Chombo kilichobeba mawe kutoka anga la mbali chatua salama

Chanzo cha picha, JAXA / EPA
Chombo kilichobeba mawe kutoka kwa sayari ndogo yaani asteroidi kiko sawa, kulingana na wanasayansi.
Chombo kilichobeba mawe hayo kutoka kwa jiwe la kwenye anga ya mbali katika sayari ndogo yaano asteroid kwa jina Ryugu, kimeshuka vizuri karibu na eneo la Woomera kusini mwa Australia Jumamosi jioni saa za eneo hilo(GMT).
Timu ya wanasayansi wa Australia imebaini chombo kutoka anga za mbali juu ya ardhi yake huku parachuti iliyotumika katika safari hiyo ikitua juu ya mti.

Chanzo cha picha, JAXA / EPA
Sampuli hiyo ya mawe awali kabisa ilichukuliwa na chombo cha anga cha Japani cha Hayabusa-2.
Chombo cha Japani kilitumia zaidi ya mwaka mmoja kuchunguza sayari ndogo ya Ryugu kabla ya kurejea duniani.
Wakati kinawasili katika sayari yetu, Hayabusa-2 iliachilia chombo cha Ryugu kilichokuwa na mawe hayo adimu kutoka anga za mbali na injini yake ikaungua na kuelekea upande mwingine.
Hatahivyo, chombo cha Ryugu kilifanikiwa kuingia katika anga la dunia.

Chanzo cha picha, Jaxa / EPA

Chanzo cha picha, EPA
Mtandao wa Twitter wa maafisa wa chombo cha Japani cha Hayabusa-2 walisema chombo hicho na parachuti yake vimepatikana saa moja na dakika 47 usiku.
"Tumechukua chombo hicho chenye hazina muhimu," mkuu anayesimamia safari hiyo Dkt. Yuichi Tsuda alisema.
Aliongeza kuwa hakuna kilichoharibika.
Dkt. Hitoshi Kuninaka, mkuu wa Taasisi ya Anga za Mbali Japani alisema: "Tulianza kuunda chombo Hayabusa-2 mwaka 2011. Na sasa ndoto yetu imetimia."
Safari itakayofuata itajumuisha chombo kwa jina MMX, ambacho kitalenga kuleta sampuli kutoka mwezi mkubwa katika sayari ya Mihiri unaojulikana kama Phobos.

Chanzo cha picha, Jaxa
Chombo cha anga cha Hayabusa-2 ambacho kilipita dunia baada ya kuachilia chombo kilichokuwa kimebeba mawe hayo kutoka anga za mbali kitatumwa tena katika safari nyingine ambayo ni kwenye asteroidi ndogo zaidi kuliko ya Ryugu na kutarajiwa kufika huko mwaka 2031.












