Wanahabari watano kati ya 20 wauawa katika shambulizi la Israel hospitalini - maafisa wa Gaza
Jeshi la Israel linasema lilifanya shambulizi katika eneo la Hospitali ya Nasser na "inajutia madhara yoyote kwa watu wasio husika na vita na kuwa hawalengi waandishi wa habari".
Muhtasari
- Jinsi shambulizi lilivyotokea kama lilivyonaswa moja kwa moja
- Je, tunajua nini hadi sasa kuhusu waandishi wa habari waliouawa katika mashambulizi?
- Arsenal wanataka kumsajili beki wa Bayer Leverkusen Piero Hincapie
- Israel inasema itapunguza wanajeshi nchini Lebanon ikiwa itachukua hatua za kuwapokonya silaha Hezbollah
- Ukraine yaonyesha kombora jipya linalodhaniwa kuwa la Neptune
- Mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na nchi za Ulaya "kufanyika Geneva siku ya Jumanne"
- Saka kukosa mechi kwa wiki nne kwa jeraha
- India itanunua mafuta itakapopata 'kwa bei nzuri', balozi wa nchi hiyo Urusi amesema
- Takriban watu wanane wauawa katika shambulizi la Israel kwenye hospitali ya Gaza, wizara ya afya yasema
- M23 yaituhumu serikali kwa kutumia mamluki wa kigeni katika mashambulizi yanayoendelea
- Vikosi vya wanamgambo vya Sudan vyaongeza mashambulizi ili kudhibiti jiji la al-Fashir
- Warundi wajitokeza kwa wingi kuchagua viongozi wa vijiji na mitaa
- Idadi ya vifo yaongezeka Sanaa baada ya mashambulizi ya anga ya Israel
- Hamas yaishutumu srael kwa "kuchelewesha na kukwepa mambo ," huku idadi ya vifo karibu na vituo vya misaada ikizidi 2,000
- Wanajeshi wa kikosi cha taifa Marekani kubeba silaha Washington kuzuia uhalifu
- Kadi ya kumbukumbu ya Michael Jordan na Kobe Bryant yauzwa kwa rekodi ya dunia
- Mashambulizi ya Ukraine huko Urusi yapandisha bei ya mafuta duniani
- Mashambulizi ya Ukraine huko Urusi yapandisha bei ya mafuta duniani
Moja kwa moja
Na Mariam Mjahid & Asha Juma
Jinsi shambulizi lilivyotokea kama lilivyonaswa moja kwa moja

Chanzo cha picha, Alghad TV
Maelezo ya picha, Wafanyakazi wa dharura na waandishi wa habari wakiwa kwenye ngazi kabla ya shambulizi la kuanza Na Shayan Sardarizadeh na Benedict Garman
Tumethibitisha video kadhaa za picha zinazoonyesha mashambulio mawili ya Israel kwenye Hospitali ya Nasser huko Gaza, na kuua waandishi wa habari.
Video moja, iliyonaswa moja kwa moja na Al Ghad TV, inaonyesha wafanyikazi kadhaa wa dharura wakijibu shambulizi la kwanza karibu na orofa ya juu ya Hospitali ya Nasser, huku waandishi kadhaa waliokuwa nyuma wakinasa tukio hilo.
Eneo lililo na ngazi, ambapo waandishi wa habari mara nyingi hukusanyika kupiga picha kote Khan Younis, linaonekana kwenye video. Kisha shambulizi linatokea moja kwa moja pale walipo wafanyikazi wa dharura na waandishi wa habari, huku moshi na vifusi vikionekana hewani. Takriban mwili mmoja unaonekana katika eneo la tukio.

Chanzo cha picha, Al Ghad TV
Maelezo ya picha, Televisheni ya Al Ghad ilionyesha wakati shambulio la pili linatokea na moja kwa moja hewani Video tofauti, iliyorekodiwa kutoka kwa ngazi hiyo hiyo, inaonyesha athari za shambulio hilo. Miili kadhaa inaweza kuonekana kwenye ngazi, huku madaktari wakijibu shambulio hilo.
Video nyingine, iliyorekodiwa mbele ya lango kuu la hospitali ya Nasser, inamuonyesha mhudumu wa afya akiwa ameshikilia nguo zilizokuwa na damu kwenye kamera, kabla ya mlipuko kufanya watu watawanyike kwenda kujificha.
Video iliyorekodiwa nje ya hospitali hiyo, inaonyesha moshi ukifuka kutoka orofa ya juu, huku waandishi wa habari wakipiga picha na kutangaza kuwa hospitali ya Nasser imeshambuliwa "kwa mara nyingine tena".
Soma zaidi:
Je, tunajua nini hadi sasa kuhusu waandishi wa habari waliouawa katika mashambulizi?

Chanzo cha picha, AP
- Hussam al-Masri alifanya kazi kama mpiga picha Reuters. Shirika la habari liliripoti kuwa aliuawa katika shambulizi la kwanza hospitalini
- Mariam Dagga, 33, alikuwa mwandishi wa habari wa kujitegemea anayefanya kazi na Associated Press (AP)
- Mohammed Salama alifanya kazi Al Jazeera na Middle East Eye
- Ahmad Abu Aziz alifanya kazi na Middle East Eye, kulingana na ripoti yake yenyewe. Kituo hicho kinasema alifanya kazi kwa kujitegemea na alikuwa na makao yake huko Khan Younis
- Bado hatuna uthibitisho wa kituo alichokuwa akifanya kazi Moas Abu Taha - Mtandao wa TV wa Marekani NBC ulisema Taha hakufanya kazi nayo kama ilivyoripotiwa awali.
Soma zaidi:
Arsenal wanataka kumsajili beki wa Bayer Leverkusen Piero Hincapie

Chanzo cha picha, Getty Images
Gunners wanataka beki wa kushoto kama kipaumbele msimu huu wa joto, huku mchezaji wa kimataifa wa Ecuador, Hincapie akiibuka kama mchezaji mwenye nguvu.
Wafanyakazi wa Arsenal wamemtazama kwa makini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, vyanzo viliiambia BBC Sport.
Hincapie ana kipengele cha kutolewa euro 60m (£52m) na anataka kuondoka klabu hiyo ya Ujerumani kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Amecheza mechi 166 katika michuano yote akiwa na Leverkusen tangu ajiunge nayo 2021 na alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda Bundesliga na Kombe la Ujerumani mnamo 2023-24.
Arsenal wametumia zaidi ya £200m kununua wachezaji wapya msimu huu wa joto na sasa wanafanya kazi ya kuuza wachezaji - huku Fabio Vieira, Reiss Nelson na Oleksandr Zinchenko wakiwa miongoni mwa wale wanaoweza kuondoka.
Pia kumekuwa na nia ya kumnunua beki wa kati Jakub Kiwior, huku Porto wakiwa miongoni mwa vilabu vinavyomtaka.
Tottenham pia wamekuwa wakihusishwa na kutaka kumnunua Hincapie, lakini vyanzo vinasisitiza kuwa yeye si mchezaji ambaye Spurs wanamfuatilia kwa sasa.
Soma zaidi:
Israel inasema itapunguza wanajeshi nchini Lebanon ikiwa itachukua hatua za kuwapokonya silaha Hezbollah

Chanzo cha picha, Reuters
Israel imeashiria kuwa itapunguza uwepo wake wa kijeshi kusini mwa Lebanon ikiwa wanajeshi wa Lebanon watachukua hatua ya kuwapokonya silaha wanamgambo wa Kishia wa Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran.
Tangazo hilo kutoka kwa ofisi ya waziri mkuu wa Israel limekuja siku moja baada ya Benjamin Netanyahu kukutana na mjumbe wa Marekani Tom Barrack, ambaye amekuwa akihusika pakubwa katika mpango wa kuwapokonya silaha Hezbollah na kuwaondoa wanajeshi wa Israel nchini Lebanon.
"Ikiwa Vikosi vya Wanajeshi wa Lebanon vitachukua hatua zinazohitajika kutekeleza upokonyaji silaha wa Hezbollah, Israel itashiriki katika hatua za kuafikiana, ikiwa ni pamoja na kupunguzwa kwa shughuli za jeshi la Israel," ofisi ya waziri mkuu wa Israel alisema.
Taarifa hiyo haikusema wazi iwapo majeshi ya Israel yatajiondoa kikamilifu katika maeneo matano waliopo Lebanon.
Jeshi la Israel limedumisha uwepo wake kusini mwa Lebanon karibu na mpaka tangu kukubaliana na Marekani kusitisha mapigano na Hezbollah mwezi Novemba.
Israel ilikuwa iondoe majeshi yake ndani ya miezi miwili na wanajeshi wa Lebanon walipaswa kuchukua udhibiti wa kusini mwa nchi hiyo, eneo ambalo kwa muda mrefu limekuwa ngome ya Hezbollah.
Soma zaidi:
Ukraine yaonyesha kombora jipya linalodhaniwa kuwa la Neptune

Chanzo cha picha, KB Luch
Ukraine imeonyesha kwa mara ya kwanza kombora ambalo huenda ni la "masafa marefu" la Neptune.
Picha ya kombora hilo iko kwenye video iliyowekwa kwenye mtandao wa kijamii wa serikali wa Ukraine.
Video hiyo haijasema aina ya kombora lililoonyeshwa, lakini maoni kwenye tovuti za habari za Ukraine yanaonyesha kuwa ni la masafa marefu la Neptune.
Mamlaka ya Ukraine inadai kwamba ilikuwa ni kurushwa kwa makombora mawili ya Neptune mnamo Aprili 13, 2022, ambayo yaliharibu meli kuu katika Bahari Nyeusi ya Urusi, meli ya Moskva.
Onyesho la kombora hilo ilifanyika siku kadhaa baada ya Ukraine kuonyesha kombora jipya la anga, Flamingo, likiwa na uwezo wa kufika umbali wa kilomita elfu moja na uzito wa tani tatu.
Kipindi hiki, Rais wa Marekani Donald Trump, Ukraine na Urusi zimekuwa zikiendelea na majadiliano juu ya uwezekano wa kumaliza vita vya Urusi na Ukraine.
Pia unaweza kusoma:
Mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na nchi za Ulaya "kufanyika Geneva siku ya Jumanne"

Chanzo cha picha, Florian Gaertner/Photothek via Getty Images
Mazungumzo ya nyuklia na nchi tatu za Ulaya - Uingereza, Ufaransa na Ujerumani yanatarajiwa kufanyika Geneva kesho Jumanne, kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya Iran.
Maafisa wa Iran au Ulaya bado hawajathibitisha rasmi taarifa hii, lakini Shirika la Utangazaji la Iran (Sada-o-Sima) liliripoti "Siku ya Jumanne, kuwa Septemba 24, Iran na nchi tatu za Ulaya ambazo ni wanachama wa JCPOA, pamoja na Umoja wa Ulaya, zitafanya duru mpya ya mazungumzo katika ngazi ya manaibu mawaziri wa mambo ya nje huko Geneva".
Siku ya Ijumaa, Agosti 22, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Ufaransa na Ujerumani.
Taarifa hii ilisema imesalia chini ya wiki moja hadi tarehe ya mwisho ya nchi hizi tatu za Ulaya kufikia suluhisho la kidiplomasia kwa mpango wa nyuklia wa Iran.
Mawaziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Ufaransa na Ujerumani walimwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres takriban wiki mbili zilizopita: "Tumeweka wazi kwamba ikiwa Iran haiko tayari kufikia suluhu la kidiplomasia kabla ya mwisho wa Agosti 2025, au haitachukua fursa ya kuongeza muda wa mwisho, nchi hizo tatu za Ulaya ziko tayari kufufua taratibu za uchochezi."
Soma zaidi:
Saka kukosa mechi kwa wiki nne kwa jeraha

Chanzo cha picha, Getty Images
Bukayo Saka anatazamiwa kukosa mechi ya Arsenal dhidi ya Liverpool siku ya Jumapili pamoja na mechi za timu za England za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Andorra na Serbia mwezi ujao.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alitoka katikati ya mechi akiwa na jeraha la msuli wa paja katika ushindi wa nyumbani wa Jumamosi dhidi ya Leeds United na inakadiriwa kuwa mshambuliaji huyo hatakuwepo kwa kipindi cha hadi wiki nne.
Nahodha wa Arsenal Martin Odegaard ana mashaka na mechi itakayochezwa Anfield kutokana na jeraha la bega alilopata kwenye ushindi dhidi ya Leeds.
Odegaard alionekana kuwa na maumivu wakati nafasi yake ilipochukuliwa katika kipindi cha kwanza cha ushindi wa 5-0 na kiungo huyo wa zamani wa Real Madrid inasemekana aliondoka Emirates Stadium huku bega lake likiwa kwenye kombeo.
Mchezaji huyo wa Norway bado hajaondolewa kwenye mchezo dhidi ya mabingwa hao wa Ligi ya Primia na kuna matumaini kwa Arsenal kwamba si mchezaji huyo wa miaka 26 au Saka ambaye atakuwa majeruhi wa muda mrefu.
Kipindi hiki kuna afueni hasa kuhusu Saka, ambaye alikosa miezi mitatu ya msimu uliopita kutokana na jeraha la misuli ya paja.
Arsenal ina wingi wa vipaji vya washambuliaji msimu huu baada ya kuwasajili Viktor Gyokeres, Noni Madueke na Eberechi Eze msimu huu wa joto.
Kocha wa Gunners Mikel Arteta pia ana Gabriel Martinelli, Leandro Trossard, Ethan Nwaneri na Max Dowman kukabiliana na kukosekana kwa Saka na Odegaard.
Pia unaweza kusoma:
India itanunua mafuta itakapopata 'kwa bei nzuri', balozi wa nchi hiyo Urusi amesema

Chanzo cha picha, Getty Images
India itaendelea kununua mafuta pale itakapopata "kwa bei nzuri" ili kulinda maslahi ya watu wake bilioni 1.4, balozi wa nchi hiyo nchini Urusi amesema.
Kauli ya Vinay Kumar inakuja siku chache kabla ya ushuru wa 50% wa Rais wa Marekani Donald Trump kwa India, pamoja na ushuru mwingine wa 25% kama adhabu kwa ununuzi wa mafuta na silaha za Urusi, kuanza kutekelezwa.
Siku ya Jumapili, Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance alisema kwamba Trump alitangaza ushuru wa mwingine kwa India kwa "msimamo wake mkali wa kiuchumi" kwa Urusi na kuilazimisha kusitisha vita huko Ukraine.
India iliongeza uagizaji wa mafuta ghafi kutoka Urusi ambayo inapata kwa bei nafuu tangu vita vilipoanza na kufanya uhusiano wake na Marekani kuzorota na kuathiri mazungumzo ya makubaliano ya kibiashara.
Soma zaidi:
Mkuu wa jeshi wa Israel adaiwa kusema Israel lazima ikubali makubaliano ya mateka

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Eyal Zamir aliripotiwa kumtaka waziri mkuu wa Israel kukubali mpango huo mpya wa kuachiliwa huru mateka Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Israel (IDF), amesema kuwa kuna “mapatano mezani” kuhusu mateka waliobaki huko Gaza, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Israel.
Kulingana na taarifa ya Channel 13 News, Jenerali Luteni Eyal Zamir alieleza kuwa jeshi la Israel limeweka mazingira ya kufanikisha makubaliano hayo, na sasa suala hilo lipo “mikononi mwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.”
Jumanne hii, baraza la usalama la Israel linatarajiwa kujadili pendekezo jipya lililotolewa na wapatanishi wa kikanda, ambalo Hamas ililikubali wiki iliyopita.
Haya yanajiri baada ya maandamano makubwa mapema mwezi huu, ambapo mamia kwa maelfu ya watu walijitokeza mjini Tel Aviv, wakitaka kumalizwa kwa vita vya Gaza na kufikiwa kwa makubaliano ya kuwaachilia mateka walioko mikononi mwa Hamas.
Jukwaa la Mateka na Familia za waliopotea limesema kuwa Zamir ametamka kile “Waisraeli wengi wanachodai,” ikiwa ni pamoja na kufikiwa kwa makubaliano ya kuwarudisha nyumbani mateka wote 50 waliobaki, ambapo takriban 20 kati yao wanadhaniwa kuwa bado hai, pamoja na kumaliza vita hivyo.
Kundi hilo linapanga maandamano mengine makubwa siku ya Jumanne.
Pendekezo la hivi karibuni, linalotoka kwa wapatanishi wa Misri na Qatar, linadaiwa kuzingatia muundo uliowasilishwa na mjumbe wa Marekani, Steve Witkoff, mwezi Juni.
Kwa mujibu wa pendekezo hilo, Hamas ingewaachilia karibu nusu ya mateka hao kwa awamu mbili katika kipindi cha siku 60 za usitishaji mapigano.
Aidha, kungekuwa na mazungumzo ya kufikia makubaliano ya kudumu ya kusitisha mapigano.
Awali, ofisi ya Netanyahu ilieleza kuwa Israel itakubali tu makubaliano yatakayohakikisha “mateka wote wanaachiwa kwa pamoja, kwa wakati mmoja.”
Jumamosi iliyopita, ndege za kivita na vifaru vya Israel vilishambulia maeneo ya Jiji la Gaza, huku Israel ikiendeleza mpango wake wa kulitwaa eneo hilo kubwa zaidi la mijini katika Ukanda wa Gaza.
Benjamin Netanyahu ameapa kuishinda Hamas, na ameendelea kupuuzia ukosoaji wa ndani na wa kimataifa kuhusu mpango wake wa kupanua vita hivyo hata kutoka kwa Jenerali Zamir mwenyewe.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Israel, Zamir amekuwa akipinga uvamizi wa kijeshi wa kiwango kikubwa, akihofia kuhatarisha maisha ya mateka na kuingiza jeshi la Israel, ambalo tayari limechoka, katika mzozo wa muda mrefu ndani ya Gaza.
Mashambulizi hayo yamelenga kuwahamisha kwa nguvu zaidi ya watu milioni moja kutoka Jiji la Gaza hadi kwenye kambi za muda kusini, lakini Israel haijatoa ratiba maalum ya ni lini wanajeshi wake wataingia rasmi katika jiji hilo.
Inaripotiwa kuwa Netanyahu anatamani mji mzima uwe chini ya udhibiti wa Israel kuanzia tarehe 7 Oktoba.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa (UN), tayari takribani watu milioni 1.9 katika Gaza sawa na karibu asilimia 90 ya wakazi wamekwisha kulazimika kuhama makazi yao.
Soma pia:
Takriban watu wanane wauawa katika shambulizi la Israel kwenye hospitali ya Gaza, wizara ya afya yasema

Chanzo cha picha, Getty Images
Takriban watu wanane wameuawa katika shambulizi lililofanywa na Israel katika hospitali moja kusini mwa Ukanda wa Gaza, wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas imesema.
Wanahabari watatu ni miongoni mwa waliofariki, maafisa wa afya na shirika la habari la Reuters limesema.
Wanajumuisha mpiga picha wa Al-Jazeera na mkandarasi wa Reuters.
Shambulio hilo limefanyika katika Hospitali ya Nasser katikati ya asubuhi siku ya Jumatatu.
Jeshi la Israel na ofisi ya waziri mkuu walisema hawakuwa na maoni ya mara moja.
Soma pia:
M23 yaituhumu serikali kwa kutumia mamluki wa kigeni katika mashambulizi yanayoendelea

Chanzo cha picha, EPA
Wanamgambo wa M23 wameituhumu serikali ya DR Congo kwa kutumia “mamluki wa kigeni” katika mashambulizi ya Jumapili, ambayo wanadai yalilenga maeneo yanayokaliwa na jamii ya Kadasomwa pamoja na viunga vyake, katika eneo la Kalehe, mkoani Kivu Kusini.
Hata hivyo, jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) halijatoa tamko lolote kuhusu tuhuma hizo za M23.
Shirika la BBC liliwasiliana na msemaji wa jeshi kuhusiana na madai hayo ya matumizi ya mamluki, lakini bado hajatoa majibu.
Ripoti za mapigano kati ya pande hizo mbili ziliripotiwa siku ya Jumamosi na Jumapili katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kivu Kusini, ambapo mashuhuda mbalimbali wamedokeza kuwa mapigano hayo yamesababisha wakazi wengi kukimbia makazi yao.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, msemaji wa kundi la AFC/M23, Lawrence Kanyuka, alisema kuwa mashambulizi ya Jumapili huko Kadasomwa “yamesababisha vifo vya watu wengi” na “kuwaacha maelfu bila makazi” kutokana na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani.
Kanyuka aliongeza kuwa hapo awali, serikali iliwahi kutumia mamluki kutoka barani Ulaya, ambao waliruhusiwa kupitia Rwanda kurejea makwao baada ya M23 kuteka jiji la Goma.
Sasa, anadai kuwa mamluki waliotumika safari hii, ambao pia anawashutumu kwa kuhusika na mauaji, “hawatarudi kwa amani”.
Wakati huohuo, jeshi la Rwanda nalo linatuhumiwa kuisaidia M23, tuhuma ambazo serikali ya Rwanda imekanusha vikali.
Mapigano makali pia yalishuhudiwa siku ya Jumamosi katika eneo la Mwenga, mkoani Kivu Kusini, katika eneo la Efpo, na kusababisha watu wengi kukimbia makazi yao, kwa mujibu wa ripoti ya Radio RFI.
Inaripotiwa kuwa mapigano hayo pia yalipelekea kundi la M23 kuteka eneo la milimani la Lubumba, takriban kilomita 80 kutoka jiji la Uvira.
Pierre Mheshera, afisa wa serikali za mitaa katika jiji la Uvira, ameieleza BBC kuwa mapigano ya Jumamosi yamesababisha wakazi wengi “kuhama maeneo ya Lubumba na Kadjoka na kuelekea Uvira.”
Mheshera amethibitisha kuwa kwa mujibu wa taarifa walizonazo, M23 kwa sasa inalitawala eneo la Lubumba.
Taarifa hizi pia zimethibitishwa na baadhi ya vyombo vya habari vya ndani nchini DRC.
Hata hivyo, hadi sasa hakuna uthibitisho rasmi kutoka kwa serikali wala kwa kundi la M23 kuhusu madai hayo.
Mwezi uliopita, pande hizo mbili zilitia saini makubaliano ya kusitisha mapigano katika mazungumzo ya amani yaliyofanyika Doha, Qatar.
Mazungumzo hayo yalilenga kufikia mkataba wa amani ifikapo tarehe 18 mwezi huu, lakini malengo hayo hayakufikiwa.
Hata hivyo, pande zote mbili kwa sasa zimeendelea na mazungumzo mjini Doha.
Wakati mazungumzo yakiendelea, pande zote mbili zimeendelea kushutumiana kwa kuanzisha mashambulizi ya hapa na pale ambayo yameripotiwa katika mikoa ya Kivu Kusini na Kivu Kaskazini.
Soma pia:
Vikosi vya wanamgambo vya Sudan vyaongeza mashambulizi ili kudhibiti jiji la al-Fashir

Chanzo cha picha, Getty Images
Kikundi cha wanamgambo wa Sudan kinachojulikana kama Rapid Support Forces (RSF) kimeongeza mashambulizi yake dhidi ya jiji la magharibi linaloshikiliwa na jeshi, al-Fashir, na kudhibiti “maeneo kadhaa ya makazi,” kwa mujibu wa tovuti ya habari inayoendeshwa binafsi ya Darfur24 iliyotoa taarifa jana.
“Video zilizothibitishwa na Darfur24 zinaonesha wapiganaji wa RSF wakidai kudhibiti maeneo kadhaa na sehemu muhimu ndani ya jiji hilo,” tovuti hiyo ilisema.
Jeshi limekanusha madai ya kusonga mbele kwa kikundi hicho, likisema kuwa wanajeshi wake wamekabiliana na mashambulizi yote ya RSF dhidi ya jiji hilo na kwamba “matokeo ya mapigano ya hivi karibuni hayajabadilika.”
Al-Fashir, ambayo ni makao makuu ya jimbo la Darfur Kaskazini na kitovu muhimu cha misaada ya kibinadamu, ndilo jiji kubwa zaidi katika eneo hilo ambalo bado lipo chini ya udhibiti wa jeshi.
RSF wamekuwa wakilizingira jiji hilo kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Kikundi hicho kimeshtumiwa kwa kuua na kuwateka raia waliokuwa wakijaribu kukimbia jiji hilo pamoja na kushambulia kambi za wakimbizi wa ndani zilizoko karibu.
Wakati huohuo, makundi ya wanaharakati wa Sudan yanajiandaa kuzindua kampeni ya kutaka muda wa ujumbe wa uchunguzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu nchi hiyo yenye vita uongezwe kwa miaka miwili, kufuatia madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea na hali mbaya ya kibinadamu, kwa mujibu wa tovuti ya Sudan Tribune yenye makao yake Paris.
Umoja wa Mataifa uliunda ujumbe huo mwaka 2023 ili kuchunguza ukiukwaji wa haki unaofanywa na jeshi na RSF.
Ujumbe huo unatarajiwa kuwasilisha ripoti yake ya mwisho kwa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mwezi Septemba, wakati ambapo muda wake unatarajiwa kumalizika.
Isitoshe, Mtandao wa Madaktari wa Sudan unasema kuwa watu 46 wamefariki kutokana na utapiamlo katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, huku wanawake wanaonyonyesha wapatao 19,000 wakihitaji msaada wa dharura wa lishe katika jimbo la Sudan la Kordofan Kusini.
Vifo hivyo vilitokea kati ya mwezi Julai na Agosti na waathirika wengi ni wanawake na watoto.
Mgogoro wa chakula unaoendelea Kordofan Kusini umetokana na mvutano unaoongezeka kati ya Sudan People’s Liberation Movement – North (SPLM-N) inayoongozwa na Abdelaziz al-Hilu na vikosi vya wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) ambao wanapigania udhibiti wa eneo hilo lenye utajiri wa mafuta.
Mgogoro wa Sudan hadi sasa umesababisha vifo vya takriban watu 150,000 na kuwalazimu watu wengine milioni 12 kuyakimbia makazi yao.
Soma pia:
Warundi wajitokeza kwa wingi kuchagua viongozi wa vijiji na mitaa

Zaidi ya Warundi milioni sita wamejitokeza kwa wingi kushiriki duru ya mwisho ya uchaguzi wa viongozi wa taasisi mbalimbali za kitaifa, mchakato ulioanza mwezi Juni.
Jumatatu ya tarehe 25 Agosti, wananchi wanapiga kura kuwachagua viongozi 3,044 wa vijiji na mitaa kutoka maeneo yote ya nchi, ambao watatumikia kwa kipindi cha miaka mitano.
Awamu za awali za uchaguzi zilifanyika mwezi Juni kwa wabunge na madiwani, na Julai kwa wagombea wa vyama vya upinzani.
Katika chaguzi hizo, chama tawala cha CNDD-FDD, ambacho kimeiongoza Burundi kwa zaidi ya miaka 20, kilitangazwa mshindi kwa asilimia 100 ya kura katika nafasi nyingi isipokuwa kwenye nafasi za madiwani wa halmashauri, ambako kilikabiliwa na ushindani mkali na kupoteza kwa chini ya asilimia 2.
Hii ni mara ya kwanza kwa chama hicho kushinda kwa kiwango hicho kikubwa tangu kipate madaraka, licha ya ushindani kutoka kwa zaidi ya vyama 20 vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi.
Soma Pia:
Idadi ya vifo yaongezeka Sanaa baada ya mashambulizi ya anga ya Israel

Chanzo cha picha, Reuters
Televisheni ya Al Masirah yenye uhusiano na Houthi imeinukuu Wizara ya Afya ya Yemen ikisema kuwa, idadi ya waliofariki kutokana na mashambulizi ya anga ya Israel dhidi ya Sanaa imeongezeka na kufikia sita, huku wengine 86 wakijeruhiwa.
Wizara hiyo imesema, "Raia sita waliuawa na wengine 86 walijeruhiwa kutokana na hujuma ya Wazayuni kwenye kituo cha umeme cha Haziz na kampuni ya mafuta kwenye barabara ya 60." Idadi iliyotangazwa hapo awali ya vifo ilikuwa niwatu wanne waliokufa na majeruhi 67 .
Alisema kuwa "Vikundi vya Ulinzi wa Raia na uokoaji bado vinatafuta na kutambua watu waliopotea."
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema kuwa mashambulizi ya anga ya Israel dhidi ya Sanaa yaliharibu ikulu ya rais mjini Sanaa, pamoja na kituo cha umeme cha mji huo. Alisisitiza kuwa kundi linaloungwa mkono na Iran "linalipa gharama kubwa kwa mashambulizi yake dhidi ya Israel."
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema kuwa mashambulizi ya anga ya Israel dhidi ya Sanaa yaliharibu ikulu ya rais mjini Sanaa, pamoja na kituo cha umeme cha mji huo. Alisisitiza kuwa kundi linaloungwa mkono na Iran "linalipa gharama kubwa kwa mashambulizi yake dhidi ya Israel."
Wakati huo huo, kanali yenye uhusiano na Houthi ilitangaza kwamba mashambulizi ya anga ya Israel yalilenga mji mkuu wa Yemen, Sanaa, siku ya Jumapili. Imewanukuu wakazi wa mji mkuu huo wakisema kuwa mashambulizi hayo ya anga yalilenga maeneo karibu na kambi ya rais, vituo vya makombora, na vinu vya mafuta na nishati.
Unaweza pia kusoma:
Hamas yaishutumu srael kwa "kuchelewesha na kukwepa mambo ," huku idadi ya vifo karibu na vituo vya misaada ikizidi 2,000

Chanzo cha picha, Getty Images
Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas, Bassem Naim, ameishutumu serikali ya Israel kwa "kuahirisha na kukwepa hali kwa kuanzisha kwa mara nyingine tena vita kwenye Ukanda wa Gaza."
Naim alisema kupitia Telegram kwamba "vuguvugu limejifunza kuhusu uvujaji wa taarifa za vyombo vya habari unaoonyesha kwamba Israel inakataa makubaliano ya sehemu ambayo vuguvugu hilo lilikubali, na k inapendelea kuelekea kwenye makubaliano ya kina, kwa msaada wa utawala wa Marekani."
Naim alithibitisha kwamba vuguvugu hilo "bado halijapokea jibu rasmi kwa kuhusiana na mapendekezo ya hivi punde, wala halijawasilishwa na mapendekezo yoyote mapya ya kuhusu mpango wa kina."
Alidokeza kwamba "Israeli imeshindwa kufikia malengo yake yoyote aliyotangazwa, isipokuwa kutekeleza mauaji na uharibifu," kulingana naye.
Haya yanajiri wakati Waziri wa Ulinzi wa Israel Yisrael Katz akiwa tayari amekwishaapa kuuangamiza mji wa Gaza kama Hamas haitakubali kusitisha vita kulingana na masharti ya Israel na kuwaachilia mateka wote ambao bado inawashikilia.
Soma pia:
Wanajeshi wa kikosi cha taifa Marekani kubeba silaha Washington kuzuia uhalifu

Chanzo cha picha, AUL LOEB/AFP via Getty Images
Wanajeshi wa Kikosi cha Taifa cha Marekani (National Guard) walioko mitaani jijini Washington D.C., kama sehemu ya kampeni ya Rais Donald Trump ya kupambana na uhalifu, wataanza kubeba silaha kuanzia leo, kwa mujibu wa maafisa wawili.
Idadi kamili ya wanajeshi watakaobeba silaha bado haijathibitishwa, lakini maafisa hao walisema kuwa wanajeshi hao watabeba bastola aina ya M17 au bunduki aina ya M4.
Maafisa hao walizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina kwa kuwa hawakuruhusiwa kuzungumza rasmi kuhusu suala hilo, haya ni kwa mujibu wa shirika la Reuters.
Kwa wiki mbili zilizopita, mamia ya wanajeshi wa Kikosi cha Taifa waliokuwa hawana silaha wamekuwa wakilinda mitaa ya Washington, kufuatia tangazo la Trump la hali ya dharura ya kiuhalifu katika jiji hilo.
Wiki iliyopita, Waziri wa Ulinzi Pete Hegseth alitoa idhini kwa wanajeshi hao kubeba silaha.
Kwa upande wake, Kikosi Kazi cha Pamoja cha Kikosi cha Taifa–DC kilitoa taarifa siku ya Jumapili kikisema kuwa askari wake watatumia nguvu “ikiwa tu hakuna njia nyingine, na kwa kujibu tishio la haraka la kifo au madhara makubwa ya mwili.”
Wakati huo huo, Rais Trump, ambaye ni wa chama cha Republican, ametangaza kuwa ana mpango wa kupanua oparesheni yake ya kupambana na uhalifu hadi jiji la Chicago, ambalo linaongozwa na chama cha Democratic.
Aidha, siku ya Jumapili, alieleza kuwa anaweza kupeleka wanajeshi katika jiji la Baltimore, Maryland, linaloongozwa pia na chama cha Democratic.
Kiongozi wa wachache katika Baraza la Wawakilishi la Marekani, Hakeem Jeffries (Democrat), alisema Jumapili kuwa Rais Trump hana mamlaka ya kupeleka wanajeshi wa Kikosi cha Taifa huko Chicago, wakati Pentagon ikiendelea na mipango ya awali kuhusu uwezekano wa kupelekwa kwao.
Iwapo Trump atatumia kifungu cha sheria cha kipengee 12406 kupeleka wanajeshi wa Kikosi cha Taifa kutoka majimbo yanayoongozwa na Republican hadi maeneo yanayoongozwa na Democratic, kuna uwezekano mkubwa wa kukabiliwa na changamoto za kisheria.
Tangu Trump kuingia madarakani, wanajeshi wametumika huko Los Angeles kuzima maandamano ya kupinga maafisa wanaokamata wahamiaji.
Mara ya mwisho kwa wanajesh kutumwa Washington DC ni wakati wa uvamizi wa Januari 6, 2021, pale wafuasi wa Trump walipovamia majengo ya Bunge la Marekani.
Unaweza kusoma pia:
Kadi ya kumbukumbu ya Michael Jordan na Kobe Bryant yauzwa kwa rekodi ya dunia

Chanzo cha picha, Heritage Auctions/HA.com
Kadi ya kipekee ya mpira wa kikapu iliyosainiwa na magwiji wa NBA, Michael Jordan na Kobe Bryant, imeuzwa kwa dola milioni 12.9 (takriban shilingi bilioni 33) katika mnada, na kuwa kadi ya kumbukumbu ya michezo yenye thamani kubwa zaidi kuwahi kuuzwa katika historia.
Kadi hiyo, inayojulikana kama Upper Deck Exquisite Collection ya msimu wa 2007–08, ina nembo mbili tofauti za NBA na iliuzwa na kampuni ya mnada ya Heritage Auctions huko Marekani.
Kabla ya kuuzwa, kadi hiyo ilikuwa mikononi mwa mmiliki wake wa awali kwa zaidi ya miaka kumi.
Ilipowekwa mnadani, ilikadiriwa kuwa na thamani ya karibu dola milioni 6.
Hata hivyo, jumla ya zabuni 82 ziliwasilishwa, na bei ya mwisho ikazidi mara mbili ya makadirio hayo.
Uuzwaji huu umevunja rekodi iliyowekwa na kadi ya mwaka 1952 ya mchezaji wa baseball Mickey Mantle, ambayo iliuza kwa dola milioni 12.6 mnamo Agosti 2022.
Kwa sasa, kadi ya Jordan-Bryant inashika nafasi ya pili katika bidhaa za kumbukumbu za michezo zenye thamani kubwa zaidi duniani.
Nafasi ya kwanza inashikiliwa na jezi ya Babe Ruth aliyovaa wakati wa Fainali ya Dunia ya mwaka 1932, ambayo iliuza kwa takriban dola milioni 24 mnamo Agosti 2024.
Michael Jordan anachukuliwa kuwa mchezaji bora zaidi katika historia ya NBA, akiwa na mataji sita ya ubingwa aliyoyapata na timu ya Chicago Bulls kati ya mwaka 1991 na 1998.
Kobe Bryant, ambaye alifariki dunia katika ajali ya helikopta mwaka 2020, alikuwa miongoni mwa wachezaji walioheshimika zaidi katika mchezo wa vikapu wa NBA.
Alishinda mataji matano akiwa na Los Angeles Lakers kati ya mwaka 1996 hadi 2016.
Soma pia:
Kiongozi wa Korea Kaskazini asimamia jaribio jipya la kombora la ulinzi wa anga

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, amesimamia jaribio la makombora mawili mapya ya ulinzi wa anga, kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Korea Kaskazini (KCNA).
Taarifa hiyo ya serikali imesema kuwa silaha hizo zina “uwezo wa juu wa kivita” na zinatumia “teknolojia ya kipekee,” ingawa haikutoa maelezo ya kina kuhusu vipengele vya teknolojia hiyo.
Jaribio hilo lilitekelezwa Jumamosi na, kulingana na KCNA, “limethibitisha kuwa sifa za kiteknolojia za aina hizo mbili za makombora zinafaa sana kwa kuharibu malengo mbalimbali ya angani,” likiwemo mashambulizi kutoka kwa ndege zisizo na rubani (drones) na makombora ya mwelekeo wa chini (cruise missiles).
Hatua hiyo inajiri wakati mvutano unaongezeka katika Rasi ya Korea.
Siku chache kabla ya jaribio hilo, Korea Kusini ilifyatua risasi za onyo Jumanne dhidi ya wanajeshi wa Korea Kaskazini waliovuka kwa muda Mfereji wa Kutenganisha Kijeshi (DMZ) unaotenganisha nchi hizo mbili.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Yonhap, Kamandi ya Umoja wa Mataifa ilieleza kuwa karibu wanajeshi 30 wa Korea Kaskazini walivuka mpaka huo unaolindwa kwa ulinzi mkali kati ya pande hizo mbili.
Pyongyang ilijibu tukio hilo kwa kuishutumu Seoul kwa kile ilichokiita “uchokozi wa makusudi,” ikiongeza ukakasi katika uhusiano wa muda mrefu uliojaa misuguano.
Wakati huo huo, Korea Kusini na Marekani zimeendelea na mazoezi makubwa ya kijeshi ya pamoja katika eneo hilo tangu Jumatatu. Mazoezi hayo yanafanyika katika kipindi ambacho diplomasia kati ya Korea Kaskazini na Kusini inadorora, licha ya ahadi za kisiasa zilizotolewa wakati wa kampeni na Rais mpya wa Korea Kusini, Lee Jae Myung, ambaye aliahidi “kuboresha uhusiano wa pande mbili.”
Licha ya juhudi hizo, dada wa Kim Jong Un amezipinga vikali, akizitaja kuwa ni za hila na zisizo na dhati.
Hili limeifanya hali ya kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili kuwa tete zaidi.
Korea Kaskazini na Korea Kusini zimegawanyika tangu kumalizika kwa Vita vya Korea mwaka 1953.
Ingawa vita hivyo vilikoma kwa kusainiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano, hakuna mkataba rasmi wa amani uliowahi kutiwa saini, jambo ambalo limeacha nchi hizo mbili zikiwa bado “kihalali katika hali ya vita,” licha ya kwamba hakuna mashambulizi ya moja kwa moja yaliyotokea kwa miaka mingi.
Pia unaweza kusoma:
Mashambulizi ya Ukraine huko Urusi yapandisha bei ya mafuta duniani.

Chanzo cha picha, Getty Images
Bei ya mafuta imepanda kwa kushtua siku ya Jumatatu baada ya Ukraine kuongeza mashambulizi yake dhidi ya Urusi, na kuongeza wasiwasi kuwa usambazaji wa mafuta ya Urusi dunaini unaweza kukatizwa.
Wakati huo huo, matarajio ya Marekani kupunguza viwango vya riba yalikuza mtazamo chanya kwa uchumi wa dunia na ongezeko la mahitaji ya nishati.
Bei ya mafuta ghafi aina ya Brent ilipanda kwa senti 6, au 0.09%, kufikia dola $67.79 kwa pipa, huku mafuta ghafi ya West Texas Intermediate (WTI) yakiongezeka kwa senti 9, au 0.14%, hadi kufikia dola $63.75 kwa pipa.
Ukraine ilizindua shambulio la ndege isiyo na rubani dhidi ya Urusi siku ya Jumapili, ambalo lilisababisha kupungua kwa uwezo wa moja ya mitambo mikubwa ya nyuklia ya Urusi na kuchochea moto mkubwa katika kituo cha kusafirisha mafuta cha Ust-Luga, maafisa wa Urusi walisema.
Zaidi ya hapo, moto katika kiwanda cha kusafisha mafuta cha Novoshakhtinsk nchini Urusi, uliosababishwa na shambulio la ndege isiyo na rubani kutoka Ukraine, ulikuwa ukiwaka kwa siku ya nne mfululizo Jumapili, kwa mujibu wa kaimu gavana wa eneo hilo.
Kiwanda hicho kinauza mafuta hasa kwa ajili ya kuuza nje na kina uwezo wa kusafisha jumla ya tani milioni 5 za mafuta kwa mwaka, sawa na takribani mapipa 100,000 kwa siku.
“Mashambulizi ya Ukraine yanapofanikiwa kulenga miundombinu ya mafuta ya Urusi... hatari kwa bei ya mafuta ghafi sasa zinapanda,” alisema mchambuzi wa soko la IG, Tony Sycamore.
Wakati huohuo, Makamu wa Rais wa Marekani, JD Vance, alisema Jumapili kuwa Urusi imepiga hatua kwenye "makubaliano makubwa" kuelekea kufikiwa kwa suluhu ya mazungumzo katika vita vyake na Ukraine.
Pia unaweza kusoma:
