Virusi vya corona: Marekani huenda ikakumbwa na wimbi la pili la maambukizi

Chanzo cha picha, Getty Images
Maafisa wa afya wa ngazi ya juu wa nchini Marekani wameonya wimbi jipya la maambukizi ya corona.
Mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia magonjwa Robert Redfield amesema kuna hatari ya mlipuko mpya wa ugonjwa wa Covid-19 kugongana na msimu wa mafya.
Itakuwa na ''athari kubwa sana" kwa mfumo wa afya wa Marekani, alisema.
Marekani imeshuhudia maambukizi zaidi ya 800,000 - ambayo ni ya juu zaidi duniani.
Watu zaidi ya 45,000 wamefariki kufikia sasa kutokana na ugonjwa wa corona nchini Marekani, kwa mujibu wa takwimu za chuo kikuu cha Johns Hopkins.
Siku ya Jumatatu,Jimbo la California lilitajwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi mapya huku mji wa New York, ukiwa na idadi kubwa ya vifo vilivyotokana na ugonjwa wa corona.

Chanzo cha picha, Reuters
Katika matukio mengine nchini Marekani:
- Rais Trump amesema kuwa atasitisha maombi ya viza za Green card,- ambayo inampa fursa mhamiaji uhalali wa kuwa na kibali cha kuishi Marekani na fursa ya kuomba uraia wa Marekani kwa kipindi cha siku- 60.
- Chuo kikuu cha Harvard kimesema kuwa kitatoa msaada wa dola milioni 8.6 licha ya kupata msukumo kutoka kwa rais Trump kuzirejesha.
- Visa vya kwanza vya virusi vya corona katika jimbo la Californiavilionekana mapema zaidi ya walivyofikiria maafisa wa afya walithibitisha. Uchunguzi umebaini kuwa mtu mmoja aliyefariki akiwa nyumbani Februari 6 katika mji wa Santa Clara amejulikana kuwa ni miongoni mwa maambukizi mapya Marekani.Mpaka sasa maambukizi mapya , yanadhaniwa kuwa ni ya mkazi wa Washington ambaye alifariki Februari 26.
- Seneta mmoja wa Marekani ametoa dola bilioni 484 ili kusaidia ufadhili wa biashara ndogo ndogo, fedha hizo zitasainiwa kutolewa kisheria siku ya Alhamisi.
Katika mahojiano ya kwenye gazeti la Washington Post, bwana Redfield alisema kuwa kuna uwezekano kuwa virusi vikarejea upya katika msimu ujao wa baridi, na hali inaweza kuwa mbaya zaidi ya wakati huu.
Amewataka maofisa wa Marekani kujiandaa kukabiliana na mlipuko mwingine wa mafua makali wakati kama huu.
'Hali ni ngumu sana'
Bwana Redfield alisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa chanjo ya mafua.
Anasema upatikanaji wa chanjo unaweza kuwasaidia kuwa na hospitali zenye vitanda ambavyo viko wazi kwa ajili ya wazee ambao watapata virusi vya corona.
Mkuu wa kituo cha kudhibiti magonjwa CDC anasema, virusi vya corona vinaweza kuingia Marekani katika msimu wa kawaida wa mafua.
Lakini kama virusi hivyo vinaweza kuibuka wakati ambao kuna msimu wa baridi kali basi hali itakuwa mbaya, mbaya, mbaya sana.


Tahadhari hiyo imetolewa wakati ambao maseneta wa majimbo mbalimbali nchini Marekani wanaondoa marufuku au wanapunguza masharti ya kutoka nje.
Bwana Redfield alisema kuwa watu kuwa kwa mbalimbali ndio jambo sahihi ili kuzuia maambukizi ya virusi hivi vipya, ni muhimu hata makatazo ya mizunguko ifunguliwe.

Chanzo cha picha, AFP
Maafisa wanapaswa kuchukua hatua ya kuwapima watu ili kufahamu wale ambao wana maambukiz, na watu waliohusiana nao.
Kituo cha kukabiliana na magonjwa kina mpango wa kuajiri watu wengine zaidi ya 650 ili kuweza kuwabaini watu hao.
Anasema, wale waliokuwa wanapinga mafuruku ya kutotoka nje ''haisaidii''.
CDC pia inatathmini uwezekano wa kutumia wafanyakazi wa sensa kusaidia kuwatafuta watu.












