Baadhi ya maeneo bora zaidi ya utalii mwaka 2022 kulingana na Lonely Planet

La guía ha destacado el desierto de Atacama como uno de los lugares recomendados para visitar.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Muongozo umelitaja jangwa la Atacama kama moja ya maeneo yanayofaa zaidi kuyatembelea

Huku hali ikirejea taratibu kuwa ya kawaida duniani baada ya janga la Covid, wale ambao wana mapumziko na wana uwezo wa kwenda likizo tayari wameanza kufikiria kuhusu kusafiri.

Mojawapo ya kuchagua ni wapi kwa kwenda ni kuangalia katika orodha ya mapendekezo ya sehemu za kwenda ya Lonely Planet.

Lonely Planet ambalo ni jarida la wasafiri limechapisha taarifa kuhusu mahali bora zaidi pa kwenda kwa mwaka 2022 wiki iliyopita, huku sehemu hizo zikigawanywa kwa misingi ya nchi, miji na kanda.

Muongozo huo umependekeza sana watu watembelee kisiwa cha Cook- Cook Islands, kilichopo katikati ya bahari ya Pacific ambacho hufahamika sana kwa maji yake safi na fukwe ambazo bado hazijaharibiwa.

"Zaidi ya ubora wake wa kiutalii na muonekano wenye mvuto wa kisiwa chenyewe, kina utajiri wa utamaduni, kikiwa na maadili ya utamaduni wa Polynesia", umeeleza muongozo huo.

Maeneo mengine yaliyoljitokeza kuwa bora ni Oman , eneo muhimu kwa wapenzi wa historia na udadisi. Eneo hili limejaa makasri, ngome na misikiti.

Nchi hii ina utajiri wa kitamaduni na maeneo ya urithi wa dunia, kama vile Ngome ya Bahla na mji wa kale wa Qalhat , pamoja na maeneo mengine yenye uzuri asilia majangwa na mwambao safi ambao haujaharibiwa.

Omán ofrece varios lugares de interés para todo aquel que esté interesado en la historia.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Oman ina maneo kadhaa mazuri kwa yeyote anayependa historia

Amerika Kusini

Lonely Planet haikusahau eneo la Amerika Kusini ambapo limetaja mji wa Mexico wa Mérida katika orodha ya miji bora zaidi na jangwa la Chile la Atacama

Merida

Muongozo huo umetaja historia ya ukoloni ya Mérida, mji maarufu zaidi uliopo katika jimbo la Yucatán, unaopatikana Kusini mashariki mwa nchi, na "sifa yake ya mchanganyiko wa maisha ya kimkoa na yasiyofuata utawala wowote ."

"Ni eneo zuri kulitembelea kwa lengo la kujifunza, likiwa na mitaa meembamba medani kubwa za kati, na majumba makubwa ya katika kanda hiyo."

"Pia ni eneo linalofaa zana kuanzisha safari yako ya uzoefu mpya kuelekea katika jimbo la Yucatan. Lina mapishi bora na malazi, masoko yanayoshamiri, na matukio yanayofanyika kila usiku."

Atacama

Kuhusiana na jangwa la Atacama , muongozo huo unatoa hakikisho kwamba kuna mandhari ya kuvutia kuwahi kushuhudiwa katika sayari.

Likipatikana kaskazini mwa Chile, jangwa la Atacama lina ukubwa wa kilomita za mraba takriban 105,000 likiwa ndio jangwa kubwa zaidi duniani.

Jangwa hili ambalo liko mbali na uchafuzi wa mazingira wa maeneo ya miji mikubwa ni eneo bora la kuvinjari.

Puerto Rico pia inapatikana katika orodha hii kutokana na uzuri wake wa kipindi cha ukoloni kilichopita na ule wa asili.

Puerto Rico tiene una combinación de historia colonial con bellezas naturales.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Puerto Rico ina mchanganyiko wa uzuri wa historia yake ya enzi ya ukoloni na uzuri wa asilia

Hii hapa ni orodha nzima kulingana na muongozo wa jarida la Lonely Planet:

1.Nchi

•Kisiwa cha Cook

Islas Cook

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kisiwa cha Cook

•Norway

Mauricio

•Belize

•Slovenia

Eslovenia

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Eslovenia

•Eel

•Oman

•Nepal

•Malawi

•Misri

Egipto

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Misri

2. Cities

•Auckland, New Zealand

Auckland, Nueva Zelanda

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Auckland, New Zealand

•Taipei, Taiwan

•Freiburg, Ujerumani

•Atlanta, Marekani

•Lagos, Nigeria

•Nicosia, Cyprus

•Dublin, Ireland

•Merida, Mexico

PICHA: Hidalgo Park, Merida, Mexico.

Parque Hidalgo, Mérida, México.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Parque Hidalgo, Merrida, Mexico.

•Florence, Italia

•Gyeongju, Korea Kusini

3. Kanda

•Westfjords, Iceland

PICHA: Westfjords, Iceland

Westfjords, Islandia

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Westfjords, Iceland

•West Virginia, Marekani

Xishuangbanna, China

•The Kent coast, Uingereza

•Puerto Rico, Marekani

•Shikoku, Japan

•Jangwa la Atacama, Chile

Desierto de Atacama, Chile

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jangwa la Atacama, Chile

•Scenic Rim, Australia

•Kisiwa cha Vancouver, Canada

•Burgundy, Ufaransa

Burgundy, France

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Burgundy, Ufaransa

PICHA: Burgundy, Ufaransa