Paul Pogba: Kiungo wa kati wa Manchester United apatikana na virusi vya corona

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba amepatikana na virusi vya corona, amesema kocha Mfaransa Didier Deschamps.
Mchezaji huyo, 27, atahitajika kujitenga na kumaanisha kwamba hatashiriki michuano ya Ligi ya Taifa la Ufaransa.
Mfaransa huyo alisafiri kwenda Sweden kushiriki michuano ya ufunguzi ya Timu ya Taifa Jumamosi, Septemba 5.
Hata hivyo, Pogba huenda akachaguliwa katika uteuzi wa timu ya ufunguzi ya United kwenye Ligi ya Primia dhidi ya Crystal Palace huko Old Trafford Septemba, 19.
Klabu yake imesema: "Kila mmoja United anamtakia Paul uponyaji wa haraka kabla ya kuanza kwa msimu ujao."
Nafasi ya Pogba katika kikosi cha Ufaransa itachukuliwa na kiungo wa kati wa Rennes Eduardo Camavinga, 17.
"Nimemaliza, mabadiliko ya dakika ya mwisho," Deschamps amesema Alhamisi.
"Paul Pogba, ambaye alikuwa kwenye ratiba tangu awali, lakini bahati mbaya amefanyiwa vipimo jana na majibu yalipotoka asubuhi, yakaonesha kwamba amepata maambukizi ya virusi vya corona."












