Matukio maarufu ya mvutano katika msikiti wa Al-Aqsa

Chanzo cha picha, REUTERS
- Author, Muhannad Tutanji
- Nafasi, BBC
Israel iliwauzia waumini wa Kiislamu kuingia katika eneo la Msikiti wa Al-Aqsa baada ya shambulio la Hamas mnamo Oktoba 7.
Kila siku ya Ijumaa, ni wazee pekee ndio walioruhusiwa kuingia na kusali, huku vijana wakiswahi katika mitaa ya Jiji la Kale.
Wiki chache kabla ya mwezi wa Ramadhani, Israel ilianza kuruhusu karibu kila mtu kuingia katika eneo la Msikiti Mtakatifu, isipokuwa wale ambao iliwazuia kupitia maamuzi ya polisi, au kupitia maamuzi ya mahakama na usalama.
Israel inawezaje kudhibiti wanaoingia?
Msikiti wa Al-Aqsa uko ndani ya kuta za Mji Mkongwe huko Jerusalem Mashariki, ambao Israel iliudhibiti mwaka 1967 baada ya kuwa chini ya utawala wa Jordan.
Mikataba iliyotiwa saini iliruhusu Idara ya Wakfu ya Kiislamu ya Jordan kusimamia maeneo matakatifu, haswa eneo takatifu kwa Waislamu. wa Patakatifu pa Patakatifu.
Waislamu waliruhusiwa kuingia na kuswali ndani ya kuta za msikiti, huku Wayahudi wakiingia na kuswali katika eneo la Ukuta wa Magharibi wa Msikiti wa Al-Aqsa.
Polisi wa Israel husimama kwenye lango la kuingilia kwenye eneo la msikiti bila kuingilia maamuzi ya watu kuingia. Huku walinzi wa Idara ya Wakfu za Kiislamu wakisimama upande wa ndani.
Baada ya 2003, kwa uamuzi wa serikali yake, Israel ilianza, kuruhusu ziara za Wayahudi chini ya ulinzi wa polisi kwenye eneo la msikiti huo, kwa kile kilichoitwa ziara za kitalii.
Kwa miaka mingi, polisi wa Israel wamehusika katika maamuzi ya kufunga na kufungua milango ya Msikiti na kuweka vikwazo wakati wa matukio ya wasiwasi.
Ni matukio gani maarufu ya mvutano?

Chanzo cha picha, REUTERS
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Waziri wa Usalama wa Taifa wa Israel Itamar Ben Gvir aliingia katika viwanja vya msikiti mara kadhaa mwaka 2023, muda mfupi baada ya kushika wadhifa wake katika serikali ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
Mwaka 2021, vita vilizuka kati ya Israel na vikundi vya Wapalestina huko Gaza kutokana na vurugu lililotokea katika viwanja vya msikiti huo.
Wakati huo, polisi wa Israel walivamia eneo linalojulikana kwa jina la Msikiti wa Al-Qibli na kufanya kampeni kubwa ya kuwakamata watu kwa kutumia nguvu.
Picha za video zilirekodi matukio ya waumini wakipigwa, na kujeruhiwa, kama ilivyothibitishwa na shirika la msaada la Hilali Nyekundu ya Palestina.
Polisi wa Israel walisema maafisa wao kadhaa pia walijeruhiwaIlikuwa ni. siku ya Ijumaa ya mwezi wa Ramadhani na kupelekea kuzuka kwa makabiliano makubwa yaliyojumuisha maeneo yote ya Palestina na kuenea hadi katika miji ya Waarabu ya Israel.
Mwezi wa Ramadhani wa 2017, polisi wa Israel walifunga milango ya kuelekea kwenye eneo la Msikiti na kuzuia kutekelezwa kwa swala.
Milango ya kielektroniki na vigunduzi viliwekwa ili kuwapekua waumini kabla ya kuingia.
Hayo yalijiri baada ya kuuawa kwa maafisa watatu wa polisi wa Israel, wakati wa operesheni iliyotekelezwa na vijana wa Kipalestina kwenye lango la msikiti, na wao waliuwawa.
Kampeni zilizoenea katika mji wa Jerusalem zilipelekea milango hiyo kuondolewa.
Mwaka 2014, ulishuhudia makabiliano mengine kati ya Israel na makundi ya Wapalestina huko Gaza, Israel ilizuia kuingia kwa waumini katika misikiti kwa siku kadhaa wakati wa mwezi wa Ramadhani, ikiwa ni pamoja na Ijumaa.
Waliruhusiwa wale walio na umri wa zaidi ya miaka 50, kama sehemu ya kile polisi walichoita wakati huo "maandalizi ya usalama kwa kuhofia mashambulizi kutokea Jerusalem."
Mwaka wa 2000, ilishuhudia kuzuka kwa kile kinachojulikana kama “Intifada ya Al-Aqsa,” au Intifada ya Pili ya Palestina, vurugu zilizotokana na kuingia Waziri Mkuu wa zamani Ariel Sharon kwenye eneo la Temple Mount.
Kufuatia vurugu, Israel ilianzisha operesheni ya kijeshi inayoitwa "Ukuta wa Kujihami" katika maeneo yote ya Wapalestina.
Makundi yenye silaha ya Kipalestina yalianzisha operesheni katika miji kadhaa ya Israel, na katika mazingira hayo, vizuizi viliwekwa kwa wanaotaka kuingi Al aqsa.
Viwanja vya Msikiti wa Al-Aqsa viko ndani ya kuta za Mji Mkongwe wa Jerusalem Mashariki, ambao kwa mujibu wa sheria za kimataifa unachukuliwa kuwa eneo linalokaliwa kwa mabavu na Israel, sawa na Ukingo wa Magharibi.














