Fahamu wasiwasi kuhusu mazungumzo ya nyuklia ya Iran na uwezekano wa shambulizi la Israel

Mkutano wa viongozi

Chanzo cha picha, Getty Images

Magazeti ya kiarabu yanajadili uwezekano wa mafanikio na kushindwa kwa awamu mpya ya mazungumzo ya Vienna, kati ya Iran na kundi la nchi zenye nguvu duniani, kufufua makubaliano ya Iran baada ya miezi mitano ya kusimamishwa wakati ambapo vitisho kutoka Israel dhidi ya Iran vinazidi kuongezeka.

Magazeti mengine yameandika kuhusu wasiwasi unaovuka mipaka ya programu ya nuklia ya Iran na taifa hilo kumiliki makombora na ndege zisizo na rubani hadi uwepo wa makundi yenye silaha matiifu kwake katika nchi nyingi eneo hilo.

Utabiri wa kushindwa

Gilbert al-Ashkar anaangazia uwezekano mara mbili kwa hatma ya awamu hii ya mazungmzo, ya kwanza na uwezekano kuwa yatafeli kutokana na kuwepo kwa serikali ya Iran inayowakilisha siasa kali na uwezekano mwingne ni kwamba kutakuwa na makubaliano ya muda na kundolewa kwa baadhi ya vikwazo kwa maafikiano kuwa Iran itaacha urutubishaji wa urani

Mwandishi anasema kuwa huu ndio uwezekano mbaya zaidi machoni mwa Israel kwa kuwa hilo litairuhusu Iran kuendelea na mipango yake ya nuklia

.

Chanzo cha picha, Reuters

Jalal Jaraghi, wa London's opinion today anatetea msimamo wa Iran akisema kuwa nchi za magharibi zinastahili kuondoa vikwazo na ziache kudai ridhaa kutoka Iran.

Mwandishi anasema kuwa lengo la Iran kwa sasa ni kuondolewa kwa vikwazo vilivyo sasa na kama nchi za magharibi hazikubaliani na matakwa, Iran itaendelea na shughuli zake kwa kasi.

Lakini Fawzia Rashid kutoka gazeti la Bahraini Gulf News, anaamini kelele za dunia kuhusu mpango wa nuklia wa Iran ni wa kuiandaa dunia kwa Iran yenye nuklia licha ya kuwepo vitisho vya Israel na Marekani.

WasiwasI unavuka masuala ya nyuklia

Khairallah Khairallah anasema kuwa kuanza kwa mazungumzo kunazua hofu akisema kuwa ni kawaida kwa nchi za kanda hiyo kuangalia kwa tahadhari mazungumzo yaliyoanza Vienna kati ya Tehran na Washington.

Wale wanaotaka kuishi kwa amani katika kanda hiyo ya kiarabu wana haki ya kuhofu juu ya uwezekano wa kuwepo makubaliano mapya kwenye mazungumzo ya Vienna kujaribu kufufua makubaliano ya nuklia na Iran, anasema Ernest Khoury wa gazeti lililo London la Araby Al-Jadeed.

Nchini Lebanon Nabih Burji anasema Iran imeweza kujiweka kama taifa kuu katika kanda na anaamini kuwa kurejea kwa makubaliano ya Vienna ni lazima yachangie kupunguza mzingiro wa Marekani dhidi ya Lebanon na Syria.

,

Chanzo cha picha, AFP

Uwezekano wa makabiliano na Israel

Bassam Abu Sharif kutoka london's Opinin today anasema kuwa vita vyovyote ambavyo vitaanzishwa na Israel dhidi ya Iran vinalenga kuzuia matumizi ya nishati ya nuklia katika utafiti wa kisayansi na uzalishajii katika sekta tofauti na vita dhidi ya makundi ya kupinga yanayopigania kupata haki kama uhuru wa Palestina.

Gilbert Al-Ashkar anaamini kuwa uwezekano wa Israel kufanya shambulizi la kijeshi unaongezeka muda unapokwenda na Israel inasubiri wakati bora ambapo itaionyesha dunia kuwa Iran imefikia uwezo wa kinyulkia.

LakiniI Ibrahim Nawar anasema kuwa nafasi ya Isreal kwa jumla ni dhaifu sana kuweza kupanga mikakati ya kijeshi dhidi ya mpango wa nyuklia wa Iran kwa sasa, lakini ina vifaa ambavyo inatumia kuuvuruga.

Anasema ukweli ni kwamba kuzungumza kuhusu Israel kuchukua hatua za kijeshi ni rahisi lakini kutekeleza ni kazi ngumu sana.