuwa na mkataba mpya wa jezi kwa ushirikiano na kampuni ya Adidas ambayo thamani yake inasemekana kwa takriban pauni milioni 60 kwa msimu, ikilinganisha na ushirikiano wao wa sasa na kampuni ya Nike.

Sababu hizo, pamoja na matumizi ya chini katika misimu iliyopita ya uhamisho wa wachezaji, iliifanya Liverpool kujikuta wakiwa katika hali nzuri ndani ya kanuni za faida na uendelevu za Ligi ya Premia (PSR) ambayo inadhibiti matumizi ya klabu kwa pauni milioni 105 katika mzunguko wa matumizi ya miaka mitatu.

"Liverpool ni klabu ya soka ambayo ni makini sana," mtaalam wa fedha wa kandanda Kieran Maguire aliambia BBC Michezo.

"Iko katika nafasi nzuri sana ya kutimiza kanuni ya PSR. Kati ya klabu sita kubwa za jadi, imetumia kiwango kidogo zaidi cha fedha katika mzunguko huu wa miaka mitatu - £325m pekee - na hiyo ni pamoja na kumsajili Florian Wirtz.

"Bado wana nafasi kubwa ya kutumia bajeti yao ya uhamisho bila wasiwasi. Zaidi ya hayo, uhamisho wa mshambuliaji unaweza kulipwa kwa awamu, kumaanisha kwamba malipo yanaweza kufanywa kwa awamu katika misimu kadhaa."

Nafasi yao pia inaweza kuimarika zaidi. Nafasi yao inaweza kuimarishwa zaidi. Siku ya Jumanne walikataa ofa ya awali wa £58.6m iliyowasilishwa na klabu ya Bayern Munich kwa mshambuliaji Luis Diaz.

Licha ya kwamba Liverpool kusema kwamba haina nia ya kumuuza Diaz, tetesi zinaarifu kuwa iko tayari kumuuza Darwin Nunez, ambaye anasakwa na Napoli na klabu za Saudi Arabia.

Klabu gani zingine zinazomuwania Isak?

Newcastle kwa muda mrefu imekariri kuwa wachezaji wake wakuu - hasa Isak sio mmoja wa wale - inapanga kuwauza.

Bila shaka, sawa na Liverpool, Newcastle - ambazo zinamilikiwa na Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi Arabia (PIF) - hazipo katika nafasi nzuri kutimiza masharti ya PSR.

Isak amesalia na miaka mitatu katika kandarasi yake, kwa hiyo Mswidi huyo huenda akashinikiza uhamisho wake.

Mbali na Liverpool, klabu zingine zinazomfukuzia mshambuliaji huyo na ambazo zina uwezo wa kumsajili Isak kwa kima cha pauni milioni 130.

"Arsenal, kama klabu yenye faida kubwa katika historia ya Ligi ya Premia, inaweza kutumia kwa urahisi zaidi ya pauni milioni 200 kuwa usajili bila ya kuwa na hofu ya kukiuka kanuni ya PSR," alisema Maguire.

Licha ya Isak kuhusishwa na uhamisho wa Arsenal, the Gunners wanatarajiwa kufikia mkataba wa Euro milioni 73.5m na klabu ya Sporting (£63.5m) kumsajili mshambuliaji wao Viktor Gyokeres msimu huu wa kiangazi.

Manchester City huenda wasiwe na mpango wa kumsajili mshambuliaji yeyote ikizingatiwa kuwa Erling Haaland na Omar Marmoush wana mikataba ya kudumu.

Huenda ikawa vigumu kwa United kumudu usajili wa Isak bila kuwauza wachezaji kadhaa muhimu, baada ya kushindwa kufuzu kwa ligi ya mabingwa msimu ujao.

Chelsea imewasajili washambuliaji Liam Delap na Joao Pedro katika dirisha hili la ushamisho wa wachezaji.

"Kinadharia, Tottenham huenda ikamudu gharamu ya kumsajili Isak," alisema Maguire. "Lakini suala la iwapo mchezaji angelipendelea kujiunga na timu iliyomaliza katika nafasi ya tano na ile iliyomaliza ligi katika nafasi ya 17 ni hadithi nyingine."

Pia unaweza kusoma:

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi