Fahamu sayansi inasema nini kuhusu uwezo wa kutabiri ya baadaye

Chanzo cha picha, Getty Images
Dunia ina watu wenye uwezo wa namna tofauti tofauti, wengine uwezo wao unaweza kuuhoji katika misingi ya kawaida ya ubinadamu lakini wengine unaweza kupata shaka na namna wanavyoweza kubashiri kwa namna ya kushangaza kuhusu masuala yajayo.
Je ulijua kile ambacho kingetokea?
Wakati mwingine maisha hutupa fursa ya kujishaua au kusema sema maneno kama vile "Nilikwambia!"lakini pia kuna wale ambao wanajiamini kuwa ni wazuri wa kutabiri ya baadaye.
Lakini ikiwa ni tuwe wa kweli, nyakati nyingi, "tunajua" kwamba kuna kitu kinaweza kutokea, baada ya kuwa kishatokea.
Mwanadamu amekuwa akitabiri ya siku za usoni tangu zamani za kale.
Wachina walikuwa na kile walichokiita I Ching yaani uganga wa Kichina wa zamani huku watabiri wa Ugiriki wakitafuta majibu kuhusu ya baadaye kupitia vilivyomo ndani ya wanyama.
Na leo hii, mashirika ya kijasusi kote duniani yanaegemea zaidi maoni ya wataalam kutabiri matukio yajayo.
Lakini pia kuna watu wa kawaida tu miongoni mwetu ambao huwa wazuri hata kuliko wataalamu linapokuja suala la kutabiri ya baadaye.
Wanawaita "watabiri mahiri" pengine inaweza kushusishwa kama vile unasikika kumhadaa mtu, ila sio kudanganya.
"Hatuzungumzii kuhusu wapiga ramli, hapana," amesisitiza David Robson, mwandishi wa vitabu.
Badala yake, wanasayansi wamebaini sifa maalum za watu wenye uwezo huo.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Ni watu ambao wanaweza kutabiri kwa mfano, vita vya wenyewe kwa wenyewe katika eneo lenye mgogoro au ambaye atashinda katika mashindano ya Olimpiki," Robson alizungumza na kipindi cha BBC CrowdScience.
Wana kipaji maalum cha kutathmni ushahidi na kutabiri yatakayofuatia siku za baadaye.
Watabiri mahiri
Neno "watabiri mahiri" lilitokana na mchezo mmoja, ambao lengo lilikuwa ni kutafuta mbinu mpya za kutabiri matukio ya kisiasa.
Chini ya maagizo ya mwanasayansi wa kisiasa Philip E. Tetlock, tangu mwaka 2011, timu hiyo imekuwa ikialika maelfu ya washirika kutoka jamii mbalimbali kufanyia majaribio ustadi wao wa kutabiri yatakayotokea siku za usoni.
Kwa miaka mingi, timu hiyo imekuwa ikitoa maswali 500 na baadaye kupata zaidi ya matabirio milioni moja na asilimia mbili ya wale ambao wangefanikiwa kutabiri yale ambayo kweli yangetokea wangepewa jina la Watabiri mahiri.

Chanzo cha picha, Getty Images
Na baadaye mradi huo ukachangia kuwepo kwa kampuni ya kibiashara ambayo iliendeshwa na Tetlock, lakini kazi zake zilizopita zilionesha kuwa utabiri wake sio wa uhakika sana.
Lakini je wale watabiri mahiri ambao hawakuchukuliwa kuwa wataalamu, walikuwa na fursa ya kuchukua jukumu muhimu zaidi? Alijiuliza mwanasayansi huyo wa masuala ya kisiasa.
Kuwa na uwazi wa kifikra
Jibu lilikuwa ndio. Baadhi yao walikuwa na uwezo zaidi wa kutabiri sahihi ya baadaye.
Lakini kwanini? Je kipi kilikuwa cha kipekee kwao?

Chanzo cha picha, Getty Images
Sio suala la kuwa "mkarimu au mzingativu" lakini ilikuwa ni kutoshikilia sana maoni fulani.
"Mara nyingi walitaka kujua zaidi, walikuwa na uwazi wa kifikra, walikuwa tayari kutafuta ushahidi na kujiuliza dhana au maoni yao yalikuwa sawa kweli? wanyenyekevu na fikra zilizotulia, kwahiyo, waliweza kutambua upendeleo waliokuwa nao wenyewe na kuchukua jukumu la kujirekebisha," amesema Robson.
Haikuwa tu kuhusu kusikiliza au kufasiri maoni ya watu lakini kuwa na uwezo wa kupitia tena utabiri au maoni kulingana na taarifa zilizopatikana … na wala sio wote wanaoweza kufanya hivyo kwasababu mara nyingi huwa tumeshikilia sana imani zetu." Hayo ni kulingana na Robson.
"Ikiwa kuna kitu makhsusi nilichokibaini ni kwamba watu wengi wanaamini sana imani zao na kuzichukulia za kipekee, walidhania kwamba ni kitu kitakatifu jambo ambalo linastahili kupitiwa tena kulingana na ushahidi uliopatikana kisayansi," amesema mwanasayansi huyo.
Jifanyie majaribio mwenyewe
Kwahiyo, wanasayansi wanachukulia watabiri hamiri matabirio yao kuwa kama dhana fulani na kwamba kila wakati huwa wanatafuta taarifa mpya, wakitathmini data walionayo na kupitia tena utabiri wao.
Aidha, kwasababu huwa na uwazi wa fikra, hufaulu katika utathmini wa kina.
"Inasemekana kuwa mara nyingi, kadiri unavyokuwa mwerevu ndivyo utakavyokuwa mzuri wa kutafuta kila aina ya sababu na misingi ya maoni yako na kutambua mapungufu kidogo wakati unajadiliana na wengine ili tu kupinga wanayosema.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Kwahiyo tatizo hasa ni kwamba kadiri unavyoendelea kuwa mzuri ndivyo unavyokuwa vizuri zaidi kujifanya mjinga mwenyewe na watu wengine."
Pengine ni vizuri hatupati vikwazo kutokana na uwezo wetu wa akili kwasababu hilo lina maanisha kwamba kuna uwezo wa kuimarika kiutabiri.
Lakini mbali na kuwa wawazi wa fikra na watathimini wa kina, kuwa na utabiri mzuri pia kunahitaji uwezo wa kufikiria.
Yaani kufikiria nje ya hali ilivyo kunasaidia (nje ya Boksi)
"Hebu fikiria upo harusini na unaulizwa unadhani uhusiano wa wanandoa utadumu."
Ni rahisi kwako kutazama furaha tu walio nayo siku ya harusi na nyakati zile, " na mara nyingi ukajibu kuwa watakuwa na maisha mazuri," lakini watabiri wazuri watatizama hali ya wakati huo na kufikiria zaidi ya taarifa za tukio hilo.
Kile utakachokuwa unafanya ni kujumuisha hisia zako kwa usaidizi wa taarifa na mengineo kupata jibu sahihi.
"Tunapofanyia watu majaribio ya kuona kama watakuwa watabiri wazuri, huwa hatuangazii tu ufahamu wao kuhusu mada fulani lakini pia ujuzi wao kuhusiana na utambuzi wa matukio."
Na wakati sio wote wenye kipaji hiki, taarifa njema ni kwamba watafiti wanaamini ujuzi huu, mtu anaweza kujifunza.













