Chombo cha anga za juu cha Perseverance rover cha Nasa chatua sayari ya Mihiri.

Maelezo ya video, "Imethibitshwa kwamba chombo Perseverance rover kimetua sayari ya mihiri": Furaha waliokuwa nayo timu inayofuatilia chombo hicho.
Muda wa kusoma: Dakika 3

Kuna roboti mpya katika sayari ya Mihiri yaani Mars.

Shirika la Anga za Juu la Marekani (Nasa) limefanikiwa kuwezesha kutua salama kwa chombo chake cha Perseverance rover katika bonde kubwa lenye kina yaani kreta karibu na ikweta ya sayari hiyo inayojulikana na Jezero.

"Taarifa njema ni kwamba chombo hicho cha anga za mbali kiko katika hali nzuri," amesema Matt Wallace, naibu meneja wa mpango huo.

Wahandisi wa Nasa waliokuwa wanadhibiti chombo hicho huko California walijawa na furaha isiyokifani walipothibitisha kwamba chombo cha Perseverance rover kimetua salama salmini katika sayari ya mihiri.

Chombo hicho chenye magurudumu 6 sasa kitakuwa kwenye sayari hiyo kwa takriban miaka miwili katika mabonde ya eneo hilo, kikitafuta ushahidi unaonesha shughuli za maisha ya awali.

Ikweta ya Jezero inadhaniwa kwamba imekuwa na ziwa kubwa kwa miaka bilioni kadhaa iliyopita.

Na mahali ambapo kumekuwa na maji, kuna uwezekano mkubwa kulikuwa na maisha yalioendelea eneo hilo.

Jezero crater

Chanzo cha picha, NASA

Maelezo ya picha, Picha inayoonesha kivuli cha roboti hiyo

Ishara zilitaarifu wadhibiti kwamba chombo Perseverance kimetua salama saa 20:55 za GMT.

Ingekuwa siku za nyuma, bila shaka wangekuwa wakisherehekea kwa kukumbatiana, kusalimiana na kadhalika lakini kwasababu ya masharti yaliowekwa kukabiliana na virusi vya corona, walionekana kufurahia tukio hilo wakiwa mbalimbali.

Furaha iliongezeka baada ya kuonekana picha mbili za kwanza zimechukuliwa.

Kulikuwa na vumbi lililoghubika mwanga lakini ungeweza kuona sehemu bapa kwa mbele na nyuma ya chombo cha rover.

Utafiti wa awali unaonesha kuwa chombo hicho kilitua takriban kilomita mbili kusini mashariki mwa eneo la delta katika ikweta ya Jezero ambako chombo Perseverance kinapanga kuchunguza.

"Tuko katika eneo zuri bapa. Chombo kimeinama kidogo tu," amesema Allen Chen, aliyeongoza timu iliyoshughulikia kutua kwa chombo hicho. "Kwahiyo, kimetua eneo zuri kwa uchunguzi na salama."

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Perseverance

Chanzo cha picha, NASA/JPL-Caltech

Maelezo ya picha, Roboti iliyotumwa ina uzito wa tani moja: vifaa saba, kamera kadhaa, vipaza sauti na mashine kubwa ya kekee

Kutua kwa chombo hicho katika sayari ya Mihiri sio rahisi na hata kama Nasa imekuwa mabingwa katika hilo, kila mmoja katika timu alikuwa amezungumzia juu ya kuchukua tahadhari wakati chombo kinatua.

Hiki ni chombo cha pili chenye uzito wa tani moja kufika sayari ya mihiri kuwezeshwa na Shirika la Anga za Juu la Marekani (Nasa).

Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2012 ambapo chombo kilitua katika bonde jingine.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Wadhibiti watatumia siku zinazokuja kutathmini chombo cha rover ikiwa pengine kuna mfumo wake wowote ulioharibika kwasababu ya kutua kwa nguvu kali.

Sasa chombo Perseverance kikiwa na mfumo wake wa kamera, ni lazima kiinuliwe. Programu iliyowezesha chombo hicho kufika katika sayari ya mihiri sasa itabadilishwa na mfumo mwingine utawekwa ambao utawezesha roboti kujiendesha kutoka eneo moja hadi jingine katika eneo hilo.

Pia cha msingi zaidi, chombo Perseverance kinatarajiwa kupiga picha nyingi zaidi wiki ijayo hivi ili wahandisi na wanasayansi waweze kuona uhalisia wa maeneo yaliyo karibu.

Landing maps

Chanzo cha picha, NASA

Maelezo ya picha, Picha ya juu: chombo rover kilitua takriban kilomita 2 kutoka eneo lililolengwa la delta la Jezero. Picha ya chini: Chombo kimetua salama

Pia moja ya lengo ni kufanya jaribio la helikopta.

Chombo Perseverance kimebeba helikopta ndogo ambayo itajaribu kufanya safari ya kwanza ya ndege katika dunia nyingine.

Ni baada tu ya jaribio hilo ambapo roboti itaanza kuangazia mambo mengine yaliyopangwa. Itaelekea katika lile eneo la delta lenye maji ambalo limegunduliwa na satelaiti.

Delta hutengenezwa kwa mito wakati mikondo yake inajiondoa katika mkondo mkubwa wa maji na kuacha uchafu wake.

Wanasanyansi wanaimani kuwa hayo yote yanaelezea historia ya biolojia ya zamani.

Chombo hicho kitachunguza eneo la chini la delta na kisha kielekee katika ukingo wa kreta. Katika eneo la ukingo satelaiti imegundua miamba ya kaboni, ambayo duniani huwa ni chanzo kizuri cha kufuatilia shughuli za kibaolojia.

Chombo Perseverance kina vifaa vya kutosha kuchunguza yote hayo kwa kina hadi kiwango cha kutumia darubini.

Picture of Mars

Chanzo cha picha, NASA

Maelezo ya picha, Picha ya pili iliyotumwa kutoka kreta ya Jezero
Presentational grey line