Kobe Bryant aingia kwenye orodha ya nyota waliokufa wanaopata mapato makubwa zaidi

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Ni miezi tisa sasa tangu aliyekuwa nguli wa mchezo wa mpira wa kikapu, Kobe Bryant kufariki akiwa na miaka 41.

Koble alifariki kwenye ajali ya helkopta akiwa na binti yake mweye umri wa miaka 13-Gianna 'Gigi' na watu wengine saba .

Kwa mujibu wa mtandao wa Forbes , hayati Kobe Bryant ameingia katika orodha ya nyota waliokufa wanaolipwa fedha nyingi sana kwa mwaka 2020.

Koble amechukua nafasi ya sita.

Baada ya kifo chake anapata mapato ya dola milioni 20 kutokana na bidha zake za mavazi na viatu huku Nike ikiripoti kuwa inapata mamilioni ya fedha kutokana na kuuza bidhaa zake za Mamba.

Pamoja na laba ,video fupi ya Kobe ya mwaka 2018 akieleza jinsi anavyocheza, imeweza kuuzwa zaidi ya nakala 300,000 kwa mwaka 2020, mara kumi zaidi ya jinsi ilivyouzika mwaka 2019.

f

Chanzo cha picha, Reuters

Lakini pia baada ya Lakers kushinda ubingwa wa NBA mnamo Oktoba, jezi ya Kobe zilikuwa za pili kwa kuuzwa sana na shirika la Lakers.

Bryant aliripotiwa kuwa na utajiri wa thamani ya $600 wakati alipofariki.

Michael Jackson bado anaongoza katika marehemu nyota wanaopata mapato makubwa zaidi.

Michael Jackson

Forbes imaeinisha orodha ya nyota waliofariki 13 wanaolipwa kiasi kikubwa cha fedha kwa mwaka 2020

1. Michael Jackson - Mwanamziki aliyefariki kwa kuzidisha kiwango cha dawa: Mwaka huu amepata mapato ya dola milioni 48

2. Dkt. Seuss / Theodor Seuss "Ted" Geisel - Muigizaji wa Marekani (alifariki kutokana na saratani): amepokea dola 33

3. Charles Schulz - mtaalamu wa katuni (alifariki kutokana na kansa): dola milioni $32.5

4. Arnold Palmer - anapata dola milioni $25

5. Elvis Presley - Mchekeshaji dola milioni 23

6 Kobe Bryant - Mchezaji mpira wa kikapu , anapata dola milioni 20

7. Juice WRLD - Mwanamuziki dola milioni 15

8. Bob Marley - Mwanamuziki (saratani) dola milioni 14

9. John Lennon - Mwanamuziki dola milioni $13

10. Prince - Mwanamuziki dola milioni 10

11. Freddie Mercury - Mwanamuziki , milioni $9

12. George Harrison - Mwanamuziki dola milioni $8.5

13. Marilyn Monroe - Nyota wa filamu, dola milioni 8