Jeff Bezos: Fahamu mpaka wa angani ambao ulivukwa na mwanzilishi wa Amazon

Chanzo cha picha, Reuters
Hatua kubwa imepigwa katika harakati za biashara kwenda anga za mbali siku ya Jumanne baada ya bilionea Jeff Bezos kupaa na kuvuka mpaka wa angani unaojulikana kama mstari wa Kármán kwa kutumia roketi yake mwenyewe.
Chombo hicho kipya kinachoitwa Shepard, kimeundwa na kampuni ya Blue Origin, kwa lengo la kuwahudumia watalii wa anga za mbali.
Chombo hicho kilianza safari katika kituo cha kibinafsi karibu na Van Horn, Texas, na mara baada ya kutoka katika mduara wa dunia ilifika umbali wa kilo mita 106.
Chombi hicho kilisafiri mara tatu ya kasi ya sauti ikifika umbali wa kilo mita 100 juu ya duna .
PUBLICIDAD
"Chombo chetu kimefika umbali wa juu zaidi wa ana za mbali. Wasafiri wetu wanajionea picha za kuvutia za dunia wakiwa juu ya mstari wa Kármán," Blue Origin iliandika katika ujumbe wa Twittter siku ya Jumanne.
Lakini Jumanne hii siku pekee kampuni ya angaa za mbali imefanikiwa kupeleka chombo hadi mpaka huu.
Zaidi ya wiki moja iliyopita bilionea wa Uingereza Richard Branson, mmiliki wa shirika la Virgin Group, alikuwa karibu kuingia milango ya anga za mbali kwa kutumia roketi yake inayofahamika kama Unity, ambayo ilimfikisha umbali wa kilomita 85 ''pekee, Blue Origin iliandika katika ujumbe wake wa Twitter hatua ambayo ilionekana kukosoa kampuni hasmu, kulingana na mwandishi wa BBC wa Sayansi Jonathan Amos.
"Shepard mpya iliondwa kupaa juu ya mstari Kármán (...)," iliandika Blue Origin, siku chache kabla ya safari ya ya bilionea wa Uingereza kwa kutumia chombo cha kinachojulikana kama Unity.
Mpaka huu ulichorwa vipi na ni nani aliamua ndio ukomo wa mpaka wa anga za mbali?
Chanzo
Shirikisho la Anga la Kimataifa (FAI), chombo kinachosimamia na kusajili rekodi za angani, kinatambua laini ya Kármán kama mpaka kati ya anga za mbali na anga ya Dunia.

Chanzo cha picha, Blue Origin
Mpaka huo ulipewa jina la kwa heshima ya mhandisi mzaliwa wa Hungury na Marekani Theodore von Kármán, ambaye alikuwa wa kwanza kujaribu kuweka alama ya mpaka wa angani katika miaka ya1950.
"Von Kármán calculated that above an altitude of approximately 100 kilometers, a vehicle would have to fly faster than orbital speed (kasi inayohitajika ardhini ili kukaa angani)," alieleza mhandisi Dennis Jenkins katika taarifa iliyochapishwa katika wavuti wa NASA mwaka 2005.
"Ingawa urefu sahihi ulitofautiana kulingana na vigeuzi kadhaa, von Kármán alipendekeza kilometa 100 zi ya aganiteuliwe kwa madhumuni ya uhandisi," iliongeza nakala hiyo.
Wakili wa Marekani Andrew G. Haley, aliyekuwa wa kwanza kuhudumu kama "mwanasheria wa angani," alibuni neno "Kármán line" mwaka wa 1957, maelezo yanapatikana katika taarifa iliyochapishwa katika Jarida la Sheria za Angani mwaka 2017, ijapokuwa Haley hakusema mpaka huo ulikuwa wa umbali gani.
Miaka michache baadae, FAI ilianza kutumia mpaka wa Kármán line , wenye urefu wa kilo mita 100 juu ya usawa wa bahari, na kwa sasa ndio sehemu ya mwisho inayotambuliwa na taasisi hii na mashirika mengine kote duniani.
"Kinadharia, mpaka huo wa kilomita 100 ukivukwa, hewa inakuwa hafifu sana kiasi cha kuwezesha ndege ya kawaida kuendelea na safari.

Chanzo cha picha, Reuters
Katika urefu huu ndege ya kawaida... huenda ikakabiliwa na hatari ya kuanguka duniani, "inaelezea Mamlaka ya kitaifa ya kusimamia Bahari na Anga nchini Marekani (NOAA, kwa ufupi).
"Kimantiki mstari wa Kármán ndipo sheria za asili zinazosimamia uwezo wa chombo cha kuruka hubadilika,''lilieleza jarida la unajimu katika nakala mnamo Machi iliyopita.
Mipaka mingine ya angani
Lakini wanasayansi hawajakubaliana anga za mbali huanzia wapi, kwa sababu Anga ya dunia inazidi kupungua kwa kilomita nyingi zaidi ya mstari wa Kármán.
"Asilimia 99.99997 ya anga ya dunia iko chini ya mstari wa Kármán," kwa mujibu wa NASA, shirika la Marekani la anga za mbali.
Lakini mwaka utafiti wa mwaka 2019 utafiti unaonyesha kwamba safu ya nje ya anga - iitwayo geocorona - inaweza kufikia hata zaidi ya mzunguko wa Mwezi, shirika hilo linasema.
Unaweza pia kusoma:
Nchi zingine huweka kikomo cha mpaka wa angani katika urefu zaidi ya ule wa mstari wa Kármán.
NASA na Jeshi la Merika, kwa mfano, huiweka kwa urefu wa kilomita 80, mahali ambapo ulimwengu unaishia.
Tafiti zingine zilizochapishwa hivi karibuni zinaweka kikomo mpaka huo juu kuliko laini ya Kármán.













