Wafcon 2024: Zifahamu timu zinazowania nusu fainali

Wachezaji Rasheedat Ajibade wa Nigeria, Racheal Kundananji wa Zambia, Hildah Magaia wa Afrika Kusini na Yasmin Mrabet wa Morocco ni miongoni mwa nyota watakaocheza robo fainali ya Wafcon

Chanzo cha picha, BBC Sport

Maelezo ya picha, Wachezaji Rasheedat Ajibade wa Nigeria, Racheal Kundananji wa Zambia, Hildah Magaia wa Afrika Kusini na Yasmin Mrabet wa Morocco ni miongoni mwa nyota watakaocheza robo fainali ya Wafcon
Muda wa kusoma: Dakika 5

Baada ya awamu ya makundi ya mashindanu ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawake Nigeria, Morocco na Afrika Kusuni zimefuzu kwa robo fainali ya michuano hiyo ambayo inang'o nanga leo Ijumaa..

Hakuna timu iliyoshinda mechi tatu za kwanza, Zambia na Algeria ilijiungana kundi la timu ambazo hazihashindwa, huku Ghana pia wakifuzu licha ya kupoteza mechi yao ya Ufunguzi.

Mali na Senegal ambazo pia zimefuzu kwa robo fainali wako mbioni kuwania nafasi ya timu nne bora zitakazofuzu kwa nusu fainali ya WAFCON.

Ni taifa lipi litacheza dhidi ya nyingine? Je, mechi zitachezwa wapi, lini na makocha wanasemaje kuhusu wachezaji wakutazamwa?

BBC Michezo inaangazia timu nane zilizofuzu kwa robo fainali.

Nigeria vs Zambia (Ijumaa, 16:00 GMT)

Nigeria ambao ni washindi mara tisa hawajawahi kukosa kufika nusu fainali Wafcon lakini kocha Justine Madugu anasema ukame wa mabao unatia "wasi wasi " baada ya kufunga mara moja tu tangu mechi yao ya ufunguzi.

"Hatuna nafasi ya kufanya makoso," alisema Madugu, akiunga mkono timu hiyo ambayo haijashindwa hata mechi moja.

"Lazima tuwe sawakwa 100% - kisaikolojia, kimwili na kiujuzi."

Zambia ilifunga mabao saba na kupoteza manne njiani kufikia hesabu ya Nigeria ya pointi saba, huku washambuliaji Barbra Banda na Racheal Kundananji wakiwa na pointi tatu kila mmoja.

Racheal Kundananji and Barbra Banda wakishangilia bao

Chanzo cha picha, Backpage Pix

Maelezo ya picha, Wachezaji wa Zambia Racheal Kundananji na Barbra Banda

Banda anatumai kuwaiga wanaume wa Zambia, ambao walishinda Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka wa 2012.

"Itakuwa wakati mzuri kwa Zambia," Mwanasoka huyo Bora wa Mwaka wa Wanawake wa BBC aliambia BBC.

"Mwaka huu sasa inaweza kuwa zamu yetu, tunatumai kufikia lengo hilo kama timutimu."

Hata hivyo, kipa wa Nigeria, Chiamaka Nnadozie hajashtushwa na tishio la Banda na Kundananji.

"Nimekuwa nikiwafuatia, nikijaribu kuelewa mchezo wao," nyota huyo wa Super Falcons alisema.

"Kama kipa, unahitaji kutarajia chochote. Niamini, niko tayari kwa ajili yao."

Timu hizo zilikutana kwenye fainali za 2022, wakati Zambia iliposhinda 1-0 na kumaliza nafasi ya tatu.

Morocco vs Mali (Ijumaa, 19:00 GMT)

Ghizlane Chebbak akiwa na wachezaji wenzake wa Morocco

Chanzo cha picha, Backpage Pix

Maelezo ya picha, Ghizlane Chebbak (kushoto) aliiwezesha Morocco kutoka sare dhidi ya Zambia kabla ya mchezaji Bora wa Wafcon 2022 Wafcon kufunga hat-trick dhidi ya DR Congo
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ushindi wa 1-0 dhidi ya Senegal uliifungulia njia Morocco kueleaka fainali kwa kuepuka kukutana na Nigeria na Afika Kusini,

Atlas Lionesses wlaishindwa mara mbili katika mechi zo zote mbili za kwanza dhidi ya Zambia na DR Congo na kocha Jorge Vilda - mshindi wa Kombe la Dunia la 2023 akiwa na Uhispania - alisema wachezaji wake "wana furaha" baada ya mechi yao ya kufanya vyema katika mechi yao ya kwanza ya michuano hiyo.

Mali inatarajia kuwa nahodha Fatoumata Karentao atapona jeraha ambalo lilimlazimu mlinda lango huyo kuondolewa uwanjani wakati wa mechi yao dhidi ya Banyana Banyana ya Afrika Kusini.

Kocha wa Female Eagles, Mohamed Saloum, anasema yeye na wachezaji wake bado wanadhamiria kuendeleza harakati zao za kufuzo kwa nusu fainali mwaka wa 2018.

"Kuanzia robo fainali, tutaona ubora halisi wa timu," alitabiri Saloum, ambaye alichukua jukumu la 2017.

"Tunategemea sana ubora wetu. Hatujali kuhusu changamoto ya kimwili au kitu kingine chochote."

Algeria vs Ghana (Jumamosi, 16:00 GMT)

Ghoutia Karchouni (wa pili kushoto) alifunga bao lililoiwezesha Algeria kujinyakulia nafasi katika robo fainali ya michuano hiyo.

Chanzo cha picha, Shirikisho la Soka Afrika

Maelezo ya picha, Ghoutia Karchouni (wa pili kushoto) alifunga bao lililoiwezesha Algeria kujinyakulia nafasi katika robo fainali ya michuano hiyo.

Algeria ambayo haijashindwa iko katika hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza chini ya uelekezi wa stadi wa Farid Benstiti.

"Sishangai hata kidogo," bosi wa zamani wa Lyon na Paris St-Germain alitafakari, baada ya kuamua kutumia "mbinu ya ulinzi" badala ya kushambulia na kufanikiwa kutoka sare ya 0-0 dhidi ya Nigeria.

"Najua ubora wa wachezaji hawa - ni wajasiri, wazuri sana kiufundi."

Lakini Fennecs bado hawajakubali, Benstiti alikiri kwamba mbinu za kimantiki zinaweza kuhitajika tena wakati wa mechi za mtoano.

"Mkakati ulikuwa mzuri kwa sababu hatukutaka kushindwa," Mfaransa huyo mwenye asili ya Algeria aliongeza.

"Nilijifunza mengi kuhusu timu yangu na itanisaidia ninapoamua kutumia kizuizi kidogo."

Ghana ilimaliza hatua ya makundi kwa kufunga mabao matatu ndani ya dakika 28 za mwisho katika ushindi wao wa 4-1 dhidi ya Tanzania.

Washindi hao mara tatu wanalenga kucheza nusu fainali ya nane na kulipiza kisasi cha kufungwa 2-1 katika hatua ya makundi 2018, wakati Mali ilipofuzu kwa gharama zao.

"Tunajua tuna uwezo wa kwenda njia yote," alisema kocha Kim Lars Bjorkegren.

"[Kuelekea] mwisho wa mashindano, kila mchezo ni kama fainali."

Afrika Kusini vs Senegal (Jumamosi, 20:00 GMT)

Bambanani Mbane playing women's football for South Africa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mchezaji wa Afrika Kusini Bambanani Mbane

Akisaidiwa na mkwaju wa adhabu kutoka kwa nahodha Refiloe Jane, ushindi mnono wa Afrika Kusini dhidi ya Mali ulimwacha kocha Desiree Ellis akisifia uchezaji wa "umahiri" wa timu yake.

Ellis, ambaye ameiongoza timu yake hadi kileleni mwa kundi lao katika michuano mitatu iliyopita, anahofia timu ya Senegal iliyoichabanga DR Congo kabla ya kushindwa kwa bao moja na Zambia na Morocco.

"Lazima tuwe juu ya mchezo wetu... lazima tufanye vizuri zaidi." Ellis alionya.

Wakati wachezaji saba tofauti wameifungia Afrika Kusini, mabao manne ya Senegal yalifungwa na mfungaji bora wa michuano hiyo Nguenar Ndiaye.

"Lengo ni kupita hatua hii muhimu na kufika nusu fainali kwa mara ya kwanza," mchezaji Mame Moussa Cisse alisema.

"Tutaisoma [Afrika Kusini] vizuri na kufanyia kazi sifa na uwezo wao, lakini pia sifa zetu wenyewe kurekebisha kile ambacho hakikuwa kizuri katika hatua ya makundi, ili tufanye vyema."