Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumapili: Man City wanamtazamia Wirtz kuchukua nafasi ya De Bruyne
Manchester City wamemtambua kiungo mkabaji wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Florian Wirtz, 21, kama mchezaji mbadala bora wa kiungo wa Ubelgiji, 33, Kevin de Bruyne. (Fabrizio Romano)
Manchester City wako tayari kutumia £100m kumsajili Wirtz, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Bayern Munich kuwania saini yake. (Sunday Mirror)
Manchester United , Nottingham Forest , Juventus , na Bayern Munich wote wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Jean-Philippe Mateta, 27 kutoka Crystal Palace msimu huu. (TeamTalk)
Aston Villa wametiwa moyo na Chelsea kuhusu mpango wa kumsajili winga wa Uingereza Noni Madueke, 23, huku mchezaji huyo akiwa hana furaha kwa kukosa muda wa kucheza Stamford Bridge. (Football Insider)
Wakala wa mshambuliaji wa Sporting Viktor Gyokeres atakuwa kwenye mechi ya Arsenal ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid, jambo linalochochea tetesi kwamba mshambuliaji huyo wa Sweden mwenye umri wa miaka 26 yuko tayari kujiunga na The Gunners. ((Football Transfers))
Liverpool na Manchester City wanafuatilia hali ya kandarasi ya mshambuliaji wa Barcelona Lamine Yamal lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania mwenye umri wa miaka 17 anaonekana kusalia na klabu hiyo ya Catalan. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Barcelona itafikiria mpango wa kubadilishana wachezaji utakaomhusisha beki wa kati wa Uruguay Ronald Araujo, 26, na winga wa Liverpool mwenye umri wa miaka 28 wa Colombia Luis Diaz. (Relevo - in Spanish)
Arsenal wametajwa kufanya usajili wa wachezaji watano msimu wa majira kiangazi sasa mkurugenzi mpya wa kandanda Andrea Berta ndiye anayeongoza. (Guillem Balague kupitia TNT Sports)
Manchester City wanatumai kumsajili winga wa Aston Villa Morgan Rogers, 22, huku Pep Guardiola akimpenda sana mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, ambaye hapo awali alikuwa katika akademi ya City. (TeamTalk)
Aston Villa wanafikiria kuuza timu yao ya Ligi ya Wanawake ya Super League (WSL) kwasababu ya hofu kuwa wanaweza kukiuka kanuni za faida na uendelevu za Ligi ya Premia (PSR). (Times - subscription required)
Uamuzi wa Alejandro Garnacho kuweka nyumba yake kuuzwa si kwa sababu winga huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 20 anapanga kuondoka Manchester United . (Mirror)