'Dunia mbili kubwa' zaidi zenye uhai zagunduliwa karibu na mfumo wa jua

Chanzo cha picha, Mark Garlick/PA Wire
Sayari mbili zaidi zimegunduliwa na kundi moja la wanasayansi wa kimataifa karibu na mfumo wa jua.
Na kuna uwezekano wa sayari nyengine ya tatu karibu na sayari hizo mbili.
Sayari zote mbili zinazunguka kwa ukaribu -nje ya eneo lenye uhai kwa jina GJ887 - nyota ndogo iliopo umbali wa miaka 11 ya mwanga wa jua.
Ukaribu uliopo kati ya sayari hizo mbili na nyota - ni mkubwa kuliko ukaribu kati ya Mercury na jua.
Sayari hizo mbili ambazo uwepo wake umethibitishwa , zimetajwa kuwa 'dunia kubwa' .
Zina ukubwa ambao ni mara 4 na saba zaidi ya dunia, lakini ziko sawa na Uranus na Neptune.
''Pia zimedaiwa kuwa na msingi dhabiti'' , amesema Sandra Jeffers wa chuo kikuu cha Gottingen na kiongozi wa utafiti huo, akizungumza BBC.
Sayari hizo zinaaminika kuwa na mazingira yenye uzito ikiliganishwa na dunia yetu.
Utafiti huo ulifanywa na mradi wa Red Dots, na kubuniwa na vyuo mbalimbali duniani ili kutafuta sayari zinazofanana na dunia na zilizo karibu na mfumo wa jua na matokeo yake yakachapishwa katika jarida la sayansi .
Je ni nini kinachojulikana kuhusu dunia hizi mbili zilizopo karibu?
'Kamera zenye uwezo mkubwa'
Sayari zote mbili, zilizopewa majina ya GJ 887b na GJ 887c, ziligunduliwa kwa kutumia chombo chenye mionzi ya kiwango cha juu kinachotafuta sayari European Southern Observatory (ESO) kilichopo huko La Silla, nchini Chile.

Chanzo cha picha, ESO/M. Kornmesser
Kulingana na uchunguzi, sayari hizo mbili zipo karibu na nyota yao.
Ile iliopo mbali na nyota hiyo, GJ 887c, huchukua takriban siku 21.8 za dunia ya kawaida kufanya mzunguko mmoja na GJ 887b huchukua siku tisa 9.3 za duniani kukamilisha mzunguko mmoja katika jua.
Mizunguko hiyo ni ya kasi na mifupi ukilinganisha na sayari ya Mercury ambayo huchukua siku 88 za duniani kukamilisha mzunguko mmoja katika jua.
Wataalam wa angani tayari wamegundua sayari nyengine zilizopo karibu na mfumo wa jua kama vile Proxima Centauri na Wolf 359, iliopo umbali wa miaka 4.2 na 7.9 ya mwanga mtawalia. Lakini hazipo karibu sana kama vile GJ887.
Hivyobasi sayari ya GJ887 ndio ilio karibu zaidi. Lakini GJ887 ndio iliojikusanya karibu zaidi , kulingana na taasisi ya fizikia ya angani Andalusia (IAA-CSIC. ilioshiriki katika utafiti huo..
''Mifumo hii ya sayari hupatikana sana katika nyota nyingine - kati ya asilimia 15 hadi 30 ya nyota ya solar-type - lakini hatujawahi kuona moja ilio karibu sana na jua," alisema Guillem Anglada-Escudé, kutoka taasisi ya sayansi ya angani (ICE-CSIC) kutoka chuo kikuu cha Barcelona na mmoja wa wwanzilishi wa utafitoi huo.
'Nyota bora zaidi'
Sayari hizo mbili zinapatikana karibu na eneo lenye uhai karibu na nyota .
Hiyo ni eneo ambalo sayari za mfumo fulani zinaweza kuwa na mazingira ambayo yanaruhusu uhai

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini nje ya ukanda huo, wanasayansi wanaamini kuwa GJ 887b na GJ 887c zinaweza kuwa na joto kali sana kiasi cha kwamba maji hayawezi kusalia katika hali ya yake.
Viwango vya nyuzi joto vya dunia zote mbili zinakadiriwa kuwa kati ya 70º na 200ºC, kulingana na Taasisi ya tafiti wa angani iliopo catalonia.
Walakin, watafiti wa mradi huo wanasema kwamba nyota kwa jina GJ 887 haina utendakazi wowote hatua inayopendelewa na mazingira ya sayari zinazokaribiana.
Iwapo GJ 887 "ingekuwa na uhai kama ilivyo katika Jua , kuna uwezekano kwamba upepo mkali wenye nguvu ungefagia anga za sayar hiyoi," Kulingana na Chuo Kikuu cha Göttingen katika taarifa iliyotolewa Alhamisi.
Lakini kukosekana kwa upepo huo kunamaanisha kuwa "sayari mpya zilizogunduliwa zinaweza kusalia na anga zao, au kuwa na mazingira mazito kuliko dunia, na uwezekano wa kubeba maisha, licha ya kwamba zinapokea mwanga zaidi kuliko Dunia," anaongeza.
"Sayari mpya zilizogunduliwa zina uwezekano mkubwa kuona iwapo zina mazingira na kuzitafiti kwa undani . Kwa kuzisoma, wanasayansi wataweza kuelewa iwapo mazingira hayo yanafaa kwa uhai ," Jeffers pia aliiambia BBC World.
Sayari ya tatu?
Wanasayansi waligundua ishara za kile kinachowezekana kuwa sayari ya tatu , ambayo ni kubwa zaidi ya mbili za kwanza katika mfumo wa GJ 887.
Sayari hiyo ya tatu itakuwa miongoni mwa maeneo yenye uhai.

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images
Dkt. John Barnes, mtaalamu wa uchunguzi katika Chuo Kikuu cha Open huko Uingereza na mwingine wa waandishi wa utafiti huo, waliambia Chombo cha habari Cha (PA) kwamba "ikiwa ishara hiyo inatoka kwa sayari, itakuwa na mzunguko wa siku 51".
"Hatahivyo, tunaona ishara zilizo na kipindi kama hicho ambacho tunajua lazima kinatoka katika nyota. Ndiyo maana hatuwezi kusema kwamba ishara ya tatu ni ya sayari. Iwapo uchunguzi wa baadaye utathibitisha kama ni sayari, itapatikana ndani ya eneo lenye uhai, "akaongeza Barnes.
Melvyn Davies, profesa wa anga za juu katika Chuo Kikuu cha Lund nchini Sweden, ambaye hakuhusika katika utafiti huo, aliandika katika jarida la Sayansi, kwamba "ikiwa uchunguzi mwingine unathibitisha uwepo wa sayari ya tatu katika eneo lenye uhai, basi GJ 887 inaweza kuwa moja ya mifumo ya sayari iliyosomwa zaidi katika eneo lililo karibu na jua. "












