Sababu za 'bingwa kibonde' Liverpool kuchapwa kila siku

Arne Slot appears deep in thought during Liverpool's 3-0 loss at Manchester City

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Arne Slot ataweza kurejesha kiwango cha Liverpool
    • Author, Umir Irfan
    • Nafasi, Football tactics correspondent
  • Muda wa kusoma: Dakika 6

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu England Liverpool walianza msimu vizuri, lakini sasa wamejikuta wakiwa chini ya msimamo nafasi ya 10 baada ya mechi 12.

Katika mechi zao saba za mwisho za ligi, Liverpool wamepata pointi tatu pekee, ambapo ni Wolves walio mkiani pekee waliopata pointi chache zaidi kipindi hiki. Jumamosi wakiwa nyumbani pia wamechapswa 3-0 na Nottigham Forest.

Hii inatokea licha ya Liverpool kutumia zaidi ya pauni milioni 400 kusajili nyota wakubwa katika dirisha la majira ya kiangazi.

Hivyo ni zipi sababu za kiufundi zinazowafanya Liverpool kuwa katika hali mbaya kwa sasa?

Kwa nini Liverpool wanapata shida kutengeneza mashambulizi kuanzia nyuma

Tatizo kubwa la Liverpool msimu huu linaanzia kwenye namna wanavyotengeneza mashambulizi kutoka safu ya ulinzi.

Kutokana na Trent Alexander-Arnold kujiunga na Real Madrid majira ya kiangazi na majeraha ya mlinda mlango Alisson Becker kwa zaidi ya wiki sita, safu ya ulinzi ya Liverpool imebadilika.

Giorgi Mamardashvili amechukua nafasi ya Alisson na jambo dogo lakini muhimu linalochangia matatizo ya Liverpool ni ukweli kwamba makipa hawa wana utofauti katika uwezo wao wa kutumia miguu.

Mamardashvili ni mguu wa kushoto, jambo linalomaanisha anacheza mipira fulani ambayo Alisson hangecheza.

Hii inabadilisha namna ambavyo Liverpool imeizoea ikimtumia Alisson na kipa msaidizi wa awali Caoimhin Kelleher, ambao wote wanatumia mguu wa kulia.

A...

Chanzo cha picha, Opta

Maelezo ya picha, Ramani kuonyesha pasi za Mamardashvili katika mchezo dhidi ya Manchester City wa Novemba 9 inaonyesha namna Liverpool inavyotengeneza mashambulizi yake zaidi upande wa kulia kutokana na mguu wake wa kushoto na namna City walivyokuwa wanawakaba.

Makipa wanaweza kucheza pasi fupi haraka zaidi wanapopiga pasi zao fupi kutokana na kunyumbulika kwa miili yao, hasa pasi za upande wa kulia.

Kwa Alisson, pasi hizi zingeelekezwa kwa Virgil van Dijk, beki mwenye uwezo mkubwa zaidi wa kujenga mashambulizi. Mguu wa kushoto wa Mamardashvili unapeleka mpira zaidi kuelekea upande wa kulia, ambako sasa wapo Ibrahima Konate na Conor Bradley au Jeremie Frimpong.

Kwa sehemu kubwa ya msimu huu, Liverpool wamekuwa wakijenga mashambulizi kwa pasi fupi na wamekuwa wakipata shida, hasa upande wa kulia.

Timu pinzani zimeifanya kazi hii kuwa ngumu zaidi kwa kuwakaba Liverpool kwa namna inayokata upande wa kushoto, hivyo kuwalazimisha kwenda kulia. Washambuliaji wamekuwa wakimuweka Van Dijk kwenye presha ili kupunguza ushawishi wake kwenye mpira.

A

Chanzo cha picha, BBC Sport

Maelezo ya picha, Haaland hapa anawalazimisha Liverpool kwenda kulia. Kipa anayetumia mguu wa kulia angeweza kumpasia Van Dijk lakini Marmadashvili anampasia Konate

Mpira unapokwenda upande wa kulia wa ulinzi, Liverpool hawana uwezo mkubwa wa kutoka kwenye presha bila Alexander-Arnold.

Kile ambacho Liverpool wanakikosa kwa kutokuwepo kwake kilielezwa hapa, lakini uwezo wake wa kutumia miguu yote miwili na utayari wa kupiga pasi za hatari, iwe kuingia ndani au nyuma, mara nyingi ulikuwa suluhisho lao la dharura.

Screengrab of Trent Alexander Arnold passing the ball to his central midfielder from right back using his left foot when Liverpool played Tottenham last season.

Chanzo cha picha, BBC Sport

Maelezo ya picha, Uwezo wa Alexander-Arnold wa kupiga pasi kwenda katikati akitumia mguu wake dhaifu ni kitu ambacho Liverpool wanakikosa katika kutengeneza mashambulizi msimu huu.

Uwezo wa Alexander-Arnold wa kupiga pasi kwenda katikati akitumia mguu wake dhaifu ni kitu ambacho Liverpool wanakikosa katika ujenzi wa mchezo msimu huu.

Uchunguzi wa wachezaji mmoja mmoja unaonyesha changamoto za Milos Kerkez kutokuweza kuficha nia ya pasi anazotaka kucheza kutoka beki wa kushoto. Bradley huonekana kucheza kwa kasi, lakini kupunguza mwendo wakati wa kujenga mchezo kunaweza kusaidia timu kutuliza presha na kuwa na umiliki salama zaidi.

Kuongezeka kwa kasi ya kujenga mchezo na kupungua kwa ubora wa pasi kutoka kwa safu ya ulinzi kumesababisha kupoteza mipira kwa urahisi na umiliki wa muda mfupi.

Kwa nini Liverpool wanaukosa ubora wa Salah?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mohamed Salah alihusika sana katika mafanikio ya Liverpool msimu uliopita, hivyo kwa nini Mmisri huyo amekuwa hafanyi vizuri msimu huu?

Upande wa kulia wa Liverpool msimu uliopita ulikuwa bora, ukiwa na Salah, Dominik Szoboszlai na Alexander-Arnold.

Uchambuzi wa Alexander-Arnold msimu uliopita unaonyesha kwamba sio ubora wake kwenye mpira tu uliovutia – bali pia harakati zake bila mpira zilimsaidia sana Salah.

Katika mchezo dhidi ya Bournemouth msimu uliopita, Alexander-Arnold mara nyingi alichukua nafasi ya juu kiukweli kama kiungo mshambuliaji katikati wakati mabeki walipokuwa na mpira. Hii ilimlazimu kiungo wa Bournemouth kushuka chini kumzuia.

Nafasi hii ilifungua njia ya pasi kutoka Konate kwenda kwa Salah, hivyo Mmisri alipokea mpira kwa urahisi.

Salah alipokea mpira akiwa chini zaidi, akimruhusu kugeuka, kuangalia mbele na kuwa mbali kidogo na beki. Mwelekeo huu humfanya awe hatari zaidi – kushambulia moja kwa moja, kudribble kwa kasi na kucheza pasi kuelekea ndani.

Screengrab

Chanzo cha picha, BBC Sport

Maelezo ya picha, Anavyojiweka Alexander-Arnold kunamuwezesha Salah kupokea mpira kwa wakati na nafasi

Manufaa mengine ya nafasi ya ndani ya Alexander-Arnold ni kwamba badala ya viungo wawili wa kati kuwa juu, yeye na Szoboszlai ndio waliokuwa maeneo hayo.

Hii iliruhusu viungo wawili wa asili wa kati, Ryan Gravenberch na Alexis Mac Allister kubaki nyuma ya mpira, katikati. Hii huongeza uimara wa ulinzi wakati wa kukabili mashambulizi ya kushtukiza.

Ikilinganishwa na msimu huu, matatizo yanakuwa wazi.

Mabeki wa pembeni wa Liverpool wanajikuta wakiwa pembeni mwa uwanja katika eneo la nusu yao (Liverpool), mara nyingi wakishindwa kuwapata wachezaji muhimu katikati. Njia ya pasi kutoka Konate kwenda Salah imekuwa ikizuiwa na idadi kubwa ya wapinzani katikati.

Mara kwa mara, mabeki wa pembeni hulazimika kumpasia Salah moja kwa moja. Hivyo Salah hupokea mpira akiwa na presha nyuma yake, hivyo kushindwa kugeuka na kushambulia. Hii inapunguza ufanisi wake.

Pia kuna viungo wachache katikati walioko kwenye nafasi ya kuzuia mashambulizi ya kushtukiza pindi mpira unapopotea. Tatizo hili la nafasi limekuwa mbaya zaidi kutokana na mabadiliko na mzunguko mkubwa wa viungo watatu wa kati – mabadiliko ya kimkakati ambayo hayajazaa matunda msimu huu.

Tatizo kubwa zaidi la ulinzi la Liverpool msimu huu

Liverpool walikuwa wakibanwa wapinzani kwa nguvu chini ya Jurgen Klopp, lakini chini ya Slot mbinu zimebadilika.

Sasa Liverpool hushambulia wakiwa na mfumo wa 4-2-4. Mfumo ambao Slot hupenda ni kuwa na mchezaji mmoja zaidi kwenye safu ya ulinzi dhidi ya washambuliaji wa wapinzani, yaani "plus one".

Mara nyingi wapinzani wana mshambuliaji mmoja na wachezaji wawili wa pembeni juu. Liverpool chini ya Slot huweka mabeki wanne nyuma ili kuwa na faida ya mchezaji mmoja.

Lakini athari yake ni kwamba Liverpool mara nyingi wanakuwa na mchezaji mmoja pungufu mbele waki-press dhidi ya wapinzani.

Screengrab of Liverpool's defensive shape against Chelsea this season showcasing how they leave an extra player back, leaving them numerically outnumbered at the front of the pitch.

Chanzo cha picha, BBC Sport

Maelezo ya picha, Liverpool ikiwa pungufu ya mchezaji mmoja mbele (eneo la rangi ya njano) kwa sababu wanakuwa na mchezaji mmoja zaidi nyuma (eneo la rangi nyeupe). Kwa mazingira haya yanamruhusu Marc Cucurella kupokea mpita katika nafasi ambayo Chelsea wanaonekana kuwa na mtu mmoja zaidi.

Kitendawili kikubwa cha ulinzi kwa Slot

Katika ushindi dhidi ya Arsenal mapema msimu huu, Liverpool walianza mchezo wakitumia "plus one" kwenye safu ya ulinzi. Hii ilimaanisha Arsenal walikuwa na mchezaji wa ziada wakati wanajenga mchezo.

Katika mfano hapa chini, Liverpool wana wachezaji wanne mbele na viungo wawili. Kama wanne hao wange-'press' pamoja, basi viungo wangepitwa kirahisi kutokana na nafasi ya kipekee ya Riccardo Calafiori.

A screengrab showing Arsenal building up from the back against Liverpool with seven players (four defenders and three midfielders) compared to Liverpool's six pressing players (four attackers and two midfielders) from the game this season.

Chanzo cha picha, BBC Sport

Maelezo ya picha, Calafiori ni mtu wa ziada Arsenal wakionekana wengi dhidi ya Liverpool kwenye kutengeneza mashambulizi, saba kwa sita

Arsenal walitawala kipindi cha kwanza kwa sehemu kutokana na faida hii, hivyo Slot akabadilisha hadi kukaba mtu kwa mtu kwa mtu kipindi cha pili kutatua tatizo.

Szoboszlai akapewa jukumu la kumkaba Calafiori, jambo lililosaidia Liverpool kutawala kiasi mchezo na kuonyesha uelewa wa Slot wa tatizo.

Hata hivyo, hili liliwafanya Liverpool kubaki pia mtu kwa mtu nyuma huko nyuma, kitu ambacho Slot hakipendi.

Katika mechi nyingi baada ya dhidi ya Arsenal, Slot amerudi kwenye mbinu yake ya awali, jambo lililorejesha tatizo lile lile.

Kushuka kwa kiwango si suala la kimbinu pekee

Haya siyo matatizo yote ya Liverpool msimu huu, lakini inaonyesha baadhi ya changamoto muhimu ambazo Slot na benchi lake la ufundi wanapaswa kuzishughulikia.

Liverpool pia wanapata shida kwenye mipira ya kutengwa na mipira mirefu (long balls), katika ligi ambayo inaipa kipaumbele aina hizi za mashambulizi.

Pia kuna ukweli usioweza kuepukika kwamba kifo cha kushtukiza cha mchezaji mwenzao Diogo Jota kimeathiri fikra na hisia za wachezaji na benchi la ufundi.

Kutumia fedha nyingi mara nyingi huleta wachezaji bora, ambao wanapaswa kuboresha matokeo. Lakini kwa kuzingatia mambo mengi yanayokosekana uwanjani na nje ya uwanja, kupata uwiano bora wa kuwaunganisha wachezaji wapya si kazi rahisi.