Vita vya Ukraine: Warusi waliokaidi wakizungumzia vita

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa Waukraine ilikuwa wazi tangu mwanzo wa uvamizi wa Urusi kwamba hii 'operesheni maalum' dhidi ya Ukraine ili kuikomboa nchi hiyo yenye kujitenga na eneo la Donbas, kama Vladimir Putin alivyotangaza. Bali ilikuwa vita.
Lakini nchini Urusi ni hatia kuiita hivyo.
Nchini Urusi, watu kadhaa tayari wameshtakiwa chini ya sheria inayojulikana kama sheria ya "habari potofu".
Wanakabiliwa na hadi miaka 15 gerezani kwa kusema chochote kinachokwenda na kinyume cha uvamizi wa Urusi huko Ukraine au kukosoa jeshi.
Sheria hiyo, ya hivi karibuni katika mfululizo wa hatua zilizochukuliwa na Vladimir Putin tangu alipoingia madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 1999 kuwatisha wapinzani wake, kuzuia uhuru wa kujieleza na kunyamazisha vyombo huru vya habari, pia imesababisha kuongezeka kwa kasi kwa udukuzi wa Urusi.
Ni ongezeko kubwa la udhibiti nchini Urusi, ambapo Vladimir Putin ametumia miongo miwili madarakani akiwaondoa wapinzani, kukandamiza uhuru wa kujieleza na kunyamazisha vyombo huru vya habari: kuvunjwa kwa demokrasia ambayo ina madhara makubwa hapa Ukraine.
Mpinzani wa Urusi Vladimir Kara-Murza alijaribu kuonya juu ya hatari hiyo.
Katika hotuba aliotoa mnamo mwezi Machi, mwanaharakati wa upinzani nchini urusi akiwa nchini Marekani, Kara-Murza aliwatuhumu viongozi wa nchi za Magharibi kwa kujaribu mara kwa mara kusafisha uhusiano na Putin, kuruhusu nchi zao kuwa kama kimbilio la pesa zilizochafuliwa na kuangalia upande mwingine hata kama uhuru nchini Urusi uliendelea kupungua.
"Dunia nzima sasa inaona kile ambacho utawala wa Putin unafanya kwa Ukraine. Bw Kara-Murza aliambia Baraza la Wawakilishi la Arizona, majuma mawili ya vita. Kulipuliwa kwa wodi za wazazi na hospitali na shule. Huu ni uhalifu wa kivita", alisema.
Hata hivyo, ni kosa kubwa la uhalifu kutoa maoni hayo nchini Urusi.
Mwezi mmoja baadaye, Kara-Murza alichukuliwa na polisi na kuwekwa kizuizini mjini Moscow na kushitakiwa kwa kusambaza taarifa za uongo kuhusu jeshi la Urusi.
Bado yuko kizuizini.
Sheria anayotuhumiwa kuivunja ilipitishwa mwezi Machi mara baada ya uvamizi huo.
Kwa ujumla, ofisi ya waendesha mashtaka nchini Ukraine imesajili kesi 11,000 za uhalifu wa kivita.
Mwanajeshi wa Urusi, kwa mfano, alikiri kosa la kumpiga risasi raia asiyekuwa na hatia.
BBC pia imekusanya ushahidi, ikiwa ni pamoja na video ya CCTV ikionesha jinsi raia wawili walivyopigwa risasi na wanajeshi ya Urusi.
Wale kurudi kuharibiwa Andriivka kukusanya vitu vyao wanasema ushahidi mkubwa zaidi.
Wale wanaorejea kuokoa kile wanachoweza kutokana na mabaki huko Andriivka wana shuhuda zenye uzito zaidi.
Wakati Urusi ilipoivamia Ukraine, familia nyingi zilikimbia mji mkuu, Kiev, na kutafuta hifadhi katika vijiji kama hivyo, zikitumaini kuwa vitakuwa salama.
Kinyume chake, walilazimishwa kuishi kwenye makazi baridi kwa majuma kadhaa wakati wanajeshi walioteka maeneo hayo wakiwa wanaendesha vifaru katika mashamba yao huku wakichimba mahandaki katika bustani zao.
Baada ya wanajeshi wa Urusi kuondoka kijijini mwezi Aprili, wakuu wa vijiji walisema walikuta miili ya watu 13 katika makazi hayo.
"Mikono yao ilikuwa imefungwa kwa nyuma na wakapigwa risasi kichwani", anasema Anatoliy Kibukevych. Kisha akaanza kutaja majina ya kila muhanga.
Barabara kuu, ambayo ilikuwa imeshikwa na vifaru vya Urusi waliagiza idhibitiwe ili kuteka mji wa Kiev na imejaa vifusi, matofali yaliyoteketezwa kwa moto, vitanda vya chuma, masufuria na mabakuli na kila aina ya vyombo.
Pia kuna maombi yalioandikwa kwa rangi yanayosomeka ''Watoto''!, ''Watu!'' katika malango ya bustani wamedungwa na vipande vya makombora.

''Ukweli ni kwamba, ni adui mkuu wa serikali,'' anasema Evgenia Kara-Murza, mke wa Vladimir, kutoka Washington DC, ambako anaishi kwa sababu za usalama.
"Ndio maana nadhani utawala huu unajaribu kukandamiza upinzani wote nchini Urusi kwa sheria hii na kuwanyamazisha watu kwa kuwatisha", Kara-Murza aliiambia BBC.
Kara-Murza alisema mke wake mwanaharakati alikuwa ametiliwa sumu mara mbili katika siku za nyuma na kidogo apoteze maisha lakini hakukata tamaa.
"Nina hakika Vladimir alikuwa anajua hatari zilizopo kwa kiwango cha juu. Walikuwa wamenyamaza," anasema, Lakini anaamini sasa ni wakati ambapo watu hawaogopi tena na wanapaswa kuwaambia watu wengine wasiogope", akikumbuka fika kuwa mumewe mwanaharakani alivyotiliwa simu.

Siwezi kuficha ukweli, lakini, nitafungwa jela kwa hilo?
Wakati vita nchini Ukraine vilipoanza, mwandishi wa habari Lilia Yapparova anasema alijisikia kushurutishwa kwenda shambani na kuripoti kilichotokea.
"Sikuweza kulala kwa sababu watu walikuwa wanakufa na ilibidi niwepo".
Yapparova ni mwandishi pekee wa Kirusi aliyeweza kuripoti kutoka maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa Ukraine kwa muda mrefu.
Leo, tayari kuna waandishi watatu tu wanawake, wote wakifanya kazi katika vyombo huru vya habari.
Bi Yapparova anasema alitaka angalau kuondoa hiyo propaganda.
Siwezi kuficha ukweli, lakini, nitafungwa jela kwa hilo?
''Jambo pekee ambalo ni muhimu kwangu hivi sasa ni vita kukoma na watu kutoka Urusi waone kile kinachoendelea,'' anasema.
Lakini hiyo ni vita ya peke yake, juu ya hatari ya kufanya kazi vitani nchini Ukraine.
Meduza, tovuti ya habari anayoandikia Bi Yapparova, imepigwa marufuku nchini Urusi, kama ilivyo kwa karibu vyombo vyote huru.
Waandishi wa habari na vyombo vya habari vimetambulishwa kama ''mawakala wa kigeni'' huku Facebook na mitandao mingine ya kijamii pia ikifungwa kabisa.
Wakati huo huo, vituo rasmi vya TV vya serikali vimeripoti 'operesheni maalum' iliyofanywa na Urusi.
"Tumepoteza vita vya propaganda kwa wakati huu", Bi. Yapparova alisema, akiongeza kuwa hata wale anaowajua wanaamini katika maneno matamu rasmi ya Kirusi.
Anatambua kwamba kila neno analoliandika kutoka Ukraine - simulizi za kweli kuhusu mauaji ya raia, kupatikana kwa makaburi ya halaiki au uharibifu wa kutisha utamweka katika hatari ya kushtakiwa chini ya sheria ya 'habari potofu':
"Ninafahamu hatari zilizopo mbele. Niko tayari kwa ajili yake. Mimi sitafumbia jicho suala hili. Najua sheria hii inamaanisha nini. Mwanahabari huyo alisema. ''Lakini sikuweza kujizuia kutokana na kile kinacoendelea huko.''
"Ni kweli, mara kwa mara nina wasiwasi. Wakati mwingine kuandika habari ni chungu sana kwa sababu siwezi kuficha ukweli.? Na chochote kinaweza kutokea wakati wowote".

Je ni operesheni maalum au vita?
Kwa Michael Nacke tayari hatari inamkodolea macho.
Mwandishi huyo kijana aliondoka nchini Urusi kabla ya vita kuanza akikwepa mazingira ambayo tayari yalikuwa yameendelea kufanya kazi yake kuwa ngumu.
Na sasa, ni mtu anayetafutwa kwa kusema ukweli.
"Nilitumia neno 'vita' badala ya 'operesheni maalum'", anasema juu ya ''uhalifu'' wake kama ilivyowekwa na wachunguzi wa Urusi katika taarifa ya kurasa 91. ''Haijalishi ni sheria gani wanatumia dhidi yako, ni kukufanya unyamaze. "Haijalishi sheria gani wanaitumia dhidi yako. Wanataka kukunyamazisha tu."
Upande wa mashtaka ulichukua hatua hiyo baada ya Nacke kuweka kwenye chaneli yake ya YouTube jinsi vifaru vya Urusi yalivyofyatua risasi kwenye mtambo wa nyuklia huko Zaporizhzhia.
Tukio hilo lililaaniwa vikali, ikiwa ni pamoja na katika kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Lakini Moscow inadai kuwa vikosi vya Ukraine vilichoma moto wenyewe hivyo nchini Urusi kuripoti kitu kingine tofauti na hicho ni kinyume cha sheria.
"Baada ya yote yaliyotokea kwangu, jambo moja ninalolielewa ni kwamba ninachokifanya kina maana. Nilikuwa nikijiuliza: Je, taarifa zangu zinaweza kuzuia vita? Sasa najua kwamba angalau zinagusa mahali sahihi ", anasema.
Kila mahali katika Andriivka imeharibiwa, inaonekana jinsi vita ilivyoangamiza Waukraine.
Hatari na matokeo ya vita hivi ni kali zaidi kwa Waukraine, kama kila inchi iliyoharibika ya Andriivka inavyoonyesha.
"Tumepitia mengi. Hofu, maafa, mengi ". Alina Petrovna anasema huku mwanawe akitundikia turubai juu ya mashimo yaliyoachwa kwenye paa lao kutokana na makombora yaliyorushwa.
Bibi huyo mzee aliishi kwenye eneo la mboga za familia kwa siku 29 baada ya wanajeshi wa Urusi kuteka kijiji chake. Aliogopa sana.

Kuna mashimo ya risasi katika mlango wa mbele, kwa sababu wanajeshi walifyatua risasi ili kuwaibia.
Kitu pekee walichoacha bila kuguswa ni sanamu zake.
"Wacha watu wa Urusi waje kuona jeshi lao linafanya nini kwetu", Alina anasema, huku macho yake yakiwa yamejaa machozi, "hofu na madhila!" akarejelea maneno hayo.
Lakini idadi kubwa ya watu nchini Urusi hawatajua chochote kuhusu maovu yaliotendwa na wanajesho wao nchini Ukraine.
Kwa sababu Vladimir Putin si tu anapambana kivita na jirani wa Urusi pia anapigana vita dhidi ya ukweli.












