Je Jua lina rangi gani?

Chanzo cha picha, Getty Images
Tangu tukiwa wadogo, tulikuwa tunataka kuchora namna anga ilivyo, hatukuwa tunasita kuchagua rangi ya kuchora jua: Mara nyingi rangi iliyotumika sana ni njano.
Kama tunataka kuipendezesha zaidi, tunaongeza miale ya rangi nyingine kama ya machungwa na nyekundu
Hata hivyo nyota za karibu na jua huwa zinawekwa zaidi rangi yoyote lakini sio njano, ya machungwa ama nyekundu.
Kwa maneno mengine, jua lina rangi za upinde wa mvua' rainbow. Hata hivyo kabla ya kuanza kufikiria kuchora jua lenye rangi zaidi ya moja, lazima tufafanue kwamba haitakuwa sawa ukisema jua lina rangi nyingi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa sababu rangi hizo zinazoonekana zikitoa mwanga, unachopata kutoka kwenye jua ni rangi moja, rangi ambayo tunajua unaweza kujiuliza ni ipi hasa?
Tazama vizuri mawingi yanayoakisi mwanga wa jua. Sio ya njano sio yenye rangi rangi. Ni meupe, kwa sababu ndio mwanga unaoka kwenye jua.
Kwa nini tutaiona rangi ya njano?
Kila rangi katika wigo wa jua ina urefu unaotofautiana. Rangi nyekundu huonekana kwa mawimbi marefu zaidi. Lakini rangi zingine kama ya machungwa, njano, blue, kijani na indigo huwa na mawimbi mafupi.
Kwa hivyo ukiangalia jua kutokea angani, picha zinazotufikia katika mboni za macho yetu - sehemu ya akili inawajibika kutafsiri taarifa za picha ilizoifikia - wakati huo huo matokeo ya kile tunachokiona ni mwanga mweupe.
Na rangi hiyo ndiyo inatajwa kama 'rangi halisi' ya jua.

Chanzo cha picha, Getty Images
Jua ni la kijani?
Profesa wa Chuo Kikuu cha Republic nchini Uruguay, Gonzalo Tancredi, anaifafanulia BBC kwanini mitandao mingi inadai kwamba jua ni la kijani.
"Kama utachora mchoro wa miale ya jua kileleni mwa mchoro huo utaona ukanda wa kijani," anasema.
Kwa maneno mengine, ingawa macho ya binadamu hayawezi kutofautisha tofauti ya rangi ya miale ya jua, kama mtu ataiangalia kwa kutumia vyombo maalumu vinavyoonyesha utofauti huu, anaweza kuona miale ya kijani inajitokeza zaidi( ingawa kwa utofauti mdogo).
Hili linasaidia kuelezea kwa nini tunaona jua la njano ama kijani ukiangalia kutoka kwenye uso wa dunia. Kama utaondoa sehemu ya rangi ya blue na mawimbi yanye urefu mfupi, kitakachoojitokeza ni rangi ya njano ama itabadilika kuwa ya njano, " anasema.

Chanzo cha picha, NASA/SDO/Goddard Space Flight Center
Machweo mekundu?
Tumeona kwa nini tunaliona jua ni la njano, ingawa linatoa mwanga mweupe. Na wengi tunafahamu kuhusu mawio na macheo. Lakini kwanini jua linaonekana kujibadilisha rangi, linapochomoza asubuhi (mawio) na linapozama jioni(machweo)?
Yoyote aliyewahi kushuhudia kuchomoza na kuzama kwa jua ataona rangi nzuri za kuvutia zinazotoka katika jua, ambazo zinatengeneza anga lenye rangi ya machungwa na nyekundu.
Kwa mara nyingine unachokiona unadanganywa na macho yako kunakotokana na muingiliano kati ya miale ya jua na anga la dunia.
Kinachotokea ni kwamba wakati wa kuchomoza kwa jua, jua linakua karibu na upeo wa macho yako, na mwanga wake unakuwa umepitia anga na matabaka mengi kabla ya wewe kuuona, kwa hivyo kuzuiwa kwa rangi kama hudhurungi ni jambo kubwa. Kwa maana nyingine kabla ya wewe kuona unachokiona, mwanga mwingi unakuwa umekinzwa na vizingiti kadhaa kutoka lilipo jua mpaka kwenye uso wa dunia.
Kitendo hichi cha rangi tofauti kuonekana kwenye anga kulingana na lilipo jua kinaitwa kitaalam 'Rayleigh scattering'.
Na athari yake kubwa ya kushangaza huonekana alfajiri jua linapochomoza na jioni jua linapozama, wakati huo, rangi zaidi huonekana na mawimbi marefu ya rangi hasa nyekundu na rangi ya machungwa.

Chanzo cha picha, EyeWire, Inc.
Pengine ulichokisoma leo, kimekufundisha kitu. Lakini ni vyema tukakukumbusha ya kwamba usiliangalie jua moja kwa moja kwa kutumia macho yako, hata pia kwa kutumia vifaa kama kiona mbali, kwa sababu huenda ikaathiri uwezo wako wa kuona na huenda pia ukasababisha upofu kabisa.












