Wanawake washinikaza unyanyasaji wa kijinsia mtandaoni kukomeshwa

Emma Watson, Thandiwe Newton and Julia Gillard

Zaidi ya wanawake 200 wa hadhi ya juu wametia saini barua ya wazi kutaka hatua zichukuliwe dhidi ya unyanyasaji.

Baraua hiyo - ilitiwa saini na na wanawake akiwemo waziri mkuu wa zamani wa Australia Julia Gillard, mchezaji wa zamani wa tennis wa Marekani Billie Jean King n amuigizaji wa filamu wa Uingereza Thandiwe Newton na Emma Watson - imechapishwa katika Baraza la Usawa la Kizazi cha UN.

Bi Gillard ameiambia BBC: "Kama Waziri Mkuu wa Australia, sawa na wanawake wengine wanaoshikilia nyadhifa za umma, Mara kwa mara napokea ujumbe ulio na ubaguzi wa kijinsia katika mitandao ya kijamii, zikiwemo katuni za kiponografia."

Aliongeza kuwa jumbe hizo zilimfanya "kuwa na hasira na kughadhabika kuwa wanawake bado wanakabiliwa na unyanyasaji wa aina hiyo".

Barua hiyo ilielekezwa kwa Maafisa wakuu watendaji wa Facebook, Google, TikTok na Twitter, kuwataka "wapatie kipaumbele usalama wa wanawake katika mitandao yao".

Kwa upande wao, wakuu hao wa mitandao ya kijamii walikariri kujitolea kwao katika uimarishaji wa mifumo ya kuripoti unyansaji wa kijinsia kwa kudhibiti kile kinachooneka na na watumiaji wa mitandao hiyo na wale wnaoweza kujumuika nao mitandaoni.

Hata hivo baadhi ya wanaharakati wameelezea hofu yao kwamba ahadi hizo kamazimekuwa zikitolewa na hakuna kinachobadilika.

"Kauli kama hizi kutoka kwa kampuni za kiteknolojia ni nafasi ya kuimarisha uhusiano mwema lakini uhalisia wake unasalia kuwa hadithi za abunuasi," anasema Lucina Di Meco, mwanzilishi mwenza wa #ShePersisted Global, ambayo inakabiliana na unyanyasaji dhidi ya wanawake mitandaoni.

Woman staring at phone in bed with logos of Facebook, TikTok, Twitter and Google popping out of the screen

Chanzo cha picha, Oscar Wong

Barua hiyo inasema: "Intaneti ni mji wa karne ya 21. Ni mahali ambapo mijadala inafanyika, jamii zinajengwa, bidhaa zinauzwa na sifa kutengezwa.

"Lakini kiwango cha unyanyasaji mitandaoni kwa wanawake wengi kinashiri, ulimwengu wa kidijitali sio salama. Halii hii ni tishio kwa upatikanaji wa usawa wa kijinsia."

Barua hiyo pia iliangazia utafiti wa mwaka 2020 uliofanywa na kitengo cha upelelzi cha intelijensia ya uchumi ukijumuisha wanawake zaidi ya 4,000, ambao uligundua kuwa asilimia 38 ya wanawake katika nchi 51 wamekumbana na unyanyasaji wa moja kwa mitandaoni.

Pia ilisisitiza kuwa unyanyasaji wa mitandaoni ni mbaya zaidi dhidi ya makundi yaliyotengwa ya Waafrika, Wahindi, Walatino na wanawake waliochanganya damu.

Azerbaijani journalist Arzu Geybulla
Maelezo ya picha, Mwandishi wa Azerbaijan Arzu Geybulla

Mwanahabari wa Azerbaijan Arzu Geybulla,ambaye alishiriki katika mazungumzo hayo aliiambia BBC kuwa unyanyasaji wa mara kwa mara dhidi yake mitandaoni ulimfanya atafakari kuachana na taaluma yake.

Aliongeza kuwa anatilia shaka kama kampuni za teknolojia zinazoendesha mitandao ya kijamii zitawahi ''kutilia maanani suala la unyanyasaji".

TikTok ''tayari'' imewataka watu kutafakari athari ya maneno yao kwa wahusika kabla ya kutuma ujumbe ambao huenda una maudhui ya udhalilishaji au chuki, nayo Twitter imechukua hatua ya kudhibiti ujumbe wenye maudhui yasiyofaa.