Virusi vya Corona: Uhamiaji wa nchini Marekani kusitishwa kutokana na janga la corona, asema Trump

Chanzo cha picha, AFP
Rais wa Marekani Donald Trump ametanagaza kuwa atasaini amri ya kuzuia kwa muda aina zote za uhamiaji nchini Marekani ili kupambana na virusi vya corona .
Katika ujumbe wake wa Twitter ameelezea kile alichokitaja kama "shambulio la adui asiyeonekana ", kama anavyoviita virusi vya corona, "pamoja na haja ta kulinda kazi za raia wa Marekani," bila kutoa maelezo zaidi.
Haijulikani kufikia sasa ni programu gani za uhamiaji ambazo zitaathirika, wakosoaji wake wanadai kuwa Trump anatumia janga la corona kuwafungia milango wahamiaji.
Hii inakuja wakati ikulu ya White House ikisema pia kwamba janga baya zaidi la virusi vya corona limepungua na shughuli zinaweza kuanza kufunguliwa nchini humo.
Marekani ina jumla ya wagonjwa wa corona 782,159 na vifo 41,816 kutokana na virusi hivyo.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe

Marekani tayari imekubaliana na Canada pamoja na Mexico kuongeza zaidi muda wa kuzuwia safari zisizo na muhimu baina ya mipaka yao hadi katikati ya mwezi Mei.
Safari pia zimezuwiwa kwa kiwango kikubwa kwa watu watu wanaotoka Ulaya na Uchina kuelekea Marekani, ingawa watu wenye vibali vya kazi vya muda, wanafunzi na wafanyabiashara wanaruhusiwa.
Tangazo hilo la rais linakuja wakati utawala ukitaka shughuli zifunguliwe katika baadhi ya maeneo ya Marekani ambako zilikuwa zimefungwa kutokana na janga la corona.

Sababu za hatua hiyo
Uchambuzi wa Anthony Zurcher, Mwandishi wa BBC Amerika Kaskazini
Juhudi za Donald Trump za uongozi kwa mitandao ya habari ya kijamii zinapaswa kuchukuliwa kwa kiasi fulani kama shemu ya ukweli. Taarifa juu ya marufuku ya muda juu uhamiaji wa aina zote, ilitangazwa saa chache kabla ya kabla ya saa sita za usiku siku ya Jumatatu ,utatoa mwangaza zaidi juu ya hatua na uhalali wa kisheria wa maamuzi yake.
Na bado sio siri kwamba rais na washauri muhimu , wamekua kwa muda mrefu wakiuangalia uhamiaji kama kitu kisicho na faida kwa taifa, bali kama jambo linalonyonya taifa. Na maandishi ya ujumbe wake wa Twitter, kwamba hatua hiyo ni muhimu si kwamba tu inalinda afya ya taifa bali pia "kazi za raia muhimu wa Marekani ", inasisitizia juu ya suala hili.
Kuna wasi wasi mdogo, kwamba kwa namna yoyote ile, hatua hii itapingwa vikali na makundi yanayounga mkono uhamiaji, baadhi ya maslahi ya kibiashara na wanaopinga fikra za rais.
Hilo huenda likawa ni jambo jema kwa Trump ambaye anapenda kuanzisha vita vya kisiasa na anayependa kuwakera wapinzazi wake pale inapowezekana.
Miaka minne iliyopita , rais alifanya kampeni katika mkutano uliokua ukipinga uhamiaji mkiwemo uhamiaji wa kudumu, uwe wa muda, na kupiga marufuku kuingia kwa Waislamu nchini.
Na sasa wakati akipigania kuchaguliwa tena amepata hatua nyingine za kushinda mapambano hayo.














