Uchaguzi Tanzania 2020: Tundu Lissu akamatwa na kuachiliwa

Tundu lissu akihutubia vyombo vya habari
Muda wa kusoma: Dakika 2

Mgombea wa urais katika uchaguzi uliokamilika nchini Tanzania kupitia tiketi ya Chadema Tundu Lissu amekamatwa na kuachiliwa baada ya kuhojiwa.

Kulingana na mtandao wa Twitter wa chama cha upinzani Chadema kiongozi huyo alikamatwa na jeshi la polisi.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Tundu Lissu amekamatwa nje ya jengo la ofisi za ubalozi wa Ujerumani, Uholanzi, Uingereza na Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania.

Hatahivyo polisi haijatoa tamko lolote kuhusu kukamatwa kwake .

Wakati huohuo katibu mkuu wa chama cha ACT Wazalaendo Zitto Kabwe amesema kwamba bwana Lissu ameachiliwa huru.

Katika chapisho aliloandika katika mtandao wake Kabwe amesema kwamba Lissu alikamatwa na kuhojiwa kwa muda mfupi kabla ya kuachiliwa.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Chapisho hilo la Zitto Kabwe lilithibitishwa na mtandao wa chama cha Chadema ulioandika muda mfupi uliopita kwamba kiongozi huyo aliyemaliza katika nafasi ya pili katika uchaguzi wa urais uliokamilika nchini Tanzania ameachiliwa.

Ruka X ujumbe, 3
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 3

Baadhi ya viongozi wa upinzani nchini Tanzania wanashikiliwa na polisi baada ya kutangaza kupanga maandamano ya amani siku ya Jumatatu tarehe mbili mwezi Novemba ili kuonesha kutokubaliana na matokeo ya uchaguzi.

Polisi wanasema walimkamata mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Chadema bwana Freeman Mbowe pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema na aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam Boniface Jacob.

Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema walipiga marufuku maandamano hayo yaliyopangwa kuanza leo asubuhi, lakini viongozi wa Chadema "wameonekana kufanya vikao kuratibu maandamano ya fujo".

Amesema viongozi hao walipanga kuhatarisha usalama wa raia kwa kufanya vurugu kuonyesha kutokubaliana na matokeo, na kwamba walipanga kuingia mtaani kuchoma maeneo mbalimbali kama masoko, magari na vituo vya mafuta.

Aidha amesisitiza kuwa operesheni kubwa inaendelea kwa yeyote ambaye atashiriki kuratibu, kuwezesha au kushiriki katika maandamano hayo atafikishwa kwenye mikono ya sheria.

Baada ya rais John Magufuli kutangazwa kuwa rais kwa awamu ya pili siku ya Ijumaa usiku, viongozi wa vyama vikuu vya upinzani nchini Tanzania walitangaza kutokubaliana na matokeo hayo na kuitisha maandamano leo hii.