Neptune: Ni nini kinachojulikana kuhusu silaha hii ya Ukraine na je ni tishio kwa Moscow?

Chanzo cha picha, KB Luch
Ukraine inaweza kuwa imetengeneza kombora lake la masafa marefu ambalo kinadharia linaweza kufikia miji ya Urusi kama vile Ryazan, Kursk na hata Moscow. Idhaa ya BBC ya Ukraine ilizungumza na vyanzo vyake ili kutazama iwapo kweli ndivyo hali ilivyo.
"Mafanikio ya silaha zetu za masafa marefu: lengo lilikuwa umbali wa kilomita 700," Volodymyr Zelenskyy alisema mnamo Agosti 31. Hata hivyo, ni nini hasa rais wa Ukraine alikuwa akizungumzia bado hakijajulikana. Kuna mawazo tu kuhusu kombora jipya la Ukraine
Siku hiyo hiyo, Alexei Danilov, Katibu wa Baraza la Usalama la Kitaifa na Ulinzi, alichapisha video ya urushaji wa roketi kwenye mitandao yake ya kijamii. Video hiyo hiyo ilichapishwa na msanidi mkuu wa vifaa vya roketi nchini Ukraine, ofisi ya muundo ya Luch.
"Mpango wa makombora wa Rais wa Ukraine. Majaribio yamefaulu, maombi yanafaa,” aliandika Katibu wa Baraza la Usalama na Ulinzi wa Kitaifa.
Mjumbe wa idhaa ya BBC nchini Ukraine katika usimamizi wa kampuni ya Ukroboronprom alisema kuwa video ya Danilov inaonyesha "silaha ya masafa marefu ya kilomita 700" ambayo Zelensky anazungumzia.
Hili ni kombora la Ukraine ambalo tayari limetumika katika hali ya vita, chanzo kilisema, lakini alikataa kuzungumza juu yake kwa undani zaidi - na hakuweza hata kutaja jina lake. Mzungumzaji hakukana wala kuthibitisha kwamba inaweza kuwa toleo la kisasa la roketi ya Neptune.
Kurudi kwa kombora la Neptune?

Mfumo huu wa kombora, uliotengenezwa katika ofisi ya muundo wa Luch na kuwekwa katika huduma miaka mitatu tu iliyopita, umeundwa kuharibu meli za adui kwenye bahari kuu.
Ilikuwa ni moja ya maendeleo muhimu zaidi ya tasnia ya ulinzi ya Ukraine katika miaka ya hivi karibuni, lakini wakati wa kuzuka kwa vita kamili, ni nakala chache tu za kombora kama hilo zilitengenezwa.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mamlaka ya Ukraine inadai kuwa makombora mawili ya Neptune mnamo Aprili 13, 2022 yaliharibu meli kuu ya Meli zilizokuwa katika Bahari Nyeusi zinazomilikiwa na Urusi, cruiser Moskva.
"Kombora lililotengenezwa na Ukraine lilisaidia kurejesha utulivu katika maji ya Ukraine katika eneo la Bahari Nyeusi. Haya yalikuwa matumizi ya kwanza ya Neptune katika hali ya vita, na ikawa ya kihistoria," Zelensky aliandika juu ya tukio hili.
Baada ya shambulio hilo, Kyiv ilipokea rasmi makombora yenye nguvu zaidi ya Harpoon kutoka kwa washirika wa Magharibi na makombora ya Neptune yakawacha kutumika.
Butusov na vyanzo vya uchapishaji maalumu wa Marekani The War Zone vinadai kwamba katika mwaka uliopita sekta ya ulinzi ya Ukraine imekuwa ikifanya kazi ya kurekebisha makombora ya R-360 ya Neptune kwa matumizi sio tu dhidi ya meli baharini, lakini pia dhidi ya malengo ya ardhini.
Kulingana na data hizi, mnamo Agosti 23, mfumo mpya wa kombora wa kupambana na ndege wa Urusi S-400, ulioko eneo la magharibi mwa Crimea - Cape Tarkhankut, ulipigwa kwa mafanikio na kombora linalodaiwa kuimarishwa la R-360.
Lengo lilikuwa katika umbali wa takriban kilomita kati ya 150-18 kutoka pwani ya Ukraine.

Chanzo cha picha, Gur NOU
Baadaye, Katibu wa NSDC Danilov alithibitisha kwamba SAM ya Urusi ilishambuliwa na kombora la Ukraine, lakini alikataa kusema ni lipi.
"Hii ni bidhaa yetu mpya, ambayo imeonekana kutokuwa na dosari kabisa," alisema, na kuongeza kuwa maendeleo haya ya tasnia ya ulinzi ya Ukraine yalifanywa kama sehemu ya programu ya kombora iliyoidhinishwa mnamo 2020.
Matumizi ya makombora ya kuzuia meli kushambulia maeneo ya ardhini sio ujuzi wa Ukraine. Wiki za kwanza za vita, Jeshi la Urusi limekuwa likitumia makombora ya kupambana na meli ya juu X-22 na Onyx kwa njia hii.
Mnamo Januari 14 mwaka huu, kombora la X-22 liliharibu jengo la makazi la ghorofa nyingi huko Dnieper, na kuua watu 46.
Kuhusu Neptune, haikujulikana hapo awali kuhusu matumizi yake dhidi ya malengo ya ardhini.
Zaidi ya hayo, uimarishaji kama huo utahitaji muundo mpya wa mfumo wa mwelekeo wa kombora.
Ikiwa umbali wakwe unalingana na kilomita 700 iliyotangazwa, basi hii pia inaonyesha marekebisho makubwa ya injini. Neptune ya kupambana na meli ilikuwa na uwezo wa kuruka umbali wa hadi kilomita 300.
Juu ya bahari au juu ya nchi?
Akichambua video fupi ya sekunde 20 iliyotolewa na Danilov, mhariri mkuu wa Defense Express Oleg Katkov anasema kuwa hakuna kitu kinachoonekana ndani yake, isipokuwa wakati kiongeza kasi cha roketi kinatengana.
Neptune ya R-360 iliruka kwa njia kama hiyo.
"Maelezo ya kisayansi zaidi ni kwamba kwa hakika ni kombora la Neptune lililoundwa upya, kwa sababu suala la kurekebisha kombora hili kwa mashambulizi ya maeneo ya pwani lilitolewa tangu mwanzo wa maendeleo yake," mtaalam huyo alielezea Idhaa ya BBC ya Ukraine.
Kwa mfano, mtaalam huyo anasema, kombora la kuzuia meli la Harpoon (toleo la Harpoon Block 2) linafanya kazi sawa. Hatahivyo lina kichwa kinachofanya kazi cha rada (GOS).
Hii inamaanisha kuwa kombora kama hilo linaweza kupata, kuchanganua na kuliandama kombora kwa kujitegemea kulingana na data iliyopakiwa mapema.
Lakini wakati wa kutumia makombora ya kupambana na meli dhidi ya malengo ya ardhi, kuna tatizo muhimu. Linaweza tu kushambulia shabaha karibu na ukanda wa pwani, kwani huruka juu ya uso wa bahari kwa sehemu kubwa ya safari yake.
Hali hii inaonyesha kuwa "silaha mpya ya Ukraine ya kilomita 700" inaweza kutumika tu katika vituo vilivyoko kwenye pwani ya Bahari Nyeusi na haitoi tishio kwa Urusi (kwasababu kutoka mpaka waUkraine hadi mji mkuu wa Urusi ni takriban km 420) .
Ili kombora kuruka juu ya ardhi, lazima liwe na mfumo wa kufuata ardhi na kukabili upinzani dhidi ya silaha za kielektroniki (vita vya elektroniki).
Kwa mfano, mfumo wa DSMAC (Digital Scene Matching Area Correlator) uliosakinishwa kwenye makombora ya kisasa ya safari ya baharini huchanganua uso wa chini wakati wa kukimbia na kuulinganisha na picha ya marejeleo iliyofungwa kwa viwianishi mahususi.












