'Nililazimika kubomoa nyumba yangu' - Wapalestina wanaokabiliwa na ubomoaji Jerusalem Mashariki

- Author, Wyre Davies
- Nafasi, Mwandishi wa Mashariki ya Kati
- Akiripoti kutoka, Jerusalem
- Muda wa kusoma: Dakika 6
Kila alipotembea kando ya magofu ya iliyokuwa nyumba yake, Ahmad Musa al-Qumbar mwenye umri wa miaka 29 alihofia viongozi wa jiji la Jerusalem wangemfuata. Baba huyo wa Kipalestina aliye na watoto wanne alijenga nyumba yake ya ghorofa moja miaka saba iliyopita, kwenye ardhi anayomiliki na ambapo familia yake imeishi kwa vizaza na vizazi.
Lakini Ahmad hakuwahi kuwa na kibali cha kisheria cha kujenga.
Anaishi katika wilaya ya Jabal Mukaber ya Jerusalem Mashariki. Mbele ya Jiji la Kale na makaburi yake mengi ya kihistoria ya kidini, ni mojawapo ya maeneo yenye watu wengi na yenye ushindani mkali katika eneo hilo. Ilitekwa na Israeli kutoka Jordan katika vita vya Mashariki ya Kati vya 1967, na baadaye kuunganishwa, lakini inachukuliwa kimataifa kama eneo la Palestina.
Udhibiti wa Jerusalem ni moja wapo ya masuala yenye utata katika mzozo wa miongo kadhaa. Wapalestina wanadai rasmi Jerusalem Mashariki kama mji mkuu wao, huku Israel ikiuchukulia mji mzima kama mji mkuu wake.
"Nani" anaruhusiwa kujenga "wapi" katika jiji ni sehemu kubwa ya mzozo huo.

Kiwango ambacho nyumba za Wapalestina zinabomolewa katika eneo la Jerusalem Mashariki linalokaliwa kimabavu kimeongezeka maradufu tangu kuanza kwa mzozo huko Gaza, yanasema mashirika ya kutetea haki za binadamu. Amri ya ubomoaji huo imetolewa na mamlaka ya manispaa inayoendeshwa na Israel ambayo inasema kuwa majengo mengi, kama ya Ahmad, yamejengwa kinyume cha sheria bila idhini.
Shirika lisilo la kiserekali la Ir Amim, linasema kwamba Israel "inawaondoa kwa nguvu Wapalestina kutoka kwa makazi yao na jiji" kwa kutumia "vita kama kisingizio" .
"Ilinibidi nibomoe nyumba yangu baada ya kupigwa faini na polisi na mahakama za Israel," Ahmad ananiambia akiwa amesimama kwenye vifusi vya kile kilichokuwa makazi yake.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
"Singeweza kulipa faini na hatari ya kupoteza vitu kama vile huduma ya afya na bima ya mtoto wangu. Tulikata rufaa mahakamani, lakini walikataa.”
Sawa na watu wengine wanaokabiliwa na hali hiyo hiyo, Ahmad alilazimika kukodi tinga na kubomoa nyumba yake mwenyewe. Alisema kuwa mamlaka ya Jiji la Jerusalem ingemtoza faini ya takriban dola100,000 ikiwa wangetekeleza agizo hilo.
Ilichukua hatua hiyo kw amasikitiko makubwa- kubomoa makazi ya familia yake na mustakabali wa watoto wake kwa mikono yake mwenyewe.
Takriban majaribio yote ya familia za Wapalestina huko Jerusalem Mashariki ya kuomba kibali cha kupanga yamekataliwa na mamlaka ya Israeli. Hiyo ina maana kwamba familia zinazokua zinasema hazina chaguo ila kujenga kinyume cha sheria na kukabiliana na athari zinazoweza kutokea - faini kubwa na maagizo ya ubomoaji.
Wengine wanasema sheria na mahakama zinatumiwa kimakusudi kukandamiza ukuaji na matarajio ya Wapalestina.
"Jumuiya hizi za Wapalestina zinaomba ruhusa, na kati ya 95% hadi 99% ya maombi yanakataliwa," anasema Shay Parnes, msemaji wa shirika la haki za binadamu la Israel B'Tselem.
"Haya yamekuwa yakiendelea kwa miaka mingi," Parnes anaendelea.
"Wakati mwingine hutumia sababu za kiusalama kuhalalisha hilo, lakini huwa chini ya mfumo ule ule wa kuwafukuza Wapalestina... kwa sababu sheria ni tofauti kwa jamii tofauti zinazoishi bega kwa bega katika mji mmoja."
Upande wa Magharibi wa jiji wenye sehemu kubwa ya Wayahudi, kile ambacho hapo awali kilikuwa mandhari ya chini ya majengo yenye mawe meupe kimebadilika sana katika miaka ya hivi karibuni. Ujenzi unashamiri. Kreni zinafanya kazi takriban kila siku saa 24 na majengo mapya ya makazi na ya biashara, yanaendelea kujegwa kadiri upande huo wa Jerusalemu unavyopanuka.
Kumekuwa na ujenzi wa kutatanisha, pia, katika baadhi ya maeneo ya Jerusalem Mashariki ambapo ardhi imedaiwa na Israel kutoa nafasi kwa makazi ya Wayahudi. Huko Har Homa, inakadiriwa kuwa watu 25,000 sasa wanaishi katika nyumba mpya zilizojengwa kwenye ardhi iliyonyakuliwa rasmi na Israel mnamo 1991.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kando ya barabara kuna vijiji vya Wapalestina vya Umm Tuba na Sur Baher, ambapo vituo vingi vya umma ni duni kuliko zile vya Har Homa.
Kinyume kabisa na kazi ya ujenzi katika upande mwingine wa barabara kuu, nyumba kadhaa zimebomolewa hapa kwa nguvu katika miaka ya hivi karibuni katika kile Amnesty International inakielezea kama "ukiukwaji wa wazi wa sheria za kimataifa na sehemu ya muundo wa kimfumo wa mamlaka ya Israeli kwa nguvu. kuwaondoa Wapalestina."
Ni picha sawa na hiyo katika makazi ya Gilo, inayopanuka kwa kasi katika kile kinachochukuliwa kimataifa kama Jerusalem Mashariki inayokaliwa, huku, inasemekana, vitongoji vya jirani vya Palestina vinanyimwa uwezo wa kukua kwa kiwango sawa.
Jumuiya ya kimataifa inachukulia makaazi ya Waisraeli katika Jerusalem Mashariki kuwa haramu chini ya sheria za kimataifa, lakini serikali ya Israel inapinga hili. Israel pia inakanusha kuwa ubomoaji ni sehemu ya sera ya makusudi ya ubaguzi ambayo imeshika kasi chini ya kifuniko cha ovyo katika vita vya Gaza.
Katika taarifa, Manispaa ya Jerusalem ilisema tuhuma hizo ni "za uwongo kabisa" na kwamba ilikuwa na msaada wa ndani kwa "mipango kamili ya ujenzi na ujenzi katika karibu maeneo yote ya Jerusalem Mashariki".
Mipango hiyo "inalenga kutoa chaguzi za upanuzi wa kitongoji, kushughulikia suala lililoenea la ujenzi haramu, na kutenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa miundo ya huduma za manispaa," iliongeza.
Lakini si vigumu kupata mifano ambapo amri za ubomoaji wa Israel dhidi ya nyumba za Wapalestina zinatekelezwa kote Jerusalem Mashariki.

Juhudi za familia za Wapalestina kuomba kibali cha kupanga huko Jerusalem Mashariki zimekataliwa na mamlaka ya Israel. Hiyo ina maana kwamba familia zinazokua zinasema hazina budi kujenga kinyume cha sheria na kukabiliana na athari zinazoweza kutokea - faini kubwa na maagizo ya ubomoaji.
Wengine wanasema sheria na mahakama zinatumiwa kimakusudi kukandamiza ukuaji na matarajio ya Wapalestina.
"Jumuiya hizi za Wapalestina zinaomba kibali cha kujenga au kupanga kwa kati ya 95% hadi 99% lakini maombi yanakataliwa," anasema Shay Parnes, msemaji wa shirika la haki za binadamu la Israel B'Tselem.
"Haya yamekuwa yakifanyika kwa miaka mingi," Parnes anaendelea.
"Wakati mwingine hutumia sababu za kiusalama kuhalalisha hilo, lakini huwa chini ya mfumo ule ule wa kuwafukuza Wapalestina... kwa sababu sheria ni tofauti kwa jamii tofauti zinazoishi bega kwa bega katika mji mmoja.''

Katika tathmini ya kina ya sera, Ir Amim aligundua kuwa tangu kuzuka kwa vita vya Gaza mnamo tarehe 7 Oktoba 2023, "kueshuhudiwa ongezeko la kasi ya kukuza na kufuatilia kwa haraka mipango mipya ya makazi huko Jerusalem Mashariki sambamba na ongezeko la kiwango cha ubomoaji wa nyumba za Wapalestina".
"Ni wazi Israel inatumia vita kuimarisha makazi yake," inaendelea.
Inakadiriwa kuwa kuna takribani 20,000 ya ubomoaji yaliyosalia katika Jerusalem Mashariki - maagizo ambayo hayana kikomo cha kuisha.
Baadhi ya wachambuzi wanahisi kwamba tangu tarehe 7 Oktoba, wanachama wa siasa kali za mrengo wa kulia wa serikali ya Benjamin Netanyahu na katika Manispaa ya Jerusalem wamekuwa na ujasiri zaidi katika kueleza hadharani nia yao kuhakikisha nyumba nyingi za Wayahudi zinajengwa kwenye ardhi inayokaliwa au kugombaniwa.
Wakati Wapalestina, kama familia za Ahmad na Lutfiyah, wanahofia kupoteza makazi yao, wanasisitiza kwamba watabaki na hatimaye kuanza upya maisha yao hapa Jerusalem Mashariki.
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi












