Virusi vya Corona: Obama asema uongozi wa Trump umefeli kukabiliana na ugonjwa huo

Barack Obama amemkosoa Rais Donald Trump mara mbili katika siku za hivi karibuni

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Barack Obama amemkosoa Rais Donald Trump mara mbili katika siku za hivi karibuni
Muda wa kusoma: Dakika 2

Aliyekuwa rais wa Marekani Barrack Obama kwa mara nyingine tena amemkosoa mrithi wake Donald Trump kwa jinsi anavyolishughulikia suala la virusi vya corona.

Katika hotuba kwa hafla iliyopeperushwa kupitia mtandao, alisema kwamba mlipuko wa virusi vya corona umedhihirisha kwamba maafisa wengine hawafanyi kazi walioajiriwa kusimamia.

Amesema kwamba ni 'janga la machafuko' jinsi Trump anavyoangazia suala hilo , katika mkutano uliovuja wiki iliopita.

Rais huyo wa zamani pia aliwahutubia wanafunzi wa shule ya upili katika sherehe ilioandaliwa na LeBron James na ilikuwa mojawapo ya programu maalum ambayo ilishirikisha watu maarufu kama vile ndugu wa Jonas, Megan Rapinoe, Pharrell Williams na mwanaharakati wa elimu Malala Yousafzai.

Katika hotuba yake kwa takriban zaidi ya taasisi 10 za wanafunzi weusi na vyuo vikuu, bwana Obama alisema kwamba Covid-19 ilifichua mianya na makosa katika uongozi wa taifa hilo.

''Zaidi ya chochote kile janga hili linaonesha wazi kwamba wengi wa maafisa walio uongozini hawajui wanachofanya'', alisema.

Zaidi ya watu 1,200 wamefariki kutokana na virusi vya corona nchini Marekani katika kipindi cha saa 24, kulingana na takwimu mpya kutoka Chuo kikuu cha John Hopkins.

Idadi ya watu waliofariki ni 89,000, ambayo ndio ya juu zaidi duniani.

Bwana Obama pia alizungumzia kwa urefu jinsi virusi hivyo vinavyozidi kuiathiri jamii ya watu weusi nchini humo.

''Ugonjwa kama huu unafichua ukosefu wa usawa uliopo na mzigo wa ziada ambao jamii ya watu weusi wamekuwa wakikabiliana nao katika historia ya taifa hili'', alisema.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Idadi kubwa ya Wamarekani weusi wamekufa na wengine kulazwa hospitalini nchini Marekani kutokana na Covid-19.

Rais huyo wa zamani pia alizungumzia kuhusu mauaji ya Ahmaud Arbery aliyekuwa akifanya mazoezi ya kukimbia - ambaye alipigwa risasi na maafisa wa polisi weupe mwezi February - katika hotuba yake.

Alisema kwamba ubaguzi wa rangi ulibainika wazi nchini humo wakati mtu mweusi anapofanya mazoezi ya kukimbia na watu fulani wanahisi kwamba wanaweza kumsimamisha na kumuuliza maswali na kumpiga risasi, anapokataa kuwajibu.

''Iwapo dunia itaimarika , itategemea nyinyi'', aliwaambia mahafala hao.

coronavirus

Bwana Obama amenyamaza kwa kipindi kirefu tangu alipoondoka madarakani mnamo mwezi Januari 2017 na hajawahi kuzungumzia kuhusu vitendo vya mrithi wake.

Lakini wawili hao wamekabiliana vilivyo katika siku za hivi karibuni, hatua iliomfanya rais Trump kumshutumu Obama na washauri wake kwa kuendeleza juhudi za kihalifu kuhujumu utawala wale.

''Ni uhalifu mkuu wa kisiasa katika historia ya Marekani , kwa kiwango kikubwa'', rais huyo aliandika katika mtandao wake wa twitter wiki iliopita.