Roketi ya kampuni ya SpaceX yatua baada ya kupaa lakini ikalipuka

Maelezo ya video, Tazama safari yote ya SN10 kuanzia kikipaa hadi kutua

Kampuni inayotengeneza vyombo vya anga za mbali SpaceX kimefanikiwa kukiwezesha moja ya vyombo vyake Starship prototypes katika mwisho wa safari yake ya anga za juu kwa ajili ya majaribio

Chombo hicho chenye nambari ya utambulisha 10 (SN10) kilitua katika eneo la Boca Chica, Texas - kinyume na vyombo vya awali vilivyopewa nambari ya utambulisho SN8 na SN9, ambavyo vililipuka ardhini.

Lakini huo haukua mwisho wa hadithi yake. Chombo hicho kinachotazamiwa kuwagari lijalo la anga za mbali la kizazi kijacho kilionekana kuelemea mataili yake ya ziada.

Hii ilisababisha moto kuwaka katika eneo lake la chini na dakika nane baadae SN10 kikajilipua chenyewe katika eneo la kutua.

Hatahivyo, SpaceX itatiwa moyo sana na jaribio hilo na ukweli kwamba chombo hicho kimeweza kufanikiwa kusafiri kufanikiwa kufanya safari za mizunguko iliyotarajiwa na kuweza kujaribu kutua vyema. Hatua hizi za mafanikio zitaipatia imani kampuni ya SpaceX inaposonga mbele na dhana nyingine za uvumbuzi wa safari za anga za mbali.

SN10 flight

Chanzo cha picha, SPACEX

Maelezo ya picha, Chombo cha SN10 kilikwenda mwendo wa pole kilipokuwa kikitua ardhini

SpaceX imebuni chombo hiki cha Starships zinachukua nafasi roketi za Falcon ambazo zinatumiwa kwa sasa.

Vyombo hivi vinavyofahamika kama magari ya anga za mbali hufanya safari za mara kwa mara vikiwa na wasafiri au bila kuwa na wasafiri ndani yake-kwa ajili ya Shirika la safari za anga za mbali la Marekani (Nasa), Jeshi la Marekani, na safari nyinginezo za kibiashara.

Lakini Mkurugenzi Mkuu Elon Musk anasema chombo hiki kipya chenye urefu wa mita 50 kwenda juu kitafanya yote, makubwa na mazuri - kuzunguka setilaiti na kuwabeba wasafiri, katika maeneo mbali mbali ya dunia na kwenda katika safari za mbali ya dunia kama vile mwezini na katika sayari ya Mars.

Aliahidi kumsafirisha hadi mwezini Bilionea Mjapan mwanamitindo anayeendesha biashara yake mtandaoni Yusaku Maezawa mwaka 2023.

Bw Maezawa atasafiri katika Starship pamoja na watu wengine wanane, na alifungua ukurasa wa maombi kwa yeyote ambaye anataka kujiunga nae katika safari hiyo ya utalii iliyoitwa ''dearMoon''

Unaweza pia kusoma:

SN10 flight

Chanzo cha picha, SPACEX

Maelezo ya picha, Chombo cha SN10 kilikwenda mwendo wa pole kilipokuwa kikitua ardhini

Jumatano, jaribio la safari ya anga za mbali liliendelea kawaida kama ilivyofanyika awali kwa safari nyingine zilizotangulia.

Chombo hicho ambacho hakikuwa na wahudumu wala abiria SN10 kiliondoka katika eneo la manzo wa safari la Boca Chica R&D , na kupaa wima, huku kikiungua na kutoa moshi.

Hii ni hali ya kawaida ambapo nishati zake huzima baada ya muda kinapofikia umbali wa kilomita takriban 10 au maili 6.2 , ambapo chombo husafiri tambalale kwa ajili ya kurusha vitu ardhini iwapo kitahitajika kufanya hivyo.

Chombo hiki ambacho hudhibitiwa angani na kifaa kingine kipana kilichopo mwanzoni au mwishoni mwake, kinanuwia kuonyesha ni vipi vyombo vya aina hii ya Starships vitakavyoingia katika hali ya hewa ya dunia kutoka kwenye uzio(orbit).

SN10 flight

Chanzo cha picha, SPACEX

Maelezo ya picha, Chombo hiki huegemea kwenye chuma chake cha kutua. Muda mfupi baadae kikajilipua

Chombo hiki kilitakiwa kurejea kwanza kwenye mkia wake kabla ya kutua ardhini.

SN8 na SN9 havikuweza kufanikiwa . Vyote vilishindwa kufuata muongozo sahihi na kupunguza kasi ya mwendo wake

SN10, hatahivyo, kilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuweza kupunguza kasi yake taratibu na kutua kwenye eneo kilipopaswa kutua. Kilichochangia zaidi mafanikio hayo bila shaka ilikuwa ni ku kuwasha kwa taa tatu za eneo la kutua kabla ya kutua kwa chombo, kuhakikisha walau injini mbili zipo ili kutoa fursa ya chombo kushika breki na kusimama.

"Furaha ya mara ya tatu ," alisema John Insprucker, mtangazaji wa mtandao wa kampuni ya SpaceX.

Lakini mambo yote hayakuwa sawa chombo cha SN10 kilikuwa kimeinama. Miguu yake ilionekana kuvunjika. Na wakati wazimamoto walipokuwa wakijaribu kuzima moto kwenye eneo la chini la chombo, ghafla kililipuka.