Jinsi Trump anavyotumia 'Nadharia ya Mwendawazimu' kujaribu kubadilisha ulimwengu

- Author, Allan Little
- Nafasi, Mwandishi mwandamizi
- Muda wa kusoma: Dakika 5
Mwezi uliyopita alipoulizwa ikiwa ana mpango wa kuungana na Israel kuishambulia Iran, Raia wa Marekani Donald Trump alijibu "Huenda nikafanya hivyo. Huenda nisifanye hivyo. Hakuna mtu anayejua nitakachokifanya".
Aliufanya ulimwengu kuamini kwamba atafanya uamuzi juu ya suala hilo ndani ya wiki mbili ili kutoa nafasi kwa Iran kurejea kwenye meza ya mazungumzo. Lakini baadaye akawashambulia.
Kuna kitu kinaibuka hapa: Kitu kinachotabirika zaidi kumhusu Trump ni hulka yake ya kitotabirika. Anabadili msimamo. Anajikanganya mwenyewe. Haeleweke.
"[Trump] amebuni sera thabiti ambayo inasemekana kuwa ya msingi imara zaidi, hasa katika masuala ya kigeni, tangu zama za Richard Nixon," anasema Peter Trubowitz, profesa wa uhusiano wa kimataifa katika Chuo cha Uchumi cha London.
"Na hii inafanya maamuzi ya sera kutegemea zaidi mwenendo wa Trump, sifa yake, tabia yake."

Chanzo cha picha, Getty Images
Trump ameamua kutumia mbinu hii kisiasa; ameguaza hali ya kutotabirika kwake kuwa kiungo muhimu cha kimkakati na mali ya kisiasa. Amepandisha daraja hali ya kutotabirika. Sasa sifa hii ilikuja nayo Ikulu inaendesha sera za kigeni na usalama.
Inabadilisha sura ya ulimwengu.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaita hali hii Nadharia ya Mwendawazimu, sifa ambayo kiongozi hutumia kumshawishi adui yake kwamba ana uwezo wa kitu chochote, kufikia makubaliano. Ikitumiwa kwa mafanikio inaweza kuwa aina ya shinikizo na Trump anaamini inamsaidia, kuwaelekeza washirika wa Marekani anakotaka.
Lakini je, mbinu hii inaweza kutumiwa dhidi ya maadui? Na je, nini kitatokea hila hii iliyokusudiwa kuwapumbaza wapinzani isipofanya kazi? BBC inatathmini faida na athari za mbinu ya kutotabirika kisiasa.
Kushambulia, kutusi, na kukumbatia
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Trump alianza muhula wake wa pili madarakani kwa kumkumbatia Rais wa Urusi Vladimir Putin na kuwashambulia washirika wa Marekani. Aliikashifu Canada kwa kusema inapaswa kuwa jimbo la 51 la Marekani.
Alisema yuko tayari kutumia nguvu za kijeshi kuiteka Greenland, eneo linalojitawala la mshirika wa Marekani Denmark. Na kuongeza kuwa Marekani inapaswa kuchukua tena umiliki na udhibiti wa Mfereji wa Panama.
Kifungu cha 5 cha mkataba wa Nato kinamshurutisha kila mwanachama kuwatetea wenzake. Trump alitia mashakani dhamira Marekani kuhusiana na suala hilo. "Nadhani Kifungu cha 5 kinahusu msaada wa maisha" alitangaza Ben Wallace, waziri wa zamani wa ulinzi wa Uingereza.
Mwanasheria Mkuu wa Conservative Dominic Grieve alisema: "Kwa sasa muungano wa kuvuka Atlantiki umekwisha."
Msururu wa umbe wa maandishi uliovujishwa ulifichua mienendo ya dharau zinazofanywa na Ikulu ya Trump dhdi ya washirika wa Ulaya. "Nakubaliana nawe kuhusu msimamo wako dhidi ya viongozi wa Uropa wanaotaka vitu vya bure," Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth aliwaambia wenzake, akitumia neno "PATHETIC" kuashiria jinsi alivyochukizwa.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Mapema mwaka huu mjini Munich, Makamu wa rais wa Marekani JD Vance alisema kuwa Marekani haitaendelea tena kuwa mdhamini wa usalama wa Ulaya
Kauli hiyo ilionekana kugeuza ukurasa wa mshikamano wa miaka 80 ya trans-Atlantic. "Alichofanya Trump ni kuibua mashaka makubwa na maswali kuhusu uaminifu wa ahadi za kimataifa za Marekani," anasema Prof Trubowitz.
"Makubaliano yoyote yaliyofikiwa kati ya nchi hizo [barani Ulaya] na Marekani, kkuhusu y masuala ya kiusalama, kiuchumi au mengine, sasa yanategemea notisi ya muda mfupi iliyotolewa na nchi hiyo yenye uwezo mkubwa duniani.
"Nahisi baadhi ya watu wanaomzunguka Trump wanafikiri kuwa kutotabirika ni jambo zuri, kwa sababu inampa Donald Trump nafasi ya kuimarisha uwezo wa taifa hilo kwa maslahi yake...
Kutabirika kusikoeleweka
Trump sio rais wa kwanza wa Marekani kutumia mbinu ya kutotabirika. Mnamo mwaka wa 1968, wakati Rais wa Marekani Richard Nixon alipokuwa akijaribu kumaliza vita huko Vietnam, alikuta adui wa Vietnam Kaskazini hawezi kushindwa.
"Wakati mmoja Nixon alimwambia Mshauri wake wa Usalama wa Kitaifa Henry Kissinger, 'unapaswa kuwaambia wajumbe wa Kivietinamu Kaskazini kwamba Nixon ana kichaa na hujui atafanya nini, kwa hivyo ni bora kufikia makubaliano kabla mambo hayajabadilika'," anasema Michael Desch, profesa wa uhusiano wa kimataifa katika Chuo Kikuu cha Notre Dame. "Hiyo ndio nadharia ya mwendawazimu."

Chanzo cha picha, Getty Images
Julie Norman, profesa wa siasa katika Chuo Kikuu cha London, anaafiki kwamba sasa kuna nadharia kutotabirika.
"Ni vigumu sana kutabiri kitakachotokea siku moja hadi nyingine," anasema. "Na huo umekuwa mwenendo wa Trump kila wakati."
Trump alifanikiwa kutumia sifa yake ya kutotabirika kubadilisha uhusiano wa ulinzi wa Atlantiki. Na inavyoonekana ili kumweka Trump karibu, baadhi ya viongozi wa Ulaya wamebembeleza na kujipendekeza.
Mkutano wa kilele wa Nato wa mwezi uliopita mjini The Hague ulikuwa ni zoezi la uchumba usio wa kawaida. Katibu Mkuu wa Nato Mark Rutte hapo awali alimtumia Rais Trump (au "Dear Donald") ujumbe mfupi wa simu, ambao Trump aliuvujisha.
"Hongera na asante kwa hatua yako madhubuti nchini Iran, ilikuwa ya kushangaza kweli," aliandika.
Katika tangazo lijalo kwamba wanachama wote wa Nato wamekubali kuongeza matumizi ya ulinzi hadi 5% ya Pato la Taifa, aliendelea: "Utafanikisha kitu ambacho HAKUNA rais katika miongo kadhaa anaweza kutekelezwa."

Chanzo cha picha, Getty Images
Anthony Scaramucci, ambaye aliwahi kuwa mkurugenzi wa mawasiliano wa Trump katika muhula wake wa kwanza, alisema: "Bwana Rutte, anajaribu kukuaibisha bwana. Ameketi kwenye Air Force One akikucheka."
Na hii inaweza kuwa udhaifu waTrump: vitendo vyao vinaweza kuwa msingi wa wazo kwamba Trump anatamani kusifiwa. Au kwamba anatafuta mafanikio ya muda mfupi, akiwapendelea juu ya michakato mirefu na ngumu.
Ikiwa hivyo basi dhana yao ni sahihi, na inaweka mipaka uwezo wa Trump wa kuwafanya wapinzani kuwa wapumbavu - badala yake, amethibitisha vyema na kubaini jinsi wanavyodhibiti mienendo yao.
Wapinzani hawawezi kustahimili haiba na vitisho
Swali linaloibika katika mbinu hii ya kutotabirika au Nadharia ya Mwendawazimu inaweza kufanya kazi dhidi ya wapinzani.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, mshirika ambaye alikemewa na Trump na Vance katika Ofisi ya Oval, baadaye alikubali kutoa fursa kwa Marekani za kunyonya rasilimali za madini za Ukraine.
Vladimir Putin, kwa upande mwingine, bado hajakubali vitisho vya Trump vile. Siku ya Alhamisi, kufuatia simu, Trump alisema "amesikitishwa" kwamba Putin hayuko tayari kumaliza vita dhidi ya Ukraine.

Chanzo cha picha, Reuters
















