Mkenya Manvir Singh ashinda mbio za magari za milimani Rwanda

Mashindano ya magari

Manvir Singh Baryan, dereva kutoka Kenya ndiye aliyeibuka na ushindi wa mashindano ya kimatifa ya mbio za magari ya Rwanda Mountain Gorilla na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwa bingwa wa Afrika wa mbio za magari.

Singh alitamba tangu mwanzo hadi mwisho wa mashindano haya akitumia muda wa saa 1 na dakika 47 katika barabara zenye urefu wa km zaidi ya 200 upande wa mashariki mwa Rwanda.

Gari lake aina ya Skoda lenye thamani ya dolla laki 2 na themanini elfu likipisha nguvu magari mengine.

Magari 16 yalishirikisha mashindano haya,lakini mwishowe yakamaliza magari 4 tu.

Mbio hizi ni mkondo wa 6 kwenye kalenda ya mashindano ya mbio za magari barani Afrika.

Dereva huyo anahitaji alama moja tu kutoka kwa mashindano yatakayofanyika Zambia ambayo ndiyo ya mwisho, akiwa anahitaji alama moja tu ili kutawazwa bingwa wa Afrika.

Gari linaloshiriki mashindano
Madereva