Chombo kilichotumwa mwezini na China kwa lengo la kukusanya mawe na mchanga chawasili

Kinalenga kukusanya mawe na mchanga kilo mbili ili kuleta duniani

Chanzo cha picha, CNSA

Maelezo ya picha, Kinalenga kukusanya mawe na mchanga kilo mbili ili kuleta duniani
Muda wa kusoma: Dakika 1

Taifa la China limefanikiwa kuwasilisha chombo chengine cha anga za mbali katika mwezi.

Chombo hicho kwa jina Change e-5 mission kiliwasili katika sakafu ya mwezi muda mfupi uliopita kwa lengo la kukusanya sampuli za mawe na vumbi ili kuleta duniani.

Mpango huo ulilenga eneo moja lenye volkano karibu na eneo kwa jina Oceanus Procellanum .

Chombo hicho kinatarajiwa kusalia huko kwa siku chache zijazo kikichunguza mazingira na kukusanya mawe hayo na vumbi lililopo.

Kina vifaa kadhaa ikiwemo kamera rada na kijiko na kifaa cha kuchimba .

lengo ni kukusanya takriban kilo 2 za mchanga na kutuma katika kifaa ambacho kinaweza kuwasilisha bidhaa hizo duniani.

Ni takriban miaka 44 tangu hatua kama hiyo kuchukuliwa .

Huo ulikuwa ujumbe wa Urusi ambao ulikusanya chini ya gramu 200 za mchanga.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Ikilinganishwa na uzinduzi wa chombo hicho duniani wiki moja iliopita kuwasili kwake katika mwezi hakukuangaziwa mubashara na runinga za China.

Muda tu baada ya chombo hicho kuwasili katika sakafu na kuthibitishwa ndiposa walipotangaza mafanikio hayo.

Picha zilizopigwa zilitolewa huku chombo kimoja kikionekana kivuli chake katika sakafu hiyo yenye vumbi jingi.

Walishangilia walipoona kwamba kimetua salama salmini

Chanzo cha picha, SHUTTERSTOCK