Tetesi za soka Jumanne: Trafford anataka kuondoka Manchester City

 Trafford

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Mlinda lango wa Kiingereza wa Manchester City, James Trafford, mwenye umri wa miaka 23, anataka kuondoka klabuni mwezi Januari baada ya kushuka nafasi katika chaguo la makipa kufuatia kuwasili kwa mlinda lango wa timu ya taifa ya Italia Gianluigi Donnarumma, mwenye umri wa miaka 26, kutoka Paris St-Germain.

Wakati huo huo, mlinda lango wa Kijerumani Stefan Ortega, 33, huenda pia akatafuta changamoto mpya. (Mail)

Mshambuliaji wa Crystal Palace wa Ufaransa, Jean-Philippe Mateta, 28, anatamani kuhamia Serie A, huku AC Milan ikiwa miongoni mwa vilabu vinavyovutiwa. (Talksport)

Atletico Madrid ilikataa jaribio la Manchester United kumsajili Conor Gallagher kwa mkopo majira ya kiangazi yaliyopita, lakini klabu hiyo ya Hispania huenda ikawa tayari kumuachia kiungo huyo wa England, 25, kwa takribani pauni milioni 26 mwezi Januari. (Here We Go Podcast and Fabrizio Romano)

Unaweza kusoma
Conor Gallagher

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambuliaji wa Newcastle, William Osula, 22, bado anatakiwa na Eintracht Frankfurt, lakini klabu hiyo ya Bundesliga haina nia tena ya kumsajili mshambuliaji wa West Ham na timu ya taifa ya Ujerumani Niclas Füllkrug, 32. (Sky Sports Germany)

Arsenal wamefikia makubaliano ya awali ya kuwasajili mapacha kutoka Ecuador, Edwin na Holger Quintero, wote wakiwa viungo washambuliaji wenye umri wa miaka 16, kutoka Independiente del Valle, watakapofikisha umri wa miaka 18 mnamo Agosti 2027. (ESPN)

Sunderland wanataka kumsajili mchezaji wa zamani wa Arsenal Matteo Guendouzi, 26, huku kiungo huyo wa Lazio na timu ya taifa ya Ufaransa akiwa tayari kutazama uwezekano wa kujiunga na Black Cats. (i Paper)

Matteo Guendouzi

Chanzo cha picha, Getty Images

Roma watafikiria kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Mathys Tel, mwenye umri wa miaka 20, mwezi Januari endapo watashindwa kumpata mshambuliaji wa Manchester United, Joshua Zirkzee, 24, raia wa Uholanzi. (Il Messaggero)

Manchester United wanamfuatilia beki wa kushoto wa Eintracht Frankfurt na timu ya taifa ya Ujerumani, Nathaniel Brown, 22, ambaye pia anawavutia Real Madrid na Barcelona. (Florian Plettenberg)

Tottenham wanamtaka mshambuliaji wa Porto Samu Aghehowa, 21, mwezi Januari, lakini wana wasiwasi watashindwa katika jitihada zao za kumnasa mshambuliaji wa Bournemouth Antoine Semenyo, 25, raia wa Ghana, huku Manchester City wakiwa nao kwenye mbio za kumnasa (Teamtalk)

Samu Aghehowa

Chanzo cha picha, Getty Images

Mlinzi wa zamani wa Real Madrid, Sergio Ramos, 39, anataka kurejea Ulaya mkataba wake na Monterrey ya Mexico utakapomalizika mwishoni mwa Desemba, huku AC Milan ikiwa miongoni mwa vilabu vinavyovutwa naye. (Calciomercato)

Nottingham Forest wanamvizia mlinzi wa Inter Milan Stefan de Vrij, 33, raia wa Uholanzi, ambaye mkataba wake na klabu hiyo ya Italia unamalizika majira ya kiangazi yajayo. (Football Insider)