Mzozo wa Urusi, Ukraine: Nani mwenye uwezo iwapo vita vitatokea?

Chanzo cha picha, RUSSIAN DEFENCE MINISTRY
Ukraine inasubiri kuona ni hatua gani inayofuata itakayochukuliwa na Urusi huku kukiwa na hali ya kutoaminiana na kuhusu hofu ya mashambulio katika kanda hiyo ya Ulaya Mashariki.
Mashirika mbali mbali ya ujasusi ya magharibi yameionya mara kadhaa kwamba Urusi itaivamia jirani yake Ukraine.
Rais Biden hivi karibuni alitangaza kwamba anatarajia rais wa Urusi kuingilia masuala ya ndani ya Ukraine, lakini anataka kuzuwia vita.
Tayari Bidena ameelezea hofu juu ya uingiliaji kati wa jeshi la Urusi katika Ukraine.
Rais wa Volodymyr Zhelensky alijibu wiki iliyopita akisema kuwa "Hakuna maisha yaliyopotea kwa upande wetu. Kwahiyo hakuna Uingiliaji hapa . "
Urusi, kwa upande mwingine, imekuwa ikiwapeleka wanajeshi zaidi ya milioni kwenye mpaka wake na Ukraine katika kipindi cha wiki chache zilizopita. Hatahivyo, Urusi imekuwa ikilaani shambulio dhidi ya Ukraine kuanzia mwanzoni.
Madai ya Urusi kwa nchi za Magharibi
Ombi kuu la Urusi ni kwamba Ukraine isiruhusiwe kamwe kujiunga na NATO. Iliutaka Muungano wa NATO kuacha harakati zake zote za kijeshi katika Ulaya Mashariki.
Huku hali ya wasi wasi ikiendelea kuongezeka, wiki hii Marekani iliruhusu nchi kadhaa kutuma silaha zake ili kuisaidia Ukraine.
"Iwapo Urusi itaingilia Ukraine, kutakuwa na ulipizaji wa haraka na thabiti kutoka kwa Marekani na washirika wake," alisema Wazir iwa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken.
Joe Biden, kwa upande wake,alirejelea kauli yake ya awali kwamba uvamizi ndani ya Ukraine utachukuliwa kama shambulio.
Anthony Blinken alikutana na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Ulaya katika mji mkuu wa Ujerumani Berlin kujadili uratibu wa nchi za Ulaya wa kukabiliana na uvamizi wa Ukraine.
Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema kwamba kuhusika kwa Urusi katika Ukraineni hatari kwa dunia.

Chanzo cha picha, Wizara ya ulinzi ya Urusi
Agosti 2021, Ilifanya mazoezi makubwa ya kijeshi katika Crimea, na muda mfupi baadaye silaha nzito zilipelekwa karibu na jimbo la Donbass mwashariki mwa Ukraine.
Wiki chache baadaye, hatahivyo, iliondoa vikosi vyake pale. Lakini sasa vikosi vya Urusi vimepelekwa tena Donbass.
Urusi imekuwa ikipeleka wanajeshi wake mara kwa mara katika jimbo hilo trangu Novemba mwaka, na kwa ushirikiano na taifa jirani la Belarus, vikosi vya nchi mbili zinapanga kufanya kufanya mazoezi ya kijeshi katika Belarus.
Urusi inataka nini hasa?
Rais wa Urusi Vradimir Putin kwa muda mrefu amekuwa kiishutumu Marekani kwa kukiuka ahadi yake iliyoitoa miaka 1990 kwamba NATO haitapanua uwepo wake katika eneo la Ulaya mashariki na sasa imekiuka ahadi hiyo.
"Wametukatisha tamaa," Putin aliuambia mkutano wa waandishi wa habari mwezi uliopita. Hatahivyo kulikuwa na tofauti baina ya pande mbili juu ya uhakikisho lililotolewa wakati huo na kiongozi wa Muungano wa Usovieti Mikhail Gorbachev.
Tayari, nchi za Ulaya Mashariki na Ulaya ya Kati ambazo zilikuwa tayari ni wajumbe wa Muungano wa Usovieti zamani, au chini ya ushawishi wake, walikuwa sehemu ya NATO.
Miongoni mwao wakiwa ni Poland, Lithuania, Latvia na Estonia ambazo zinpakaa na Urusi.
Urusi inadai kupanuka kwa NATO, jeshi lake na sialha ni tisho kwa usalama wake.
Urusi iliitwaa Crimea mwaka 2014, ikidai kuwa ilikuwa na haki za kihistoria, Ukraine ilikuwa sehemu ya Muungano wa Usovieti.

Chanzo cha picha, REUTERS
Putin anaadhimisha kuanguka kwa Muungano wa Usoviet katika mwaka 1991 kama "fanikio la kihistoria". Katika makala ndefu ya mwaka jana, Putin alisema kuwa Warusi na Waukraine wana "utaifa mmoja." Wataalamu wanaamini kwamba hii inafichua wazo la Putin.
Katika makala hiyo, Putin pia alimkosoa kiongozi wa sasa wa Ukraine kwa kuendesha "mradi wa kupinga Urusi".
Unaweza pia kusoma:
Ukraine, kwa upande mwingine, inapakana na Urusi katika mashariki mwa Urusi na Muungano wa Ulaya upande wa magharibi. Hatahivyo, kutokana na kwamba ni mjumbe wa Muungano wa zamani wa Usovieti, Ukraine pia ina uhusiano wa ndani wa kijamii na wa kiutamaduni na Urusi.
Urusi itafanya nini kwa Ukraine
Urusi ilitoa uungaji mkono wake kwa makundi yanayotaka kujitenga ambao walitwaa maeneo ya mashariki mwa Ukraine.
Tangu wakati huo, zaidi ya watu 14,000 waliuawa katika mapigano baina ya waasi wanaounga mkono Urusi na vikosi vya Ukraine.
Mzozo baina ya waasi na jeshi la Ukraine Tunaendelea hadi leo.












