Utekelezaji wa amri ya kutotoka nje ya Nairobi - maelfu walikwama kwenye barabara za jiji

Msongamano wa magari

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Maelfu ya waendesha magari na wasafiri walijipata mashakani usiku wa Jumamosi baada maafisa wa usalama jijini Nairobi kufanya oparesheni ya kuhakikisha wakazi wa jiji wanazingatia sheria ya kutotoka nje kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi afajiri.

Hakuna magari yaliyoruhusiwa kuingia au kutoka katika mji mkuu.

Katika baadhi ya barabara polisi waliwaagiza waendesha magari kuzima injini, kutoka ndani ya gari na kukaa kando ya barabara.

Kanda za video zilizowekwa katika mitandao ya kijamii zilionesha msongamano mkubwa wa magari huku baadhi ya magari yanayotoa huduma za dharura kama ambulensi zikipata wakati mgumu kupita katika barabara hizo.

Madereva waliofadhaika walipiga honi mfululizo huku baadhi ya abiria wengine wakiamua kukamilisha safari zao kwa kutembea.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Siku chache kabla ya sherehe za Pasaka, Rais Uhuru Kenyatta alitangaza kusitishwa kwa shughuli zote za usafiri na matembezi ndani ya jiji la Nairobi na majimbo mengine, kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi alfajiri , kama hatua ya kudhibiti mlipuko wa maambukizi ya COVID-19 nchini.

Rais alisema hakuna usafiri wa barabarani ,angani na reli utakaoruhusiwa kuingia na kutoka sehemu hizo zilizotajwa kama zenye janga 'zilizoathiriwa sana na Corona'.

Polisi waliondoa vizuizi vya barabarani saa kadhaa baadae, kuwaruhusu watu kwenda nyumbani.

Rais Wa Kenya Uhuru Kenyatta

Chanzo cha picha, Ikulu,Nairobi

Maelezo ya picha, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

Masharti mengine ni yapi?

Kando na kuzuia usafiri wa watu katika kaunti hizo tano rais Kenyatta pia alipiga marufuku mikutano au mikusanyiko ya watu katika maeneo hayo.

Serikali pia i;ifutoilia mbali pasi zilizokuwa zimetolewa kwa watu wanaotoahuduma muhimu kwani zimekuwa zikitumiwa vibaya na wizara ya Afya na ile ya usalama wa ndani zitatathmini upya mwongozo wa kuzitoa pasi hizo.

Shughuli zote za kuabudu katika kaunti za Nairobi, Nakuru, Machakos, Kiambu, na Kajiado zilizuia hadi wakati uamuzi huo utakapobadilishwa.

Katika sekta ya burudani ,baa haziruhusiwi kuhudumu katika kaunti hizo tano husika na mgaahawa imetakiwa kutoa huduma za kuwapelekea wateja vyakula waliko na imepigwa marufuku dhidi ya kuuza pombe.

Hakuna masomo ya ana kwa ana yatakayokubaliwa na vyuo viku vyote na shule zimefungwa. Wafanyikazi wa mashirika ya serikali na ya kibinafsi wametakiwa kufanyia kazi nyumbani isipokuwa kwa wale wanaotekeleza uduma muhimu zinazowahiaji kwenda kazini.

Hospitali zimetakiwa kupunguza idadi ya watu wanaokuja kuwaona wagonjwa hadi mtu mmoja kwa kila mgonjwa .

Mikutano yote itakayoruhusiwa itakuwa na watu wasiozidi 50 ilhali mazishi yataandaliwa ndani ya kipindi cha saa 72 na ni watu 50 pekee watakaoruhisiwa mazishini .

Serikali pia imesema watu walio na umri wa miaka 58 na zaidi ndio watakaopewa chanjo kwanza.

Usafiri kutoka Nje ya Kenya

Kuhusu usafiri wa kigeni Kenyatta alisema safari zote za kimataifa zitaendelea ingawaje cini ya masharti makali ya kuzuia kusambaa kwa Corona.

Alisema wageni wanaoingia Kenya watahitajika kuwana vyeti malaum vya kuthibitisha kwamba wamepimwa corona na hawana virusi hivyo.

Vipimo hivyo vinafaa kufanywa saa 96 kabla ya kuwasili Kenya .

Kenya ilikuwa imelegeza masharti hayo mwishoni mwa mwaka jana baada ya kupungua kwa visa vya maambukizi lakini idadi ya maamukizi ya ugonjwa huo imekuwa ikiongezeka katika wiki za hivi karibuni.

Nairobi imetajwa kusheheni asilimia 60 ya visa vyote vya maambukizi ya Corona vinavyosajiliwa nchini Kenya