Wanaanga wa SpaceX warejea: Chombo cha Dragon chatua duniani

Maelezo ya video, "Asanteni kwa kusafiri hadi anga la mbali" - Doug Hurley na Bob Behnken warejea duniani
Muda wa kusoma: Dakika 2

Wanaanga wawili wa Marekani wametua huku chombo cha kwanza kufadhiliwa na kampuni binafsi kikiwasili duniani kutoka Kituo cha Anga cha Kimataifa.

Chombo cha anga cha Dragon kinachomilikiwa na kampuni ya SpaceX kilichokuwa kimewabeba Doug Hurley na Bob Behnken kilifika duniani katika ghuba ya Mexico kusini tu mwa Pensacola ghuba ya pwani ya Florida.

Hii ni mara kwanza timu iliyokwenda anga za mbali kuwasili katika bahari ya Marekani tangu wakati wa chombo cha Apollo miaka 45 iliyopita.

Waliofika kwa maboti ya kibinafsi yaliokuwa karibu na chombo cha Dragon waliombwa kuondoka huku kukiwa na wasiwasi wa kemikali hatari kutoka kwenye chombo hicho.

Afisa wa utawala wa Nasa Jim Bridenstine amesema uwepo wa boti hizo "hakikuwa kile tunachotarajia".

"Cha kushangaza ni kwamba watu ambao hawakutarajiwa waliwasili katika eneo ambalo wawili hao walitua chenye kemikali ya nitrogen tetroxide, hilo sio jambo zuri," amesema.

Picha za boti hizo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Presentational white space

"Ni heshima na farahi kwetu," amesema Hurley wakati mwanaanga huyo anawasili nyumbani.

"Kwa niaba ya chombo cha SpaceX na timu ya Nasa, karibuni tena duniani. Asante kwa kusafiri hadi anga la mbali," Timu ya SpaceX imeandika.

Rais Donald Trump - aliyehudhuria hafla ya kuzinduliwa kwa chombo hicho miezi miwili iliyopita - alipongeza kurejea kwa ujumbe huo salama.

"Asanteni nyote!" aliandika kwenye mtandao wa Twitter. "Ni furaha sana kurejea kwa wanaanga wa NASA duniani baada ya safari ya miezi miwili iliyokuwa salama."

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Presentational white space
Presentational grey line

Kunusuru mabilioni ya serikali

Analysis box by Jonathan Amos, science correspondent
Maelezo ya picha, Uchambuzi na Jonathan Amos
Bob Behnken (L) and Doug Hurley (R)

Chanzo cha picha, NASA

Maelezo ya picha, Bob Behnken (kushoto) na Doug Hurley (kulia) walikwenda kituo cha anga za mbali mwisho wa Mei

Kumalizika salama kwa safari hiyo ni mwanzo wa enzi mpya kwa Shirika la Anga za mbali la Marekani.

Safari zote za kwenda zaidi ya duniani zitakuwa zinafadhiliwa na makampuni binafsi siku za usoni kama vile SpaceX.

Shirika la serikali limesema kupata watu wa nje kufadhili safari hizo kutanurusu mabilioni ya madola ya ambazo zitatumika katika mambo mengine kama kupeleka wanaanga kwenye mwezi, kama sehemu ya mpango wake na baadae kwenye sayari ya mihiri yaani Mars.

Kampuni ya utengenezaji ndege ya Boeing pia nayo inatengeneza chombo kipya lakini imelazimika kuchelewesha kukizindua baada ya kupata matatizo ya kiprogramu kwenye chombo chake cha Starliner.

Presentational grey line

Kuonekana kwa parachute nne kikielea juu ya maji katika ghuba ya Mexico ilikuwakithibitisho kwamba kimesafiri na kurejea salama.

Maelezo ya video, SpaceX ni nini na kwanini inashirikiana na Nasa?

Chombo cha Dragon kilirushwa kwenda anga la mbali mwishoni mwa Mei kupitia roketi ya Falcon 9 ambacho pia kimesimamiwa na kampuni ya SpaceX.

Sasa kitafanyiwa maboreshona na kurushwa tena kwenda anga la mbali mwaka ujao.

Bwana Bridenstine alipongeza kila mmoja aliyehusika kufanikisha safari ya Hurley na Behnken kwa juhudi zao.

"Hatutaki kununua chombo, kumiliki na kufanya nacho shughuli zetu kama iliyokuwa awali," amesema.

"Tunataka kuwa mteja kwa wateja wengi katika soko linaloendelea kukua kwenye mzunguko wa dunia. Lakini pia tunataka kuwa na kampuni nyingi zinazotoa huduma na kuwepo na ushindani dhidi yao kigharama, uvumbuzi na usalama na kutengeneza mzunguko wa maendeleo ya kiuchumi na uwezo."