Mzozo wa Ukraine: Hatua kali za usalama zinazotumiwa kumlinda Rais Putin

Vladimir Putin junto a sus guardias de seguridad

Chanzo cha picha, Getty Images

Hakuna kitu kinachopuuzwa katika maisha ya Vladimir Putin.

Kila hatua ya anayochukuliwa na Rais wa Urusi inafuatiliwa kwa karibu na mamia ya walinzi wanaoandamana naye saa 24 kwa siku.

Chakula chake kinandaliwa kwa makini na vinywaji vyake vyote lazima vilindwe na washauri wak ewa karibu.

Hii ni kwa sababu afisa huyu wa zamani wa KBG-huduma ya usalama wa Soviet- anafahamu fika juu ya vitisho vinavyomkabili, hasa wakati huu wa vita.

Putin anaongoza uvazi wan chi yake dhidi ya Ukraine na hii inaleta hatari zaidi za kiusalama.

Mengi zaidi

Lakini ni nani hasa anayehusika na ulinzi wa usalama wake? Na ni baadhi yah atua zinazochukuliwa ili kudhibiti usalama wake?

Hapa tunakufahamisha kile tunachokijua kuhusu hilo.

Kundi la walinzi mahiri

Miongoni mwa vikosi kadhaa vya usalama vinavyohudumu nchini Urusi, kuna kikosi kimoja kilicho na jukumu maalumu la kumlinda rais na familia yake: Huduma ya Usalama ya Rais wa Urusi.

Kikosi hicho kinasimamiwa na Huduma ya Ulinzi wa Jamhuri ya Urusi (FSO),ambayo asili yake ni KGB ya zamani, na ambayo pia inawalinda maafisa wengine wa ngazi ya juu wa Urusi, akiwemo Waziri Mkuu, Mikhail Mishustin.

Kikosi kinachofuata hicho ni cha wanaume wanaovalia nguo nyeusi na waliona vifaa maaalum vya kusikiza masikioni, hawa wanamlinda rais usiku na mchana.

Kulingana na Russia Beyond, chombo kinachomilikiwa na serikali, walinzi hawa wanapokusindikiza kwenye shughuli ya nje ya nchi, hujipanga kwenye miduara minne.

Mduara wa karibu zaidi unaundwa na walinzi wake wa kibinafsi.

Mduara wa pili unajumuisha walinzi ambao hawawezi kutambuliwa hadharani.

Mduara wa tatu unazunguka eneo la umati wa watu kuzuia watu wanaotiliwa shaka kuingia. Na mduara wa mwisho, ni wa walenga shabaha walio juu ya majengo yaliyokaribu.

Mlenga shabaha wa FSO akiwa kwenye moja ya kuta za Kremlin, katikati mwa Moscow.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mlenga shabaha wa FSO akiwa kwenye moja ya kuta za Kremlin, katikati ya Moscow.

Walinzi hawa pia huandamana na Putin kutoka sehemu moja hadi nyingine.

"Putinhapendelei kutumia helikopta; mara nyingi anaandamana na msafara mkubwa wa pikipiki, magari mengi meusi na kadhalika.

''Maeneo anayopitia wakati huo ndege yoyote isiyo na rubani inazuiwa kupaa angani na magari yote yanasimamishwa hadi msafara wake upite'', anasema Mark Galeotti, mtalamu wa usalama wa Urusi na Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi Mayak, ambalo limepewa jukumu la kuchanganua masuala ya usalama nchini humo, aliambia BBC Mundo.

Huduma ya Usalama wa Rais wa Urusi inasiadiwana " Jeshi la Ulinzi la Urusi " , ama Kikosi cha Rosgvardia, ambacho kilibuniwa na Putin mwenyewe miaka sita iliyopita na imetajwa na wengine kama "jeshi la kibinafsi " la rais.

Kikosi hicho ni huru katika vikosi vya Wanajeshi wa Urusina, ingawa dhamira yake ni kulinda mipaka, kukabiliana na ugaidi na kulinda usalama wa wananchi miongoni mwa majukumu mengine, kipaumbele chake ni kumlinda Putin dhidi ya vitisho vya aina yoyote vinavyoweza kujitokeza

"Kila mmoja anajua kwamba kikosi hicho ni cha walinzi wa kibinafsi wa Putin," Stephen Hall, mwanazuoni wa Urusi katika Chuo Kikuu cha Bath, Uingereza, aliambia BBC Mundo."Na rais sana sana analindwa na kikosi hicho na vikosi vingine vya usalama," aliongeza.

Mkuu wa sasa wa Jeshi laUlinzi wa Kitaifa ni Viktor Zolotov, mlinzi wa zamani wa Putin

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mkuu wa wa sasa wa jeshi Jeshi la Ulinzi wa Kitaifa ni Viktor Zolotov, mlinzi wa zamani wa Putin

Kwa sasa anayeongoza Walinzi wa Kitaifa ni Viktor Zolotov, mlinzi wa zamani wa Putin. Zolotov mwandani wa karibu wa rais na katika miaka ya hivi karibuni ameongeza idadi ya wanajeshi ambao ni sehemu ya kikosi hiki cha usalama kwa karibu 400,000.

Je, ni hatua gani zinachukuliwa ili kumlinda?

Ingawa ni vigumu kujua ni kwa kiwango gani hatua zinazochukuliwa kumlinda Putin zinakwenda, Kremlin yenyewe na wataalam wa usalama wa Urusi wametoa mwanga kuhusu suala hilo.

Moja ya masuala ambayo yanachukuliwa kwa tahadhari zaidi ni chakula.

Kulingana na Mark Galeotti, akihofia kuwekewa sumu, Putin ana mwonjaji wa kibinafsi ambaye hukagua kila kitu ambacho rais anaenda kula

El presidente Putin en una cena oficial.

Chanzo cha picha, Getty Images

"Ni sehemu ya mtindo ambao uko karibu na mfalme wa zama za kati kuliko rais wa kisasa," anaiambia BBC Mundo.

Pia, anaposafiri nje ya Urusi, timu ya Rais inashughulikia kila kitu unachotumia.

"Wanabeba chakula na vinywaji vyote ambavyo atatumia. Kwa hiyo, kwa mfano, ikiwa kuna tosti rasmi ya mvinyo, anachukua kutoka kwenye chupa ambayo timu yake inamletea, si kutoka kwa wengine," anaelezea Galeotti.

Stephen Hall, kwa upande wake, anasema kwamba walinzi wake wa kibinafsi huangalia kwa karibu jinsi anavyopikiwa ili kuepusha hatari yoyote.

Simu janja

Hatua nyingine ambayo imechukuliwa kumlinda ni kuzuia simu mahiri ndani ya Kremlin.

Rais wa Urusi mwenyewe amethibitisha kuwa hatumii vifaa hivi.

Mnamo mwaka wa 2020, katika mahojiano na shirika la habari la serikali ya Urusi TASS, alikiri hivyo, akionyesha pia kwamba ikiwa anataka kuwasiliana na mtu, kuna laini rasmi wa kufanya hivyo.

Washauri wake pia wamekubali hivyo. Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema mara kwa mara kwamba Putin hatumii simu za mkononi kwa sababu "hana muda mwingi."

Gari maalum lenye silaha

Chanzo cha picha, Mikhail Svetlov

Maelezo ya picha, Gari maalum lenye silaha

Lakini ukweli ni kwamba miongoni mwa sababu zinazoeleza kusita kwa Putin kutumia teknolojia hii ni kutokuwa na imani kubwa na mtandao.

Huko nyuma, kwa kweli, aliwahi kuashiria kuwa mtandao ni "mradi wa CIA" - Shirika la ujasusi la Amerika - na ametoa wito kwa Warusi kutofanya upekuzi wa Google kwa sababu anaona kuwa Wamarekani wanafuatilia habari zote.

"Putin haitumii mitandao, inajulikana kuwa hapendi simu. Na vizuri, hebu tuwe waaminifu, kutoka kwa mtazamo wa usalama, Putin yuko sahihi kabisa. Simu za mkononi si salama sana, "anasema Galeotti.

Kutokana na hili, msomi huyo anathibitisha kwamba Putin anafahamishwa kupitia faili za karatasi ambazo washauri wake wanampa.

Rais wa Urusi hatumii simu aina ya smartphone.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais wa Urusi hatumii simu aina ya smartphone.

"Anaanza siku yake kwa taarifa tatu za kiusalama. Moja ni kile kinachoendelea duniani, kisha kinachoendelea nchini Urusi, na tatu ni kile kinachoendelea ndani ya watu mashuhuri," anasema.

"Kwake, hii ndiyo habari muhimu zaidi na ambayo itaeleza siku yake itakuaje."

"Nakumbuka nilizungumza na wanadiplomasia na maofisa wa wizara ya mambo ya nje ambao waliniambia wamechanganyikiwa kwamba ikiwa watakuwa na taarifa zinazokinzana na huduma zao za kijasusi, Putin ataelekea kudhani kuwa majasusi wake wako sahihi na wanadiplomasia wana makosa.", anaongeza.

Kutengwa wakati wa janga la Covid

Hivi sasa, ni vigumu sana kumfikia Vladimir Putin.

Viongozi wachache wanaokutana naye lazima wafanye hivyo kwa kuheshimu mita kadhaa za umbali. Inakumbukwa wakati akikutana na mwenzake wa Ufaransa, Emmanuel Macron, ambaye alilazimika kukaa upande mwingine wa meza ndefu.

Sehemu ya hatua hizi zimerithiwa kutoka kwa janga la Covid.

La reunión entre Putin y Macron

Chanzo cha picha, Getty Images

Yeye hasafiri mara nyingi nchini na kuonekana kwake kwenye hafla za umma sio kawaida kabisa. Walinzi wa usalama ni miongoni mwa watu wachache ambao Putin ana uhusiano wa kibinafsi nao," anasema.

Kulingana na Galeotti, hii inaelezea, kwa sehemu, kwa nini wengi wao wameteuliwa kushika nyadhifa za juu (kama ilivyo kwa Viktor Zolotov, katika National Guard).

Vladimir Putin bajándose de un auto junto a su guardaespaldas.

Chanzo cha picha, Getty Images

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kijasusi wanasema hatua kali za usalama zinazomzunguka Putin kwa kiasi fulani zinaelezewa kuwa "paranoia" ya kirusi/Aina ya uwoga kuhusu usichojua.

Wengine wanasema kwamba rais, kwa tajriba yake katika KGB, anajua vyema kuliko mtu yeyote jinsi ilivyo muhimu kulinda usalama wake mwenyewe.

Kuwa hivyo iwezekanavyo, kila kitu kinaonyesha kwamba ulinzi na kutengwa kwake kunaongezeka tu. Na kwamba, kama Galeotti anasema, mambo yanafanywa huko Kremlin "kama Putin anavyotaka yafanywe."