Waziri Mkuu wa Iraq al-Kadhimi anusurika kifo katika shambulio la ndege isiyo na rubani nyumbani kwake

Chanzo cha picha, Getty Images
Waziri Mkuu wa Iraq Mustafa al-Kadhimiamesema kuwa hakujeruhiwakatika shambulio dhidi ya makazi yake mjini Baghdad- katika eneo lsalama la Green Zone.
Ndege iliyokuwa na vilipuzi iligonga nyumba na kuwajeruhi walinzi sita katika katika jaribio la mauaji dhidi ya Waziri Mkuu, maafisa walisema.
Bw. Kadhimi ametoa ''wito wa utuliivu na kutaka kila mmoja kujizuia kuchukua hatua yoyote".
Shambulio hilo lililotokea baada ya vurugu zilizotokea ufuatia matokeo ya uchaguzi wa hivi karibuni, limelaaniwa na Marekani na Iran.
Vyanzo vya usalama vinasema ndege tatu zisizo na rubani zilitumiwa katika shambulio hilo, lililotekelezwa kutoka kwa daraja la umma lililo karibu Mto Tigris, lakini zilidunguliwa.
Hakuna mtu aliyejitangaza kuhusika na shambulio hilo, lililofanywa katika eneo la mji lililo na majengo ya serikali na balozi za kigeni.

Chanzo cha picha, EPA


Chanzo cha picha, EPA

Pcha zilizochapishwa katika vyombo vya habari vya Iraq zinaonesha sehemu iliyoharibika ya makazi ya Waziri Mkuu pamoja na gari aina ya SUV iliyoegeshwa katika gereji.
Mabaki ya ndege hiyo isiyo na rubani iliyokua na vilipuziyamechukuliwa na maafisa wa usalama kwa ajili ya uchunguzi, afisa wa usalama ambaye jina lake halikutajwa aliambia shirika la habari la Reuter .
"Ni mapema kusema ni nani alitekeleza shambulio hilo," afisa alinukuliwa akisema. "Tunadurusu ripoti zetu za kijasusi na kusubiri matokeo ya awali ya uchunguzi ili kubaini waliohusika."
Ndege iya kibiashara isiyo na rubani ana ambayo ilikuwa na vilipuzi ilitumiwa na wanamgambo wa kundi la Islamic State wakati ilipokua inashikilia sehemu ya kaskazini mwa Iraq, hasa wakati wa vita vya Mosul mwaka 2017.
Bw al-Kadhimi, Mkuu wa zamani wa ujasusi, aliapishwa kuhudumu katika wadhifa wake wasasa mwezi Mei mwaka jana

Uchambuzi: Shambulio linaweza kuashiria kuongezeka kwa hatari
Iraq ilifanya uchaguzi chini ya mwezi mmoja uliopita, na sasa iko katika mchakato mrefu na mbaya wa kujaribu kuunda muungano unaotawala.
Idadi ya waliojitokeza kupiga kura ilikuwandogo sana - 41% tu - na ukosefu huo wa ushiriki unaonyesha kwamba Wairaq wengi hawaamini mabadiliko yoyote ya kweli yapo mbele.
Vyama vinavyounga mkono Irani vilifanya vibaya zaidi kuliko walivyotarajia, na kupoteza viti vyao vingi. Wafuasi wao wamekuwa wakipinga matokeo tangu wakati huo, wakifanya maandamano nje ya eneo salama la Green Zone mjini Baghdad na kutaka kura zihesabiwe upya.
Kiongozi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia Moqtada al-Sadr alidai kuwa ameshinda, huku chama chake kikipata viti vingi zaidi.
Anashinikiza kuwepo kwa serikali isiyo na kuingiliwa na mataifa ya kigeni - na muhimu zaidi hiyo inamaanisha kutoka Iran na Magharibi. Anataka kukomesha ushawishi wa Tehran katika masuala ya ndani ya Iraq.
Makosa haya ya kisiasa yanamaanisha kuwa mvutano ni mkubwa, na jaribio hili la maisha ya Waziri Mkuu al-Kadhimi linaweza kugeuka kuwa ongezeko la hatari lenye athari kubwa.

Shambulio hilo la ndege isiyo na rubani limekosolewa pakubwa:
- Kiongozi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia, Moqtada al-Sadr, ambaye chama chake kilikuwa mshindi mkubwa zaidi katika uchaguzi huo, alikitaja kuwa kitendo cha kigaidi dhidi ya uthabiti wa nchi hiyo ambacho kililenga "kuirejesha Iraq katika hali ya machafuko inayodhibitiwa na vikosi visivyo vya dola."
- Rais Barham Saleh alisema ni uhalifu wa kutisha dhidi ya Iraq, na kuongeza katika tweet: "Hatuwezi kukubali kwamba Iraq itaingizwa kwenye machafuko na mapinduzi dhidi ya mfumo wake wa kikatiba."
- Katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Kitaifa la Iran, Ali Shamkhani, alivishutumu "asasi za kigeni" zisizojulikana kwa "kuunda na kuunga mkono vikosi vya kigaidi na uvamizi" nchini Iraq ambavyo "havijaleta chochote isipokuwa ukosefu wa usalama, mifarakano na ukosefu wa utulivu".
- Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson alimweleza Bw Kadhimi kwa njia ya simu kwamba analaani vikali shambulio hilo.
- Rais wa Marekani Joe Biden alisema wahusika wa shambulio hilo lazima wawajibishwe na kulaani "kwa maneno makali wale wanaotumia ghasia kudhoofisha Iraq"
- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitoa wito kwa Wairaq "kukataa ghasia zote na majaribio yoyote ya kuyumbisha Iraq"













