Matajiri wa Urusi: Wanaficha wapi 'pesa zao haramu'?

roubles, euros, dollars, sterling notes

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa miongo kadhaa, Matajiri wakubwa wa Urusi wamekuwa wakihamisha kutoka nchi moja hadi nchi nyingine au ughaibuni mabilioni ya dola walizopata kwa njia haramu, na kuziweka katika kampuni fiche na kufanya kuwa vigumu kuzifikia.

Sasa, mataifa kote duniani yanachukua hatua ya kutafuta mabilioni hayo.

Je, kuna pesa ngapi 'haramu' za Kirusi duniani kote?

Baraza la washauri la Marekani la Atlantiki linasema kuwa Warusi wana takriban $1tn ya kile inachokiita "fedha haramu" za matajiri wa nchi hiyo zilizofichwa nje ya nchi.

Ripoti yake ya 2020 ilikadiria kuwa robo moja ya kiasi hiki inadhibitiwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin na washirika wake wa karibu - Warusi matajiri wanaojulikana kama "viongozi tajiri sana wa kibiashara na wenye ushawishi mkubwa wa kisiasa."

Pesa hizi zinaweza kutumiwa vibaya na kuchangia katika ujasusi, ugaidi, ujasusi wa kiviwanda, hongo, njama za kisiasa, habari potofu, na madhumuni mengine mengi maovu," ripoti hiyo ilisema.

Pesa hizi haramu zilipatikana vipi?

Shirika lingine la wataalam la Marekani, Wakfu wa Kitaifa wa Demokrasia, linasema Putin amewahimiza washirika wa karibu "kuiba kutoka kwa bajeti ya serikali, kupora pesa kutoka kwa biashara za kibinafsi, na hata kupanga unyakuzi wa moja kwa moja wa biashara zenye faidi."

Inasema kwamba kwa njia hii, wamejitengenezea utajiri kibinafsi unaoingiza makumi ya mabilioni.

Viongozi wa upinzani wa Urusi Boris Nemtsov na Vladimir Milov wamedai kuwa kati ya 2004 na 2007, $60bn zilihamishwa kwa kampuni zilizosajiliwa katika mataifaya nje kwenda kwa wapambe wa Putin.

Nyaraka zinazovuja za Pandora Papers na Muungano wa Kimataifa wa Wanahabari wa Uchunguzi, zinabainisha kuwa watu wa karibu wa Putin wamekuwa matajiri sana - na wanaweza kumsaidia kusafirisha utajiri wake mwenyewe.

Pesa hizo zinashikiliwa wapi?

Kihistoria, kiasi kikubwa cha fedha hizi zimekwenda Cyprus - kulikochangiwa na kodi za kuvutia.

Kulingana na Baraza la Atlantiki, $36bn ya pesa za Urusi zilienda huko mnamo 2013 pekee.

Kiasi kikubwa cha fedha hizo zilifika kupitia kampuni zilizosajiliwa katika mataifa ya nje, ambayo hutumiwa kuficha wamiliki wa kweli.

Mnamo mwaka wa 2013, Shirika la Fedha la Kimataifa liliishawishi Cyprus kufunga makumi ya maelfu ya akaunti za benki zinazomilikiwa na kampuni za mataifa ya nje.

Cyprus ni mahali maarufu kwa pesa za Urusi hivi kwamba limepewa jina la utani la 'Moscow on the Med'

High-angle shot of a yacht marina in the British Virgin Islands

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Visiwa vya Virgin vya Uingereza ni mahali pa kupendeza kwa pesa za Urusi

Maeneo ya Ngambo ya Uingereza kama vile Visiwa vya Virgin vya Uingereza na Visiwa vya Cayman, pia ni sehemu zinazopendwa zaidi.

Ripoti ya Global Witness ilisema kuwa mnamo 2018, viongozi tajiri sana wa biashara na wenye ushawishi mkubwa wa kisiasa wa Urusi walikuwa na wastani wa $45.5bn katika maeneo haya yasiyotoza kodi nyingi.

Baadhi ya pesa hizi hufika hadi kwenye miji mikuu ya fedha kama vile New York na London, ambapo zinaweza kuwekezwa na kuvuna mapato.

Shirika la kupambana na ufisadi la Transparency International linadai kwamba angalau $2bn (£1.5bn) ya mali ya Uingereza inamilikiwa na Warusi wanaoshutumiwa kwa uhalifu wa kifedha, au wanaohusishwa na Kremlin.

Upana wa utakatishaji fedha wa Urusi ulifichuliwa zaidi katika ripoti ya 2014 ya Mradi wa Kuripoti Uhalifu na Ufisadi.

Ilisema kuwa kati ya mwaka wa 2011 na 2014, benki 19 za Urusi zilifuja $20.8bn kwa kampuni 5,140 katika nchi 96.

Pesa inafichwaje?

Njia ya kawaida ambayo viongozi tajiri sana wa biashara na wenye ushawishi mkubwa wa kisiasa wa Kirusi huficha pesa zao "hizo haramu" nje ya nchi ni kupitia makampuni ya nje ya nchi.

"Viongozi hao wa kibiashara wenye ushawishi" huajiri wanasheria bora, wakaguzi wa hesabu, mabenki, na washawishi duniani ili kuunda njia za kisheria za kuficha na kufuja fedha zao," linasema Baraza la Atlantiki.

Kiongozi mkubwa ana makampuni nje ya nchi yasiyojulikana katika mamlaka, na fedha zake huhamishwa kwa kasi kubwa sana."

Mnamo mwaka 2016, Muungano wa Kimataifa wa Wanahabari wa Uchunguzi ulichapisha Karatasi za Panama, ambazo zilionyesha kampuni moja pekee ilikuwa imeanzisha kampuni 2,071 nje ya nchi kwa Warusi matajiri.

Je, ni hatua gani zinachukuliwa ili kugundua pesa za matajiri hao?

Kufuatia uvamizi wa Ukraine, nchi zimetangaza msururu wa hatua za kufuatilia pesa za Urusi.

Marekani inaunda kikosi kazi kipya cha "KleptoCapture" ili kukabiliana na fedha za matajiri wa Urusi wenye ushawishi.

Itaendeshwa na Idara ya Haki na inakusudiwa kutwaa mali iliyopatikana kwa njia isiyo halali.

Serikali ya Uingereza imechukua hatua kuongeza matumizi yake ya Kanuni za Utajiri Zisizoelezeka, ambazo zinawalazimu watu kuthibitisha walikopata pesa taslimu za kununua mali nchini Uingereza.

A street in Nicosia, Cyprus, with a signboard saying "Russian products"

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Maelezo ya picha, Cyprus ni mahali maarufu kwa pesa za Urusi hivi kwamba limepewa jina la utani la 'Moscow on the Med'

Amri za Kufungia Akaunti huruhusu mahakama kufungia fedha katika benki au jumuiya ya majengo ikiwa zinashuku kuwa pesa hizo zinahusishwa na shughuli za uhalifu.

Na serikali imeidhinisha Sheria ya Uhalifu wa Kiuchumi, yenye sajili ya umiliki wa manufaa kwa mali inayomilikiwa na mashirika ya ngambo.

Uingereza pia imefutilia mbali "mpango wake wa visa kwa wawekezaji", ambao hutoa haki za makaazi kwa matajiri wa kigeni ikiwa watawekeza kiasi kikubwa cha pesa nchini humo.

Malta, kimbilio linalopendwa zaidi la Ushuru kwa Urusi, pia imefuta mpango wake wa "pasipoti ya dhahabu" ambayo iliruhusu wababe wa kibiashara kununua uraia.

Cyprus na Bulgaria zilitupilia mbali mipango yao ya pasipoti mnamo mwaka 2020.

Mengi zaidi