Virusi vya Corona: Mgongano kati ya haki za raia na sheria za kudhibiti maambuki Afrika

Polisi wa Uganda wakiwapiga wafanyabiashara wa mtaani waliokataa kutoka mtaani

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Polisi wa Uganda wakiwapiga wafanyabiashara wa mtaani waliokataa kutoka mtaani

Askari wenye silaha wamekua wakiwapiga na kuwarushia maji ya gesi watu katika maeneo mbalimbali ya mataifa ya Afrika na wengine kufikia hata kuwauwa ili kuhakikisha kuwa hatua za kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa corona zinachukuliwa.

Hatua zilizochukuliwa na polisi na askari, zimezuwa mjadala juu ya uhuru wa mtu binafsi na haki za binadamu, na kwa upande mwingine ni kuwa wanapaswa kuwalinda watu ili wasipate maambukizi ya virusi vya corona.

Kutoka na janga la kiafya, baadhi ya serikali za Afrika wameanzisha sheria ya dharura ya adhabu mtandaoni.

Angalizo limetolewa na wanaharakati wa haki za binadamu kuwa janga hili likiisha ,hatua hizi zinaweza kunyima watu uhuru wa masuala muhimu.

Amri ya kutotembea usiku imeweka nchini Kenya

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Amri ya kutotembea usiku imeweka nchini Kenya

Amri ya kutotoka nje usiku nchini Kenya.

Mamlaka imesema kuwa amri ya watu kutotoka nje, kutokuwa katika mikusanyiko ya watu inalengo la kuokoa maisha ya watu lakini hatua hizo tayari zimegharimu maisha ya watu.

Kijana mwenye miaka 13, raia wa Kenya aliyekuwa akicheza katika maeneo ya nyumbani kwao jijini Nairobi, alipigwa risasi na polisi na kufa kwa sababu alikuwa nje.

Vifo vingine vitatu vimeripotiwa kikiwemo cha dereva wa pikipiki aliyepigwa na polisi, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.

Rais Uhuru Kenyatta amewaomba radhi wakenya wote, kwa madhara ambayo yametokea kutokana na hatua walizochukua askari.Hatahivyo rais amewataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kufuata maaagizo waliyopewa ili kuhakikisha kuwa maambukizi ya corona yanazuiliwa.

Wapenzi wa jinsia moja

Nchi ya jirani ,Uganda,shirika la Human Right Watch limetoa madai kuwa polisi walikuwa wanatumia nguvu za ziada kuwapiga wafanyabiashara ndogondogo wa matunda na mbogamboga pamoja na waendesha bodaboda.

Polisi Afrika kusini wanafanya operesheni maalum kuzuia watu kutoka nje

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Polisi Afrika kusini wanafanya operesheni maalum kuzuia watu kutoka nje

Polisi Afrika kusini wanafanya operesheni maalum kuzuia watu kutoka nje

Hata hivyo polisi waliwakamata watu 23 wakati katika operesheni hiyo na hao wote ni wapenzi wa jinsia moja ambao hawana makazi na kuwashutumu kuwa wamekiuka maagizo kwa kuzurura na hivyo kueneza maambukizi.

Haki za binadamu ni muhimu kuzingatiwa wakati serikali ikichukua jitihada za kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huu, haswa kwa watu ambao hawana uwezo na hawana nyumba za kuishi kama vijana wa mtaani na wafanyabiashara,"HRW ilisema.

Katika hatua hiyo ya kukosoa hatua zinazochukiliwa na maafisa, askari 10 walishtakiwa kwa unyanyasaji kwa kumpiga mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 38 na kumlazimisha aogelee kwenye matope huko maeneo ya magharibi, Elegu.

Maafisa hawajakiri makosa yao bado.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video, Coronavirus: Utajuaje kuwa umeathirika na virusi?

Wakati Afrika Kusini kumerikodiwa kuwa na visa vingi vya ugonjwa wa Covid-19 barani Afrika, watu wapatao wanane wameuliwa na polisi tangu operesheni hiyo ianze Machi 26, Mkuu wa polisi wa masuala ya uchunguzi ameeleza.

'Bunduki zenye risasi'

Karibu mataifa yote barani Afrika yanapambana kuzuia maambukizi ya virusi vya corona huku kukiwa na na visa 10,000 vimethibitishwa kuwepo na wakiwa na hofu ya ugonjwa huu kusambaa zaidi.

Mataifa mengi ya Afrika hayana mfumo mzuri wa Afya ambao unaweza kukabiliana na janga hili la afya.

Makundi ya upinzani nchini Ghana yanahofia sheria mpya inayompa mamlaka rais kuweka amri ya watu kutotoka nje.

"Tunataka marais watumie mamlaka ya dharura katika katiba kuwa rais atatakiwa kuhudhuria bunge kila miezi mitatu ili wabunge waweze kuwasiliana naye juu ya hatua ambazo zinahitajika kuchukuliwa," Ras Mubarak, mbunge wa Upinzani chama cha National Democratic Congress, aliiambia BBC.

" Sheria mpya inamruhusu kuwa na silaha na kutumia anavyojisikia, haswa katika kuwazuia watu kutotoka."

Waziri wa sheria nchini bwana Gloria Akuffo alitetea sheria hiyo na kusema kuwa ilikuwa muswada maalum kwa ajili ya kusaidia taifa kulilinda kiafya lakini pia kwa manufaa ya siku zijazo".

coronavirus

Taarifa zaidi kuhusu virusi vya corona:

coronavirus

'Wakati Muafaka'

Mataifa mengine yalikuwa na wasiwasi huohuo.

Walimkosoa rais wa Malawi bwana Peter Mutharika kuwa anatumia mlipuko wa ugonjwa wa corona kutatua matatizo yake ya kisaisa ".

"Serikali itataka kutumia sababu ya maambukizi ya corona ili kuongeza muda wao wa kuwa madarakani," Gift Trapence,kiongozi wa shirika la kutetea haki za binadamu( Human Rights Defenders Coalition), ameiambia BBC.

Bwana Mutharika, ambaye mwezi Julai mwaka huu atarudia kugombani a nafasi ya urais ametangaza hali ya dharura katika taifa lake.

Mamlaka mapya yanamruhusu kutoruhusu mkusanyiko wa watu wengi.

"Wanafurahia kuwa hali hii ya corona kwa sababu wanataka kuitumia ili wabaki madarakani," bwana Trapence alisema.

Waziri wa habari nchini Malawi bwana Mark Botomani amekanusha madai hayo na kutaka yapuuzwe.

Ethiopia imetangaza hali ya tahadhari

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ethiopia imetangaza hali ya tahadhari

"Lengo letu kama serikai ni kutaka kuweka mazingira ambayo yatamlinda kila mtu na afya yake," waziri alisema.

Taifa ambalo ni la pili kwa kuwa na idadi kubwa ya watu, Ethiopia, limetangaza hali ya dharura na kuhairisha uchaguzi wa rais mpaka mwezi Agosti kwa sababu ya mlipuko wa corona.

Picha;Ethiopia ni taifa lenye idadi kubwa ya watu Afrika, limetangaza hali ya dharura

Waziri mkuu ambaye ni mshindi wa Nobel Prize bwana Ahmed Abiy alisema kuwa walijadiliana na upinzani ili kupanga namna ya kukabiliana na janga hili la corona, na hivyo kukubaliana kuwa uchaguzi utabidi uchelewe kidogo.

Ingawa wapinzani bado walisema kuwa tamko la hali ya dharura lisitumiwe vibaya.

Tahir Mohammed, kutoka chama chama cha National Movement of Amhara, alisema kuwa wana haki ya kufahamu kipi ambacho wanaruhusiwa kukifanya na kipi hawaruhusiwi kufanya.

"Tunachoona sasa ni kuwa serikali inaangazia manufaa ambayo wanaweza kupata," aliiambia BBC.

Magufuli akosolewa

Kundi lingine la haki za binadamu wamekuwa na wasiwasi kuhusu watu wanaolengwa na ambao wanakosoa maagizo ya maafisa kuhusu namna namna ya kukabiliana na janga la corona.

Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) imefungia vituo vitatu vya TV kwa kurusha matangazo ambayo yanasema tofauti na kile ambacho rais alimaanisha katika kukabiliana na virusi vya corona.

TCRA haikufafanua makosa yao lakini iliripoti kuwa walimkosoa rais John Magufuli kwa kusema kuwa makanisa yasifungwe.

Waandishi 10 ambao waliandika madhara yaliotokana na amri ya nchi kufungwa walipigwa na maaskari, Robert Sempala, kutoka Human Rights Network for Journalists nchini Uganda, aliiambia BBC.

Wakati Jumuiya ya kulinda waandishi nchini Afrika Kusini imeeleza kuwa sheria mpya ya kutuma taarifa ambazo si sahihi zinamuweka mtu kwenye madai ya jinai.

Simu za mkono kufuatiliwa

Haki ya kuwa huru inawapa wasiwasi baadhi ya watu.

Wanaharakati wanataka watu wataarifiwe kama simu zao zinafuatiliwa

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wanaharakati wanataka watu wataarifiwe kama simu zao zinafuatiliwa

Mamlaka ya Kenya imekuwa ikifuatilia simu za mikononi za watu ambao wanahisiwa kuwa na ugonjwa wa Covid-19 ili kuweza kuwatenga kwa muda wa siku 14, alisema msemaji wa serikali , Cyrus Oguna.

"Tunataka kuwafahamu ni kina nani, na wako wapi,"Bwana Oguna alisema, na kuongeza kuwa program ya simu imetengenezwa ili taarifa muhimu ziweze kupatikana.

Wakili mmoja nchini Kenya ambaye amebobea mambo ya usiri ,bwana Mugambi Laibuta alisema kuwa uhuru ni jambo ambalo mtu hawezi kuliingilia , watu wanapaswa kupewa taarifa kuwa wanafuatiliwa na namna taarifa zao zitakavyotumika.

Afrika Kusini pia inatumia simu za mikononi kutoka makampuni mbalimbali kuweza kuwafuatilia watu ambao walihusiana na wagonjwa wa Corona.

Msemaji wa Umoja wa mataifa kwenye kitengo cha uhuru ,Bwana David Kaye, alisema kuwa anaelewa kwa nini serikali imeamua kutumia hatua hizo ili kukabiliana na janga hili la afya.

Kwa hali ilivyo kwa sasa ni ngumu kuhoji kwa nini.

Lakini kuzuia matumizi ya mamlaka vibaya , sheria zote mpya hazitasalia wakati ambao janga la corona litakuwa limeisha, aliongeza.