Virusi vya Corona: Kwa nini amri ya kutotoka nje inaweza isifanikiwe Afrika?

A Kenyan woman together with her son wear face masks during Easter Sunda

Chanzo cha picha, EPA

Mataifa mengi barani Afrika yameanzisha utaratibu wa kupiga marufuku ya kutotoka nje ikiwa ni jitihada ya kukabiliana na mlipuko wa virusi vya corona.

Lakini je, watu wenyewe wanahusishwa katika maamuzi haya kama yanaweza kufanyika kwao?

Mataifa ya barani Afrika yamejifunza namna ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kama maambukizi ya virusi vya Ukimwi na Ebola hivyo wanaweza kutumia uzoefu huo kukabiliana na madhara ya ugonjwa wa Covid-19.

Jambo muhimu ambalo jamii inapaswa kujifunza ni kutorudi nyuma katika mapambano ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.

Huu ndio uhalisia wa maisha.

Sign saying Stay Home

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Ni muhimu kubaki nyumbani katika kipindi cha mlipuko

Kwanza, mlipuko wa magonjwa ya kuambukiza huwa unakuja kitofauti katika jamii mbalimbali, kwa mujibu wa hali za watu husika wa eneo husika.

Jambo lingine ni hatua za kukabiliana na janga lenyewe kwa mfano amri ya kuzuia watu kutoka nje, inaweza kuchukuliwa bila watu kuridhia matokeo yake.

Ni pale tu wananchi wenyewe wanaposhirikishwa katika mipango na utekelezaji wake wa kukabiliana na mlipuko huo, ndio jitihada zinaweza kufanikiwa.

Maelezo ya video, Virusi vya Corona: Marufuku ya kutotoka nje ndio suluhu ya corona
Presentational white space

Maafisa wa afya walianzisha muongozo mzuri kwa umma wakati wa mlipuko wa Ukimwi: "Fahamu hali yako, jikinge na hatua za kukabiliana hili suala kisiasa."

Ni muhimu kufikiria kuwa Covid-19 si ugonjwa wa mlipuko unaopatikana sehemu moja bali uko dunia nzima, lakini jinsi ya kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo unabidi utofautiane kulingana na watu na eneo husika.

Kuna hatua za msingi ambazo ni moja kila sehemu.

Lakini kasi ya maambukizi inatofautiana kulingana na eneo na eneo.

Maeneo ya mjini yanaweza kuwa tofauti na maeneo ya kijijini.

Maelezo ya video, Virusi vya Corona: Jinsi marufuku ya misongamano inavyokumbana na vikwazo Afrika

Maambukizi yataenea tofauti pia katika maeneo ya kambi za wafungwa na watu wanaosafiri mara kwa mara.

Magonjwa barani Afrika yana changamoto tofauti

Katika ugonjwa huu mpya , jambo muhimu la kuzingatia ni jamii kubabidili mwenendo wa tabia zao kama vile namna ya kusalimiana, kukusanyika na watu , kuosha mikono au kuwa mbali na watu.

Wataalamu wanaweza kuweka miongozo yao kulingana na wastani wa tatizo na kile ambacho kinatarajiwa, lakini pale tu jamii ikielewa umuhimu wa hali ilivyo.

Bara la Afrika limekuwa na changamoto ya magonjwa tofautitofauti ukitofautiana na mabara mengine.

Kuna sababu nzuri za kuogopa ugonjwa wa Covid-19 ambao unaweza kuathiri wagonjwa wa kifua kikuu wapatao milioni 10 au wale ambao wana upungufu wa kinga mwilini na wale wenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Presentational white space

Kidogo kinachofahamika kuhusu maambukizi ya virusi vya corona yana maana gani kwa wagonjwa wenye malaria au wenye utapia mlo.

Kwa upande mwingine, Idadi kubwa ya watu barani Afrika ni vijana.

Sababu kubwa iliyofanya Italia kuwa na idadi kubwa ya vifo kutokana na maambukizi ya corona ni kuwa na idadi kubwa ya - 23% ya idadi ya watu wa Italia wana miaka zaidi ya 65 - na ndio wako kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi ya ugonjwa huo.

Utofauti wa asilimia mbili kwa idadi ya wazee ambao wana umri zaidi ya miaka 65. Kwa sababu hiyo tu idadi ya vifo ikutokana na virusi vya corona naweza kuwa ya chini katika bara hili.

Iko wazi kuwa kila taifa la Afrika, linapaswa kubuni namna nzuri ya kukabiliana na janga hili kulingana na uhitaji wake.

Kwa nini serikali zinapaswa kuzungumza na watu

Serikali hazina takwimu au mbinu za kutekeleza kile ambacho kinatarajiwa kutokea na hawana wataalamu wa kutosha kuweza kukabiliana kwa haraka na janga hili.

Lakini kuna njia ambazo zina unafuu, nyingine zimejaribiwa tayari kwa wananchi kujulishwa.

Madaktari na wataalamu wa afya wanaweza kueleza ukweli kuhusu masuala ya afya, jamii inaweza kueleza uhalisia wa mazingira yao na mambo gani yaliwezekana kufanyika kwao na kufanikiwa.

A trader sleeps by his melon stall in Kampala, Uganda - Wednesday 8 April 2020

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Muuzaji matunda nchini Uganda akiwa amepumzika huku akisubiri wateja
Presentational white space

China, Ulaya na Amerika Kaskazini, wote wamekabiliana na janga la mlipuko huu kwa kuweka amri ya watu kutotoka nje.

Serikali za Afrika zimefuata hatua hiyohiyo ya kuweka katazo la watu kutotoka nje lakini inawezekana kuwa njia hiyo isiweze kufanya kazi katika bara la Afrika.

Ni mataifa machache kama Afrika kama Rwanda na Afrika Kusini, yameweza kutekeleza hatua hiyo.

Kwa wengi ambao wanategemea kipato cha kila siku kununua chakula, kwa siku chache tu hali ya umaskini na njaa .

Watu wengi tayari wameathirika katika ukosefu wa ajira, upatikanaji wa fedha, ukame ambao umesababishwa na nzige.

Amri ya watu kutotoka nje imeweza kutishia jamii kwa kuongeza idadi ya watumiaji dawa za kulevya, maambukizi ya kifua kikuu maambukizi ya virusi vya ukimwi na magonjwa mengine.

Kama kufungia watu ndani kunaweza kutekelezeka, msaada wa dharura unahitajika.

Amri ya kutotoka nje ilivyoshindwa kufanya kazi

Hatua hii imepelea watu kukosa ajira zao au kushindwa kupata fedha za kujikimu na familia zao katika mataifa ya Ulaya na Marekani kwa ajili ya kununua chakula na kununua mafuta.

Baadhi ya mataifa kwa mfano Uganda na Rwanda, wanatoa chakula cha bure.

Ghana imetangaza kuwa huduma ya umeme, maji ni bure na kodi itaondolewa.

Lakini serikali za Afrika hazina ufadhili wa kutosha kuweza kuendelea kutekeleza hatua hiyo bila kupata msaada wa kimataifa

A section of the Ibadan expressway is deserted by motorists following the lockdown by the authorities to curb the spread of the COVID-19 coronavirus in Lagos, on March 31, 2020

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mji wa Lagos, huwa una pilikapilika nyingi lakini uko kimya sasa

Kama mahitaji muhimu hayawezi kupatikana kutokana na amri ya katazo.Maskini wanaweza kuona bora wapate maambukizi kuliko kubaki na njaa.

Wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa Ebla, wakati ambao serikali ya Liberia ilipoamrisha askari kuutenga mji mkuu, Monrovia, mwaka 2014, ilibainika kuwa siku chache walizofungia watu hakuna mabadiliko yoyote yaliyotokea katika kuzuia maambukizi.

Kwa haraka serikali iliamua kuwaambia viongozi wa jumuiya kubuni namna nzuri ambayo itapitishwa kama sera itakayoweza kuwawezesha kukabiliana na na ugonjwa

Somo ambalo sekta ya afya ilijifunza kutoka Sierra Leonepia.Kwamba jamii ilishirikishwa kubuni hatua nzuri ya kuzuia maambukizi na wakati huo , mashirika ya kimataifa yalichukua

Jitihada gani zinahitajika barani Afrika

Somo ambalo mataifa ya barani Afrika yanapaswa kujifunza ni kuchukua hatua za haraka na kuwashirikisha jamii.

Mfumo wa afya wa Afrika uko nyuma, na ugonjwa wa Covid-19 dunahitaji hatua za dharura kukabiliana nao na kuanzia kwenye serikali.

Hospitali za Afrika zinahitaji kuwa na mahitaji muhimu kama ya vipimo vya kupimia, vifaa vya usafi , vifaa vya watu kuikinga na wahudumu wa afya kujikinga wakati wakiwahudumia wagonjwa, vifaa vya kusaidia watu kupumua.

Kuna uhaba wa vifaa tiba duniani kote sasa, inasikitisha kuwa hata mataifa yaliyoendelea nayo yanapambania kupata mahitaji - hali itakuwa ngumu kwa matifa ya Afrika kuwa katika mstari huo huohuo.

Lakini mashirika ya kimataifa yamezitaka serikali za Afrika kuainisha mahitaji yake ili waweze kusambaza.

Hatua nyingine ni kujenga vituo vya huduma ya afya ili kuwahudumia wagonjwa wa mlipuko jambo ambalo bado, ni wiki ya ya nane sasa tangu ugonjwa huo kuingia katika jamii hii.

Ni muhimu sasa kungekuwa na maturubai katika maeneo ya shule ili kujiandaa kwa janga hilo.

A medical staff member works at the yet to be used field hospital build to treat a large number of patients due to the spread of the coronavirus disease (COVID-19), at the Aga Khan University Hospital in Nairobi

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wodi mpya ya wagonjwa wa Corona, nchini Kenya

Hakuna hospitali au viituo vya afya vya kutosha kwa wahudumu wa afya kuweza kuhudumiwa wagonjwa wa Covid-19 bila kuingilia katika hospitali za kawaida kuwahudumia wagonjwa wengine, wamama wajawazito.

Kuchanganya wagonjwa wa mlipuko na wagonjwa wengine kunaweza kuhatarisha maambukizi kukuwa zaidi na vifo kuongezeka.

Jamii inaweza kusaidia kwa kujitolea sehemu ya kujenga maturubahi na kuweka kambi za muda kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa corona kwa mujibu wa mtaalamu wa afya na usalama.

Ni changamoto kubwa kufanya uchumi ,uendelee kufanya kazi na kuachilia mbali changamoto ya njaa.

Mataifa ya Afrika hayawezi kufunga soko lake la vyakula ambavyo havijasindikwa, la sivyo watu watakufa kwa njaa.

Lakini waendaji sokoni wanaweza kupunguza misafara ya sokoni ili kupunguza hatari ya maambukizi. Kwa kufuata muongozo uliowekwa wa kujizuia kuwa katika maeneo ya msongamano wa watu, kuwa wasafi na kuzuia kushikana.

Pendekezo lingine ni kila nyumba kununua chakula kwa wingi .

Baadhi wa mataifa yalihamia kwenye mihamala ya simu badala ya fedha taslimu ambo ambalo linawezekana kwa baadhi ya nchi na kwingine lisiwezekane.

Coronavirus
Banner

Jambo la muhimu ni si kuainisha mawazo mazuri ya kuyafuata lakini ni wafanyabiashara, wateja na mamlaka kukaa kwa pamoja kujadili ni njia gani nzuri kuifuata.

Wao ndio wanaua njia sahihi inayoweza kufanya kazi katika mazingira yao na namna watakavyoweza kufuatilia kwa karibu utekelezaji wake.

Amri ya kutotoka nje imeweza kusababisha majanga makubwa katika jamii. Si tu katika upande wa umaskini , njaa lakini pia imehatarisha namna ya kuzuia maambukizi kusambaa.

'Hatuna muda wa kupoteza'

Leo , wataalamu wa afya wamependekeza kuwe na namna mbadala na kuepuka suala la kufungia watu.

Hii njia inaonekana kutofanya kazi kwa sababu hawajawauliza wananchi maoni yao ya namna ya kukabiliana na janga hili.

Hakuna muda unaopotea kwa kuwauliza viongozi wa kijiji au mitaa nini kinaweza kufanyika sasa.

Uzoefu uliopatatikana wakati wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kama Ukimwi na

Ebola ni somo tosha kwa waafrika.

Wananchi wenyewe sio tatizo bali wao ndio suluhisho.

Uzuri watu huwa wanaifunza haraka sana wanapopewa maagizo na wako tayari kufikiria kulinda jamii zao.