Wingu lisilo la kawaida linalosafiri kilomita 10,000 kutoka Afrika hadi Amerika

Chanzo cha picha, NOAA
Wingu jeusi lililojaa vumbi limekuwa likitanda katika eneo la Atlantic kwa siku kadhaa.
Katika picha zilizonaswa na setlaiti kutoka Afrika hadi eneo la Caribbean, wingu hilo lenye rangi ya kahawia limetanda katikati ya mawingu meupe yaliopo kama kawaida wakati mwengine wa mwaka.
Ni ishara nyengine kwamba safu nyengine ya hewa ya eneo la sahara - iliokauka na yenye vumbi jingi kutoka katika jangwa la kaskazini mwa Afrika - linaelekea America ya kusini.
Katika eneo la Caribean tayari wameanza kuhisi athari zake: Mataifa kadhaa katika eneo hilo yamependekeza kwamba raia wake wavalie barakoa na kutotoka nje kutokana na wingi wa vipande vidogo vidogo katika hewa hiyo.
Pia zimetoa onyo kwa wahudumu wa baharini kama wenye maboti kuchukua tahadhari kwani hewa hiyo inaweza kuwazuia kuona wanaokoelekea.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kulingana na Olga Mayol, mtaalamu katika taasisi ya masomo ya mifumo ya kitropiki katika chuo kikuu cha Puerto Rico, mawingu hayo yana vipande vingi vya vumbi kuwahi kuonakana katika eneo hilo katika nursu karne ya mwisho.
Wingu hilo la kiasilia lilianza kuonekana katika eneo la Afrika magharibi wiki moja iliopita na sasa limesafiri zaidi ya kilomita 5000 kuelekea eneo la Caribbean , ikiwemo Marekani na Vinezuela.
Shirika la hali ya hewa nchini Marekani NOAA linasema kwamba vumbi hilo la sahara litaendelea kusogea kuelekea magharibi kupitia bahari ya Caribbean hadi litakapofika maeneo ya kaskazini mwa kusini mwa Amerika, katikati ya America na pwani ya ghuba la Marekani katika siku zijazo.
Mataifa kadhaa katika maeneo hayo tayari yameripoti kuwepo kwa vumbi hilo kutoka jangwa la sahara na watumiaji wa mitandao ya kijamii wamesambaza picha za eneo lililobadilishwa na wingu hilo mbali na rangi nzuri zinazojitokeza wakati wa alfajiri na jioni jua linapotua.

Chanzo cha picha, EPA
Je wingu hilo husababishwa na nini?
Hewa kavu, iliojaa vipande vidogo vidogo vya vumbi hutanda katika jangwa la sahara mwisho wa msimu wa baridi na hewa hiyo husafiri kuelekea eneo la magharibi juu ya anga ya bahari ya Atlantic kila baada ya siku tatu ama tano.
Inapotokea, hufanyika kwa mufa mfupi: haichukui zaidi ya wiki moja, lakini uwepo wa upepo mkali wakati fulani wa mwaka kuna uwezekano kuvuka bahari ya Atlantic na kusafiri kwa takriban kilomita 10,000.
Je tukio hilo hufanyika mara ngapi?
Kuwasili Amerika kwa wingu hilo sio suala la kawaida na hufanyika mara kadhaa kwa mwaka, hatahivyo kulingana na wataalam wa hali ya hewa, wingu hilo ni mojawapo ya mawingu mazito zaidi ambayo
limewasili katika nusu ya mwisho ya karne.
Kwa kawaida, wingu hilo la sahara huongezeka katikati ya mwezi Juni, huanza kujikusanya mwisho wa June hadi katikati ya mwezi Agosti na kuanza kutoweka kwa kasi .
Je lina athari gani?
Kama matukio yote ya kiasili, mawingu ya vumbi la Sahara huchangia kwa njia tofauti ya mizunguko ya asili ya sayari.
Vumbi linashirikisha kemikali ambazo hutoa mbolea kwa mchanga na bahari.
Vumbi hilo lenye madini hufyonza jua hatua ambayo inachangia kudhibiti joto la sayari.
Madini yanayopatikana katika vumbi hilo pia husambazwa katika mchanga wa Tropiki kupitia mvua inayonyesha katika eneo hilo.
Baadhi ya kemikali zilizopo katika vumbi hilo husababisha uhai baharini, ijapokuwa baadhi ya wataalam wameonya kwamba baadhi ya sumu huenda zikadhuru baadhi ya spishi kama vile matumbawe.
Kulingana na Shirika la hali ye hena baharini nchini Marekani NOAA, joto hilo ,ukavu na upepo mkali unaosababishwa na hewa hiyo ya jangwa la sahara pia hukandamiza ukusanyaji wake na kuongezeka kwa vimbunga vya tropiki.
Shirika la Vimbunga nchini Marekani limekadiria mwaka huu kwamba kutukuwa na vimbunga vingi zaidi ya kawaida, lakini iwapo mawingu ya aina hii yatatanda hewani huenda kasi ya vimbunga hivyo ikapungua.
Je wingu hilo lina maana gani kwa afya ya binadamu?
Mojawapo ya madhara mabaya yanayotokana na vumbi hilo uhusishwa na afya ya binadamu kwa kuwa linaathiri ubora wa hewa.
Hewa kavu ilio na vumbi kutoka jangwa la sahara ina unyevu wa asilimia 50 zaidi hatua ambayo huathiri ngozi na mapafu.
Vipande vyake pia vinaweza kumdhuru binadamu na magonjwa ya kupumua na hata kusababisha mzio ama kuwashwa na macho na pua.
Siku ya Jumapili , idara ya afya nchini Purto Rico iliwaonya watu wanaougua asthma na magonjwa ya mfumo wa kupumua na wale wenye mzio, pamoja na wale walioathrika na Covid 19 kwamba wanafaa kuchukua tahdhari ili kutoathrika zaidi.













