Mzozo wa Ukraine: Rais Zelensky ashtumu matamshi ya Biden

Joe Biden

Chanzo cha picha, Getty Images

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameshtumu matamshi yaliotolewa na mwenzake wa Marekani Joe Biden 'kuhusu uvamizi' mdogo wa Urusi katika taifa lake.

Bwama Biden alikuwa amependekeza kwamba uvamizi mdogo huenda ukavutia majibu ya kiwango kama hicho kutoka kwa Marekani na washirika wake.

Lakini bwana Zelenskyalituma ujumbe wa twitter akisema: hakuna uvam,izi mdogo . sawa na kwamba hakuna majeruhi madogo na huzuni mdogo kutokana na kupoteza wapendwa.

Urusi ina takriban wanajeshi 100,000 karibu na mpaka lakini inakanusha kupanga uvamizi

Rais Vladmir Putin ametoa masharti , akisisitiza kuwa Ukraine haipaswi kamwe kuruhusiwa kujiunga na Nato na kwamba muungano huo wa kujihami unapaswa kuacha shughuli za kijeshi mashariki mwa Ulaya.

Rais Biden aliambia mkutano wa wanahabari kwamba Bw Putin angelipa "gharama kubwa'' kwa kuivamia Ukraine, lakini pia akadokeza kwamba huenda ikategemea jinsi Urusi itakavyotekeleza uvamizi huo.

"Unachokiona ni kwamba Urusi itawajibishwa ikiwa itavamia na inategemea na inafanya nini," alisema.

Mwanajeshi wa Ukraine akipiga doria katika mpaka wa mashariki na Urusi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwanajeshi wa Ukraine akipiga doria katika mpaka wa mashariki na Urusi

Maoni yake yalizua maswali juu ya jinsi Marekani inaweza kujibu uvamizi wa Urusi na maafisa wamekuwa wakikimbilia kufafanua msimamo wa Washington.

"Tumekuwa wazi sana kote," Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema Alhamisi, akiongeza kwamba uvamizi wowote wa Urusi ndani ya Ukraine utakabiliwa na "jibu la haraka, kali na la umoja" kutoka kwa Marekani na washirika wake.

Siku ya Alhamisi, Bw Biden mwenyewe alisema kwamba kuingia kwa wanajeshi wa Urusi kutachukuliwa kama "uvamizi".

Presentational grey line

Uchambuzi wa Anthony Zucher, -Mwandishi wa Marekani kaskazini

Mjini Berlin siku ya Alhamisi, Antony Blinken alisema Marekani imekuwa "wazi sana". Hatua yoyote ya jeshi la Urusi kuelekea Ukraine itakabiliwa na "jibu la haraka na kali".

Usiku uliopita, hata hivyo, Rais Biden hakuwa na uhakika kabisa - akitofautisha uvamizi mkubwa kutoka kwa "mavamizi madogo" ambayo yanaweza kusababisha athari ndogo zaidi.

Huenda huo ulikuwa ufichuzi wa wazi kutoka kwa rais wa Marekani, kupitia utabiri wake kwamba Bw Putin "atavamia" Ukraine. Lakini ilipunguza juhudi za Bw Blinken kusema kwamba lilikuwa chaguo kwamba kwa Urusi kuamua kati ya diplomasia na mzozo, bila msingi wowote wa katikati.

Bw Blinken alizungumzia zaidi suala hilo wakati wa hotuba yake ya Alhamisi alasiri, labda ili kutia moyo hisia za washirika wa Marekani waliokusanyika mjini Berlin. Huu haukuwa "mzozo wa kikanda wa mbali", alisema, bali ni tishio kwa kanuni za kimataifa za uhuru na kujitawala. Ikiwa Urusi ilitaka vita baridi mpya, Marekani na washirika wake walikuwa tayari.

Maneno hayo - na ya Bw Biden - yatagonga vichwa vya habari wakati Bw Blinken atakapokutana na mwenzake wa Urusi katika mkutano wa Geneva siku ya Ijumaa.

line

Bw Blinken alikuwa akizungumza nchini Ujerumani baada ya kukutana na mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi muhimu za Ulaya kwa mazungumzo yenye lengo la kuratibu mkakati wa nchi za Magharibi kuhusu uwezekano wa uvamizi wa Ukraine. Anatarajiwa kukutana na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov huko Geneva siku ya Ijumaa.

Kremlin hapo awali ilionya kwamba maoni ya Bw Biden yanaweza kuyumbisha zaidi hali hiyo.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson alisema kwamba uvamizi wowote wa Urusi ndani ya Ukraine "kwa kiwango chochote kile ... utakuwa janga kwa ulimwengu".

Lakini Je Putin anataka nini?

Rais wa Urusi amedai kwa muda mrefu kwamba Marekani ilivunja hakikisho ililoweka mwaka 1990 kwamba Nato haitapanuka zaidi upande wa mashariki. "Walitudanganya tu!", alilalamika katika mkutano wa wanahabari wa mwezi uliopita.

Ufafanuzi huo hautofautiani juu ya kile kilichoahidiwa kwa kiongozi wa wakati huo Usovieti , Mikhail Gorbachev. Lakini ni wazi kuwa Bw Putin anaamini kuwa dhamana hiyo ilitolewa.

Ramani inayoonesha jinsi Nato ilivyopanuka tangu 1997
Maelezo ya picha, Ramani inayoonesha jinsi Nato ilivyopanuka tangu 1997

Tangu wakati huo, nchi kadhaa za Ulaya ya kati na mashariki, ambazo zilikuwa sehemu ya Umoja wa Kisovieti au nyanja yake ya ushawishi, zimejiunga na Nato. Wanne kati yao - Poland, Lithuania, Latvia na Estonia - wana mipaka na Uru

Urusi inahoji kuwa upanuzi huu, na uwepo wa wanajeshi wa Nato na zana za kijeshi karibu na mipaka yake, ni tishio la moja kwa moja kwa usalama wake.

Nchi hiyo iliteka na kutwaa rasi ya Crimea kusini mwa Ukraine mwaka 2014 baada ya wananchi wa Ukraine kumpindua rais wao anayeiunga mkono Urusi. Tangu wakati huo, jeshi la Ukraine limeingia katika vita na waasi wanaoungwa mkono na Urusi katika maeneo ya mashariki karibu na mipaka ya Urusi.

Kuna hofu kwamba mzozo huo uliogharimu maisha ya watu 14,000 na kusababisha takriban watu milioni mbili kuyakimbia makazi yao, huenda ukaendelea kutawala na kwamba jeshi la Urusi litavuka mpaka.si.