Tetesi za soka Ulaya Jumapili: Barcelona inamtaka Marcus Rashford kusalia katika klabu hiyo

Chanzo cha picha, Getty Images
Barcelona wanamtaka Marcus Rashford, 28, kusalia katika klabu hiyo zaidi ya muda wa mkopo wake kutoka Manchester United. (Athletic - Subscription Required)
Aston Villa wanatazamia kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Tammy Abraham, 28, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Besiktas kutoka Roma msimu huu. (Telegraph - Subscription Required)
Manchester United wanatumai kuwashinda Arsenal kumsajili mchezaji wa Blackburn Rovers na Uingereza Igor Tyjon, 17. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Newcastle United wanampima beki wa kati wa Atalanta na Italia Giorgio Scalvini, 22, kufuatia jeraha la mlinzi wa Uswizi Fabian Schar, 34. (Teamtalk)
Chelsea 'imewapita' wapinzani wao katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid na Brazil Vinicius Jr. (Fichajes - In Spanish), mwenye umri wa miaka 25.
Mkufunzi wa Crystal Palace Oliver Glasner anaongoza orodha ya makocha wanaotarajiwa kuchukua mikoba katika klabu ya Manchester kwa mkataba wa kudumu . (Caughtoffside),

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati huo huo, United wanatumai kuwa na ufafanuzi kuhusu nani ataiongoza timu hiyo kwa muda wote uliosalia wa msimu mapema wiki ijayo. (ESPN)








