Mzozo wa Tigray: Wakazi wa Tigray waagizwa kujilinda dhidi ya jeshi la Ethiopia

Tigray special forces in federal military uniforms

Wakazi wa Ethiopia kaskazini mwa Tigray wameagizwa kujikusanya na kujilinda dhidi ya serikali kuu kwa kile wanachokiita uchokozi mbaya kutoka kwa serikali.

Hofu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe inaendelea kutanda miongoni mwa wananchi.

Awali, Waziri Mkuu Abiy Ahmed alikataa ombi la mazungumzo ya amani kutoka mamlaka Tigray.

Inasemekana kwamba mamia ya watu wameuawa katika mapigano ambayo yametokea siku nane zilizopita kati ya vikosi vya Tigray na jeshi.

Chama ambacho awali kilikuwa na nguvu cha Tigray People's Liberation Front (TPLF) ambacho kilitawala eneo la Tigray kimekuwa kikizozana na Waziri Mkuu Abiy tangu alipoingia madarakani mwaka 2018 na kuahidi mabadiliko kote nchini humo.

Hivi karibuni, chama cha TPLF kilikanusha marufuku ya uchaguzi iliyowekwa kwa sababu ya virusi vya corona.

Bwana Abiy alijibu kwa kusema uchaguzi huo sio halali.

Serikali ya Tigray imesema nini?

TPLF ilitangaza hali ya hatari "ikitetea usalama wa watu wa Tigray na eneo lao", kituo cha televisheni kinachomilikiwa na serikali ya Tigray limesema.

Serikali ya Tigray imesema nini?
1px transparent line

Mamlaka ya eneo imekuwa ikishutumu nchi jirani ya Eritrea mara kadhaa katika mgogoro wake, hatua ambayo Eritrea na serikali kuu wamekanusha.

Hata hivyo, serikali kuu inasisitiza kuwa vita vyao ni dhidi ya serikali ya eneo hilo- wala sio watu wa Tigray.

Wakati huohuo, Umoja wa mataifa imeonya kwamba huenda msaada wa kibinadamu unaisha.

Misaada ya kibinadamu muhimu kwa maelfu ya watu kaskazini mwa Ethiopia wako katika hatari kwasababu ya mapigano yanayoendelea Ethiopia, afisa wa Umoja wa Mataifa amesema.

"Kunasemekana kwamba kuna ukosefu wa bidhaa muhimu kama vile unga na mafuta," Mkurugenzi UN nchini humo Catherine Sozi ameiambia BBC.

Mapigano kati ya Tigray na serikali yalitokea siku nane zilizopita.

1px transparent line