Virusi vya corona: Tutaweza vipi kulinda bayoanuwai wakati wa corona?
Leo ni siku ya mazingira duniani ambayo imekuwa ikiadhimishwa tangu 1974, Mwaka huu kauli mbiu ni kusherehekea bayoanuai. Hayo yanakuja huku ulimwengu ukishuhudia majanga ya kila aina, kuanzia la kiafya la virusi vya Corona, ukame, mafuriko, vina vya maji baharini kuongezeka na mataifa kadhaa yakivamiwa na nzige wanaotishia kusababisha baa la njaa.
Lakini je ni upi umuhimu wa bayoanuwai kwa binadamu?, na ni vipi tunaweza kuepuka athari za virusi vya corona kwa mazingira?.
Naibu Mkurugenzi mkuu wa shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP Bi Joyce Msuya pamoja na mwanaharakatii wa mazingira na muasisi wa wakfu wa Green Afrika nchini Kenya Dkt Isaac Kalua, wamezungumza na Caro Robi