Virusi vya corona: Aina saba ya watu wanaoanzisha na kusambaza taarifa feki

Nadharia za upotoshaji, taarifa za uongo au uvumi kuhusu virusi vya corona imekuwa ikisambaa kwa wingi kwenye mitandao ya kijamii.
Lakini ni nani huwa anazusha uvumi huo? Na nani huwa anasambaza?
BBC imechunguza mamia ya simulizi za uongo katika kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya corona.
Tumepata wazo kuhusu nani anahusika na taarifa hizi za uongo na nini kinawahamasisha kufanya hivyo.
Aina saba za watu ambao huanzisha na kusambaza taarifa za uongo:
Wachekeshaji

Unaweza kudhani kuwa hakuna mtu ambaye anaweza kudanganywa na ujumbe wa sauti unaotumwa WhatsApp kudai kuwa serikali inawapikia chakula kingi katika uwanja wa mpira wa Wembley ili kuwalisha wakazi wa London.
Lakini baadhi ya watu hawakudhani kuwa ni utani.
Kwa kufanya ujumbe huo kuonekana kuwa wa muhimu sana, walitengeza picha ya uongo ya ujumbe wa serikali unaodai kuwa kuna baadhi ya watu walitozwa faini kwa kutoka nje ya nyumba zao mar nyingi.
Alidhania kuwa anawachekesha watu kwa kuwatisha kwa kutofuata sheria za marufuku ya kutotoka nje.
Baada ya kuwahamasisha wafuatiliaji wake katika mtandao wa kijamii wa Instagram, ujumbe huo ulifika kwenye makundi mengine ya watu kwenye mtandao wa Facebook eneo ambao wakazi wa eneo hilo walipata shaka na kudhani kuwa suala hilo ni la kweli.
"Kiukweli, sikuwa nataka kusababisha taharuki yeyote," alisema prankster, ambaye hakusema jina lake la kweli.
"Lakini kama waliamini picha ya kwenye mtandao wa jamii inabidi wajitathmini namna wanavyopokea taarifa katika mtandao.
Wahalifu mtandaoni

Ujumbe mwingine wa kugushi unaodai kuwa serikali au halmashauri za mitaa zinatumia njama za kuwaibia watu katika mlipuko huu.
Kashfa kama hiyo ulichunguzwa na kituo kimoja cha kusaidia wahitaji mwezi Machi , na kulikuwa na madai kuwa serikali inataka kuwalipa watu kwa kuwapa unafuu wa maisha na kuwataka watume taarifa za benki.
Picha za uongo huo zilishirikishwa kwenye mtandao wa Facebook.
Kwa kuwa ujumbe huo ulitumwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa kawaida, ilikuwa ni vigumu kubaini nani anahusika na utapeli huo.
Matapeli hao walianza kutumia njama hiyo tangu mwezi Februari kufanikiwa kupata pesa kwa siku za mwanzoni.
Wanasiasa

Taarifa hizi za uongo huwa hazitoki tu hewani na kufika mtandaoni bali kuna vyanzo vyake.
Wiki iliyopita rais Donald Trump alihoji kama kuachia wazi miili ya wagonjwa au kuwachoma sindano ili wapate mwanga kunaweza kusaidia kupna virusi vya corona.
Alikuwa anafikira tu bila kuangalia mazingira yanayomzunguka.
Baadae, alidai kuwa maoni yake yalikuwa hayana ukweli wowote. Lakini hayakuwafanya watu kuacha kupiga simu mtandaoni kuuliza namna ya kujitibu kama alivyoelekeza rais.
Si rahisi wa Marekani peke yake bali hata msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China aliyedai kuwa inawezekana virusi vya corona vililetwa mjini Wuhan na askari wa Marekani.
Nadharia hizo ambazo hazina ukweli wowote kuhusu mlipuko wa corona zimekuwa zikijadiliwa katika TV ya Urusi ya taifa na kwenye akaunti za Twitter za pro-Kremlin.
Simulizi za uongo

Kutokuwa na uhakika wowote juu ya ukweli kuhusu virusi vya Corona kumesababisha kwa njama nyingi za uongo kujitokeza.
Simulizi ya uongo kuhusu mtu wa kwanza kujitolea katika jaribio la chanjo ya corona nchini Uingereza kuwa alifariki zilisambaa katika mtandao wa Facebook.Wakati lilikuwa si jambo la kweli bali hadithi tu.
Mahojiano ya David Icke katika YouTube, ambayo yalikuwa yameondolewa pia yalikuwa yamezusha uongo kuwa 5G inahusiana na mlipuko wa virusi vya corona.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Bwana Icke alionekana kwenye kituo cha TV London, ambacho kilibainika kuwa kiko chini ya kiwango cha utangazaji wa Uingereza.
Kurasa yake ya Facebook baadae iliondolewa katika kampuni kwa kuchapisha taarifa za uongo kuhusu afya ambazo zingeweza kusababisha madhara makubwa kwa watu".
Nadharia hizo za uongo ziimesababisha nguzo za 5G kushambuliwa.
Wataalamu wa afya wenyewe

Mara nyingine, taarifa ambazo si za kweli zinaonekana kutoka katika vyanzo vya kuaminika kama - madaktari , maprofesa au wafanyakazi wa Hospitali.
Lakini mara nyingi wahusika huwa hawachapishi vitu vya uongo.
Mwanamke mmoja kutoka Crawley huko West Sussex alizua taharuki kwa kutuma ujumbe wa sauti wa kushtua kuwa idadi ya ya vijana na watu wenye afya njema imeongezeka kusumbuliwa na virusi vya corona.
Alidai kuwa ana taarifa za ndani kwa sababu anafanya kazi katika kitengo cha huduma ya dharura.
Hakujibu maoni yalioandikwa kuwa atume kidhibitisho cha ajira yake ili wafahamu kama kweli ni mhudumu wa afya au la.
Lakini madai aliyoyasema katika ujumbe wake wa sauti hayakuwa ya kweli.
Jamaa

Ujumbe wa sauti kutia hofu na nyingine nyingi zilisambaa na kufanya watu kuwa na wasiwasi , na wengine kutuma kwa marafiki zao na familia.
Kuna huo mmoja ambao ulimjumuisha Danielle Baker, mama wa watoto wanne kutoka Essex, aliyetuma ujumbe kutoka Facebook messenger akidhania kuwa wakweli.
"Mara ya kwanza, alishtuka akadhani kuwa hauna ukweli kwa sababu alitumiwa na mwanamke ambaye hakuwa anamjua,"alisema.
"Nikautuma kwa dada zangu kwa sababu walikuwa na watoto wa umri mmoja na wanangu na watoto wengine walikuwa wakubwa kidogo na wote wako katika hali kubwa ya hatari katika vitu wanavyotumia nyumbani."
Wanajaribu kuonekana kama wanasaidia kwa kufanya kitu ambacho kinaweza kusaidia jamii lakini kumbe ni uongo tu.
Watu maarufu

Si mama au mjomba wako tu anaweza kukupat taarifa ambazo hazina ukweli. Watu maarufu huwa wanaidia kurahisisha taarifa za uongo kusambaa zaidi kwa haraka.
Mwanamuziki wa M.I.A. na muigizaji Woody Harrelson ni miongoni mwa watu ambao walikuwa wanahamasisha kwenye mitandao ya kijamii kuwa 5G imesababisha uwepo wa virusi vya corona.
Taarifa ya hivi karibuni iliyoandikwa na shirika la habari la Reuters imebaini kuwa watu mashuhuri wanachangia kwa kiwango kikubwa kusambaza mtandaoni taarifa ambazo hazina ukweli.
Wengi wao huwa wanafuatiliwa na watu wengi katika kurasa zao za mitandao ya kijamii na hata wakiongea kwenye tv au radio huwa wanasikilizwa na watu wengi.













