Tetesi za soka Jumatano: Vilabu vya Saudia vyaelekeza macho kwa Salah

Salah

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Vilabu vya Ligi Kuu ya Saudia vina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, mwenye umri wa miaka 33, ambaye aliachwa nje ya kikosi cha Liverpool Jumapili. (Talksport)

Liverpool wameanzisha tena mazungumzo na wawakilishi wa mlinzi wa England Marc Guehi, wakitaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kutoka Crystal Palace mwezi Januari, baada ya kumkosa majira ya kiangazi. (Teamtalk)

Manchester United wanamnyemelea kiungo wa Olympiacos na timu ya taifa ya Ugiriki Christos Mouzakitis, huku Real Madrid pia wakifikiria kutoa ofa ya pauni milioni 25 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18. (Mail)

Unaweza kusoma

Barcelona bado hawajaamua kama watamsajili moja kwa moja mshambuliaji wa England Marcus Rashford, mwenye miaka 28, pale mkopo wake na Manchester United utakapomalizika. (Sport)

Liverpool ni miongoni mwa vilabu vinavyoongoza katika harakati za kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth na Ghana Antoine Semenyo, mwenye miaka 25. (Football Insider)

Tottenham wanazidisha nia yao kwa Semenyo na wanaweza kumsajili Mghana huyo mwezi Januari. (Sky Sports)

 Antoine Semenyo

Chanzo cha picha, Getty Images

Gary O'Neil yuko kwenye majina yanayozingatiwa kuchukua nafasi ya ukocha Leeds iwapo wataamua kumfuta kazi kocha kutoka Ujerumani Daniel Farke. (Football Insider)

West Ham na Brentford wanawaza kutoa ofa Januari kwa mlinzi wa Kireno Tiago Gabriel, mwenye miaka 20, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Juventus kwa mlinzi huyo wa Lecce. (The i Paper)

Beki Timothy Castagne, mwenye miaka 29, anaweza kuondoka Fulham mwezi Januari ili kuhakikisha anapata nafasi kwenye kikosi cha Ubelgiji kuelekea Kombe la Dunia msimu ujao. (DH)

Timothy Castagne

Chanzo cha picha, Getty Images

Mlinda lango wa Italia Guglielmo Vicario anafikiria kuondoka Tottenham huku Inter Milan wakionesha nia ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29. (La Gazzetta dello Sport)

Liverpool na Arsenal wanajiandaa kutoa ofa mwezi Januari kwa mshambuliaji wa Real Madrid na Brazil Rodrygo, mwenye miaka 24. (Caught Offside)

Liverpool wamewatangulia Barcelona katika mbio za kumsajili kiungo wa Atalanta na Brazil, Ederson, mwenye miaka 26. (Fichajes)

Bayern Munich wako tayari kujadili dili la euro milioni 15 (£13.2m) au zaidi ili kumuuza mlinzi wa Ufaransa Sacha Boey, mwenye miaka 25, ambaye anaivutia Crystal Palace. (Bild)

Vilabu kadhaa vya Ligi Kuu ya England vinamfuatilia mlinda lango wa Benfica na Ukraine Anatoliy Trubin, mwenye miaka 24. (GiveMeSport)