Hii ni miji mitano salama zaidi kuishi duniani baada ya janga la Corona

Chanzo cha picha, Getty Images
Miji ama Majiji kote ulimwenguni yalilazimika kufikiria upya kuhusu masuala ya usalama wakati yakikabiliana na janga laCovid-19 pandemic - na haya ni yale yanayofanya vizuri.
Hakuna jambo lolote wakati wa sasa linaloweza kubadilisha maisha ya jiji kama ilivyo kwa janga la Covid.
Kutoka kufungwa kwa maofisi katikati ya mji , kulazimishwa kuvaaa barakoa mpaka masharti kwenye migahawa, tahadhari za janga la corona zimebadilisha mazingira ya maaiji kote ulimwenguni, inaweza kuwa hivi kwa muda mrefulabda kwa muda mrefu.labda kwa muda mrefu.
Kwa kweli, ni janga la kwanza la kiwango chake kutokea kwa watu waishio mijini. Wakati homa ya Uhispania ilitikisa mwanzoni mwa miaka ya 1900, kulikuwa na ni asilimia 14% tu watu wachache waliokuwa wanashi mijini, lakini leo idadi hiyo imeongezeka hadi asilimia 57%, kwa mujibu wa Umoja wa mataifa
Kwa sababu hiyo, miji mingi imelazimika kuwa macho zaidi katika suala la ulinzi wa afya na usalama kwa jumla ili kulinda zaidi watu wao. Ili kufafanua ni mabadiliko yapi yamesababisha usalama kuwa juu, Economist Intelligence Unit hivi karibuni kilitoa Fahirisi ya majiji Salama kwa mwaka 2021, ikiorodhesha majiji 60 kwa kutumia vigezo ama viashiria 76 vya usalama katika miundombinu, maisha ya kidijitali, usalama binafsi, masuala ya mazingira na afya - hasa kwenye utayari wa kukabiliana na janga na vifo vitokanavyo na Covid-19 vikijumuishwa na vya mwaka huu.
Majiji yaliyokuwa nafasi ya juu kama Copenhagen, Toronto, Singapore, Sydney na Tokyo - yote yalikuwa na sababu zinazoonyesha jinsi usalama wa jumla unavyohusiana na mshikamano wa kijamii, ushirikishwaji wa jamii nzima na imani ya jamii. Tumezungumza na baadhi ya wakaazi wa miji hii kuona jinsi mabadiliko yaliyosababishwa na janga la Corona yamefanya miji yao kuwa salama zaidi, shirikishi na jasiri; na kile wasafiri au wageni wanahitaji kujua ili kuwa salama watakapofanikiwa kuyatembelea
Copenhagen

Chanzo cha picha, Getty Images
Copenhagen, mji mkuu wa Denmark, unaongoza kutokana na nguzo mpya ama misingi mipya ya usalama wa mazingira inayoamini, ambayo hupima muendelezou (ikiwemo masuala ya nishati mbadala), ubora wa hali ya hewa, usimamizi wa mifumo ya taka na misitu iliyopo mijini. Haya yameleta athari chanya kwa namna miji ilivyo na wakaazi wake waliweza kukabiliana vyema na masharti ya janga, ambayo yaliondolewa kabisa mnamo Septemba 2021.
"Mbuga na maeneo ya kijani kibichi pamoja na njia za maji zilikuwa maarufu sana wakati wa janga hilo. Wakazi wa jiji hili walikuwa wakitembea huku na huko wakinunua vyakula vya kubeba na kufurahia mandhari ya maeneo mengi ya jiji hilo," alisema mkazi Asbjørn Overgaard, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Copenhagen Capacity. Jiji hili pia linaendelea kutoa "miongozo ya Corona" kusaidia watu, pamoja na alama mbalimbali zilizowekwa wazi ili kusaidia watu ama vikundi vya watu wanaotembea nje.
Mioyo ya jamii au watu wa Denmark unaweza kuitafsiri kwa neno moja kwa lugha ya nchi hiyo kidenish 'samfundssind' pia inawezesha raia wa nchi hiyo kufanya kazi pamoja na kuaminiana - ikiwemo maafisa wa serikali - hilo limesaidia kuwa na mazingira salama ya kuishi. Kingine kilichogundulika nchini humo ni kwamba kuna uhusiano mkubwa kati ya udhibiti wa rushwa na usalama wa miji , kwa hivyo haishangazi kwamba Denmark kama moja ya nchi zenye kiwango kidogo chaa rushwa duniani, kimewawezesha raia wake kuzamini taasisi za cnhi hiyoi na kuaminiana wao kwa wato wakati wote wa janga hilo.
Copenhagen pia ilitekeleza mpango mkubwa wa upimaji wa Covid kwa umma, ambao ni bure kwa kila mtu, wakiwemo watalii. Takwimu zilizokusanywa zilisaidia ufuatiliaji wa kina wa milipuko huo; na kwa kuongezea, jiji litatekeleza upimaji wa maji taka ili kujiinda mapema na milipuko yoyote.
Toronto

Chanzo cha picha, Getty Images
Huu ni mji mkubwa Canada kwa usalama unakaribiana kabisa na Copenhagen hasa baada ya janga la corona, ukifanya vizuri katika maeneo ya usalamwa miundo mbinu na mazingira. Wakazi wa Toronto wanapongeza utamaduni wa kushirkishwa ambao unathamini mawasiliano kwa jamiii , hasa linapokuja suala la uelewa wa watuy kuhusu chanjo.
Farida Talaat anaonyesha jinsi mji huo ulivyoanzisha mipango kadhaa ya chanjo ya jamii kusaidia kuufanya mji kuwa salama. Kwa mfano, Mpango wa Chanjo ya Sprint ya nyumba kwa nyumba ilisaidia wakazi wa mji huo ambao hawakuweza kutoka majumbani kupata dozi za awali. Kikosi Kazi cha wataalam kiliundwa mapema katika juhudi za chanjo ili kuhakikisha zoezi la chanjo linaenda sawa.
Wenyeji pia wanahisi salama kwa sababu ya historia ndefu ya jiji la tamaduni nyingi. "Toronto, nimegundua kwamba una kuingiliana na makabila na utamaduni tofauti," anasema Filipe Vernaza, ambaye ameishi katika jiji hilo tangu 1998. " Kuna kundi la watu ambalo kuna uwezekano wa kuwa limetokana na watu kutoka makabila tofauti, mwelekeo wa kijinsia na dini tofauti. Toronto ni jiji huru ambapo unaweza kujihisi salama kwa vile ulivyo."
Singapore

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa upande wa usalama wa kidijitali, afya na miundo mbinu limekuwa la pili. Singapore kama nchi ilitumia nguvu hizo kusonga haraka wakati wa siku za mwanzo za janga hilo, ikifanya ufuatiliaji wa kidijitali na mawasiliano kwa haraka. Nchi pia inajivunia kuwa na kiwango cha juu zaidi cha chanjo ulimwenguni (kwa sasa ni 80%), lakini bado inahitaji ufuatiliaji mkali na ufuatiliaji wa mawasiliano ya watu wa karibu wa waathirika ili kukabiliana na virusi vipya.
"Kabla watu hawajaingia kwneye majengo wakaazi wote wanatakiwa kuchunguzwa kwa kutumia token za TraceTogether ama program ya simu "alisema mkazi wa Singapore Sam Lee." Hii inasaidia [mamlaka] kufuatilia watu ambao wangeweza kuchanganyika au kushirikiana na walioambukizwa haraka ili agizo la karantini linaweza kutekelezeka ili kuzuia maambukizi."
Kwa mgeni kabla ya kuingiua nchini humo, atapaswa kuweka TraceTogether token kwenye simu yake ama kuazima simu ambayo ina program ya aina hiyo kwa ajili ya kurahisisha ufuatiliaji.
Kufanyia kazi nyumbani, imekuwa njia inayotumika sana ulimwenguni kote kupunguza msongamano, kitu ambacho Lee amekiona ni kwmaba njia hii inapunguza msongamano kwenye usafiri wa umma. which Lee notes has led to less crowded public transportation. Kumekuwa na idadi ndogo kwenye vivutio vya utalii na maduka makubwa na "mabalozi maalumu wanaohamasisha kukaa kwa umbali'' wakifuatilia misongamano kuhakikisha jamii inaheshimu masharti ya afya, kwa mtu anayekiuka hutozwa faini. Umma pia unaweza kufuatilia maduka makubwa, ofisi kama posta, na maduka madogo madogo kwa kutumia mpango mpya waliouzindua unaoitwa Space Out tool.
Sydney

Chanzo cha picha, Getty Images
Hili ni jiji kubwa nchini Australia, likishika nafasi ya tano kwa miji salama hasa wakati huu baada ya janga kubw ala corona, liko pia kwenye orodha ya miji 10 ya juu kwa usalama wa afya. Australia ilikuwa moja ya nchi za kwanza kufunga kabisa mipaka yake wakati wa janga hilo na imekuwa ikisimamia sharti la kusalia ndani kasi ya maambukizi ikiongezeka. Kiwango cha kifo cha kila mtu nchini Australia kinaendelea kuwa moja ya viwango vya chini zaidi ulimwenguni. Wakati utoaji wa Chanjo ukifikia asilimia 70% huko New South Wales, masharti mengi yanatarajiw akuondolewa na mipaka ya kimataifa inatarajiwa kufunguliwa mwezi Novemba.
Pamoja na kuhisi kwmaba wanalindwa na janga hilo, wakaazi wa mji huu wanahisi pia wako salama wakiwa katika mitaa ya Sydney. "Kwa kweli sijawahi kujiona niko salama nchini kama vile ninavyoishi Sydney," anasema Chloe Scorgie, mwanzilishi wa wavuti ya kusafiri ya Australia Pasipoti Down Under, ambaye alihamia Sydney kwa mara ya kwanza mnamo 2018. "Nilizunguka Sydney nikiwa msafiri wa kike peke yangu na kamwe sikuhisi kama nilikuwa katika hatari yoyote. "
Jiji hili ni la kwanza kwa usalama wa kidijitali, ambaop unajumuisha sera ya faragha ya jiji hio, ulinzi wa makosa ya mtandaoni na vitisho pamoja na mpango mzuri wa jiji ambao unaweka sehemu za kuwekea uchafu, taa za barabarani, mpango mzuri wa usafiri na uwepo wakamera za CCTV.
Tokyo

Chanzo cha picha, Getty Images
Mji mkuu wa Japan uko katika nafasi ya tano katika miji yenye usalama mzuri kiafya, ambayo huangalia masuala kama huduma ya afya kwa wote, utayari wa janga, muda wa kuishi, afya ya akili na vifo vitokanavyo na Covid-19.
Ingawa visa vya corona viliongezeka wakati wa michezo ya Olimpiki, viwango vimeshuka sana kwani zoezi la utoaji wa chanjo limefikia karibu 60% ya idadi ya watu. Kutokana na habari hiyo njema, Japani ilitangaza kumalizika kwa hali ya dharura iliypowekwa na kuondolewa taratibu kwa masharti ya janga mpaka kufikia mwishoni mwa Septemba 2021. Nchi hiyo inapanga kuhamasisha matumizi ya vyeti vya chanjo chanjo ili kukubaliwa kupata matibabu pamoja na kwenye mtukio makubwa, na hata kuhamasisha wafanyabiashara kutoa punguzo au kuponi kwa wenye vyeti hivyo.
Tokyo ilikuwa ya tano kwenye tano bora kwa usalama wa miundombinu yake, ambayo ni pamoja na usalama kwa usafirishaji, usalama wa watembea kwa miguu na mfumo mzima wa usafirishaji. Kama jiji linalotembea lililounganishwa na reli, jiji la Tokyo lilijengwa ili kuhamasisha watu kutembea na ushiriki wa jamii - ambapo imesaidia raia wengi kushuiriki kwenye masuala ya usalama kupitia njia ya ulinzi wa uhalifu kwa jamii ama jirani na kuchocheza ile dhana yua uwajibikaji wa pamoja kwenye ulinzi wa uhalifu.saa, na hali ya pamoja ya uwajibikaji wa uhalifu kuzuia.














