Vita vya Ukraine: Ukraine imefanya nini kufanikiwa vitani dhidi ya Urusi?

Chanzo cha picha, Reuters
Mwezi mmoja katika uvamizi huu na hadi sasa, Ukraine imekaidi dhana kwamba inbelemewa haraka. Wakizidiwa kwa idadi ya kila kipimo - katika vifaru, askari, ndege - vikosi vya Ukraine, vilivyoimarishwa na raia wa kujitolea, katika sehemu nyingi wamepigana na jeshi la Urusi hadi kufika kiwango cha kutokuwa na mshindi wa wazi.
Wamepoteza maeneo, haswa kusini karibu na Crimea, ambayo tayari ilichukuliwa na kutwaliwa na Urusi mnamo 2014. Lakini lengo la awali la Moscow la kunyakua mji mkuu wa Kyiv na miji mingine mikubwa haraka, na kuilazimisha serikali kujiuzulu, imeshindwa.
Wimbi bado linaweza kugeuka dhidi ya Ukraine. Vikosi vyake vinapungua kwa hatari kwenye makombora muhimu ya kuzuia vifaru na silaha zinazotolewa na nchi za magharibi zinazohitajika kuwalinda dhidi ya Warusi wanaosonga mbele.
Vikosi vingi vya kawaida vya Ukraini vilivyo vilivyo mashariki mwa nchi viko katika hatari ya kuzingirwa, kukatwa na kuangamizwa. Na kwa robo ya wakazi wa taifa hilo wamekimbia makazi yao, wale waliokaa waliweka hatari ya kuona miji yao ikigeuzwa kuwa jangwa kutokana na mashambulizi ya Urusi ya roketi.
Hata hivyo pamoja na mambo haya, vikosi vya Ukraine vinaishinda Urusi katika vita hivi, kwa viwango kadhaa. Wiki hii msemaji wa Pentagon John Kirby aliwasifu kama wanaotetea sehemu za nchi yao "kwa akili sana, kwa uhodari sana, kwa ubunifu sana". Kwa hivyo ni nini hasa zimekuwa siri za mafanikio yao?
1. Wana motisha na ari kubwa sana

Chanzo cha picha, EPA
Kuna tofauti kuwa sana kati ya ari ya majeshi hayo mawili. Raia wa Ukraine wanapigania uhai wa nchi yao kama taifa huru, wakishangazwa na hotuba ya mkesha wa vita ya Rais Putin ambapo alisema kuwa Ukraine ni nchi bandia iliyoundwa na Urusi
Wananchi wa Ukraine wameunga mkono serikali yao na rais wao. Hii imesababisha raia wasio na uzoefu wa kijeshi kuchukua silaha kwa urahisi ili kulinda miji yao licha ya nguvu kubwa ya kijeshi kutoka kwa Urusi
"Hivi ndivyo watu wanavyopigania kuwepo kwao," anasema Brigedia Tom Foulkes, ambaye alihudumu miaka 35 kama afisa wa Jeshi la Uingereza nchini Ujerumani wakati wa Vita Baridi. "Hivi ndivyo wanavyolinda nchi yao na familia zao. Ujasiri wao ni wa kushangaza na wa kupendeza."
Hatua hiyo imewaweka huru askari wa Kiukreni kwenda kupigana kwenye mstari wa mbele, wakijua miji yao ina ulinzi wa kina.
Kinyume chake, wanajeshi wengi wa Urusi waliotumwa kupigana nchini Ukraine ni askari waliotoka shuleni, wamechanganyikiwa kwa kujikuta katika eneo la vita wakati walidhani walikuwa wakiendelea na mazoezi tu.
Wengi walikuwa na maandalizi kidogo ya vita au hawakujua lolote kwa ajili ya ukali wa mapigano waliyokumbana nayo. Kumekuwa na ripoti za wengine kutoroka jeshini, uhaba wa chakula na uporaji.
2. Komandi na udhibiti

Chanzo cha picha, EPA
Matarajio ya mapema ya shambulio baya la mtandaoni la Urusi, na kuondoa mawasiliano ya Ukraine, hayakutimia. Badala yake, Ukraine kwa namna fulani imeweza kudumisha uratibu mzuri katika maeneo kadhaa ya vita, hata pale ambapo imepoteza ardhi.
Serikali yake imekaa mjini Kyiv na imebakia kuonekana sana, huku hata naibu waziri mkuu akiwa amevalia fulana ya kaki akihutubia taifa .
Jeshi la Urusi, kinyume chake, halionekani kuwa na aina yoyote ya uongozi wa umoja, na uratibu mdogo kati ya vita vyake tofauti.
Hii inawezekana ikawa na athari mbaya kwa ari ya kijeshi ya Urusi. Imependekezwa kuwa vifo vilivyoripotiwa vya majenerali watano wa Urusi kwa kiasi fulani ni matokeo ya kulazimika kukaribia mapigano ili kuwaondoa wanajeshi wao waliolemewa vitani.
3. Mbinu kabambe

Chanzo cha picha, Reuters
Vikosi vya Ukraine vimezidiwa kwa idadi kubwa na bado wametumia ardhi na silaha zao vizuri zaidi kuliko Warusi .
Ingawa Warusi wameelekeza nguvu zao katika safu za polepole, nzito za kivita, mara nyingi magari yakiwa yamekusanyika karibu, Waukraine wamefaulu kufanya uvamizi wa kushambulia na kukimbia, wakiingia kisiri na kurusha kombora la kuangamiza kifaru kisha kutoweka kabla ya Warusi kujibu.
Kabla ya uvamizi huo, wakufunzi wa Nato kutoka Marekani, Uingereza na Kanada walikaa kwa muda mrefu nchini Ukraine, wakiongeza vikosi vyake katika vita vya kujihami na kuwaelekeza jinsi ya kutumia vyema mifumo ya kisasa ya makombora kama vile Javellin au silaha ya NLAW iliyoundwa na Uswidi au toleo jipya zaidi la Stinger.
"Waukraine wamekuwa wajanja zaidi kuliko Warusi", anasema Prof Clarke, "kwa sababu wamepigana wakitumia silaha zao zote jambo ambalo Warusi hawajafanya". Kwa hili anamaanisha wametumia kikamilifu zana zote za kijeshi walizo nazo, kama vile ndege zisizo na rubani, mizinga, askari wa miguu na vita vya kielektroniki.
Zikiunganishwa pamoja, jumla ya vipengele hivi vyote tofauti vya vita vinaweza kuunda athari kubwa kuliko jumla ya sehemu zake.

Mtaalamu mwingine wa mikakati wa kijeshi, Justin Crump, ambaye anaendesha shirika la ushauri la kijasusi la Sibylline, anasema Waukraine wamekuwa wastadi wa kutafuta maeneo ambayo yanaweza kuathiriwa na muundo wa Urusi na kuyapiga sana. "Ukraine imetumia mbinu zenye ufanisi mkubwa", anasema, ikiwa ni pamoja na kulenga maeneo dhaifu ya Urusi kama vile misafara ya vifaru , kutumia mifumo ya silaha zinazotolewa na Nato kwa matokeo mazuri dhidi ya malengo ya usahihi na kuboresha inapohitajika.
Ingawa ni vigumu kupata picha sahihi ya takwimu za majeruhi, hata makadirio adimu yaliyotolewa na Pentagon yaliweka vifo vya wapiganaji wa Urusi kuwa zaidi ya 7,000. Hiyo ni karibu nusu ya wanaume wengi kama Wasovieti walipoteza katika miaka 10 ya mapigano nchini Afghanistan na sasa ni mwezi mmoja tu katika vita hivi.
Brig Tom Foulkes pia ana maelezo kwa nini majenerali wengi wa Urusi wanauawa kwenye mstari wa mbele: "Hii inaonekana kwangu kama kampeni ya makusudi na yenye mafanikio makubwa ambayo inaweza kudhalilisha miundo Komandi ya Urusi
4. Vita vya Habari

Chanzo cha picha, HO/EPA
Na kisha kuna vita vya habari. Ukraine inashinda hatua hii ya chinichini katika sehemu kubwa za dunia - ingawa haiko nchini Urusi ambako Kremlin bado inadhibiti ufikiaji wa vyombo vingi vya habari.
"Ukraine imehamasisha nyanja ya habari kwa manufaa makubwa ya ndani na kimataifa," anasema Justin Crump. "Hii imetoka juu kwenda chini, ikisaidiwa na (Rais) Zelensky mwenye ujuzi mkubwa wa vyombo vya habari."
Ni maoni yaliyoungwa mkono na Dk Ruth Deyermond, mhadhiri mkuu wa masomo ya baada ya Usovieti katika Chuo cha Kings London. "Ni wazi kuwa serikali ya Ukraine imefanikiwa sana kudhibiti simulizi kuhusu vita, hakika kwa ulimwengu mzima," anasema. "Kile ambacho mzozo huo umefanya kwa ajili ya hadhi ya kimataifa ya Ukraine ni cha ajabu kabisa."
Lakini hivi sasa, mwezi mmoja katika mapambano haya ya kukata tamaa ya maisha na kifo kwenye mipaka ya mashariki ya Ulaya, ambayo bado inaweza kuwa haitoshi kuokoa Ukraine.
Nguvu ya nambari ya jeshi la Urusi, pamoja na mapungufu yake yote, haisadii upande wa Ukraine. Ikiwa kwa namna fulani ugavi wa mifumo ya silaha kutoka Nato utakauka basi kunaweza tu kuwa na muda mrefu zaidi wa taifa hili lililokabiliwa na hali ngumu kuweza kushikilia mstari na kujiokoa
Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine















